ephen_
JF-Expert Member
- Oct 28, 2022
- 14,949
- 54,485
Beautifull message!Maisha ni safari,kuna mnaosafiri kwa ndege,wengine kwa miguu,ila wote tunaelekea sehemu moja. Usitishwe na umbali wa unakoenda,tiwa nguvu na ulikotoka,nia ndio kila kitu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Beautifull message!Maisha ni safari,kuna mnaosafiri kwa ndege,wengine kwa miguu,ila wote tunaelekea sehemu moja. Usitishwe na umbali wa unakoenda,tiwa nguvu na ulikotoka,nia ndio kila kitu
NakujaNilizaliwa miaka kadhaa iliyopita. Katika familia ya watoto 7, mimi nilikuwa wa 6.
Kama watoto walivyo, nilikuwa mtundu kiasi ila sio mtukutu. Nakumbuka nikiwa darasa la 5,niliitwa mbele na ticha nikafanye swali la hesabu. Nikafanya swali kwa mbwembwe, nilikuwa nasumbuliwa na mafua, kabla sijaondoka pale mbele nikatoa leso ili nijifute. Wakati naitoa, kibox cha condom kikaanguka, darasa zima full kicheko. Ticha wa mathe ndio ticha wa nidhamu..nikaambiwa nitangulie ofisini.
Nikala bakora zangu za kutosha, kisha ndio nikaombwa maelezo, kila nikijitetea hawanielewi. Ukweli sio kwamba nilikuwa na dem au nilishaanza mapenzi, ni ile tu utoto utoto, unaokota kibox cha condom alaf unakaa nacho uangaliage zile picha. Kesi iliisha baada ya mzazi kuitwa.
Miaka ikakata, siku zikaenda. Darasa la saba mwishoni, wakati natoka kujisomea nikiwa na wenzangu wawili, ghafla tukasikia miguno kwenye darasa moja, kuchungulia tunakuta mlinzi wa shule yupo na muuza ubuyu [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]. Jamaa akatukimbiza maana ndio alikuwa
anajiandaa kupiga show alaf tumemtibulia.
Kitoto toto, tunakimbia huku tunacheka, nikaenda kuliparamia lori la mchanga wakati navuka barabara. Nikapelekwa hospital na kushonwa nyuzi 18,maana nilipasuka kichwani na usoni. Nikauguza majeraha, baada ya miezi kadhaa nikapona.
Baada ya kumaliza la saba, wazee wakaona nisisome shule za day, wakaamua kunipeleka seminari huko mkoani Iringa, mbali kabisa na mkoa wangu. Sijawahi ona shule ambazo wako strict kama seminari. Sema siku zikakata pia, wakati nipo kidato cha 3,hata mawazo sijui yalitokea wapi, me na rafiki yangu Shedy tukapanga tuuze nguruwe wa kanisa.
Nakumbuka tulivibana vizuri ili visitoe sauti (vitoto viwili),kumbe wakati tunaishia, kuna sister akatuona (aliutambua mzura wangu). Wala hatukupigwa, tuliambiwa tutaje tulipowapeleka ili tusamehewe. Tukataja, wakafatwa. Tukashangaa wik end wazazi wetu wamefika, wakakabidhiwa barua zetu za kufukuzwa shule, tukaambiwa tusepe.
Mshua aliongea sana siku hiyo, njia nzima hadi tunafika home. Kwanza hakuninunulia chochote cha kula njiani, maji nilikunywa kwavile yanatolewa ndani ya bus. Kufika home,ilifanywa mipango nikajiunga na shule fulani ya private ili nimalizie O level. Nikiwa kidato cha 4,me na mdogo wangu ndio tukafanya ule msala wa kumfungia dingi kwa nje,alaf tukala ndizi zote.
Kufupisha,fatisha hii link kusoma kilichotokea maana nilishawahi kuandika hiki kisa:
Wanangu na nyie mtazaa tu
Wakati dingi anatwambia hii kauli mimi na mdogo wangu, hapo alikuwa amevimba kwa hasira akiwa hana cha kufanya. Nakumbuka enzi hizo na mdogo wangu, mimi nikiwa kidato cha nne, mdogo wangu akiwa cha 3. Tulikuwa watundu japo sio watukutu. Kuna siku tuliondoka home bila kuaga, alaf kuna kazi...www.jamiiforums.com
Nikamaliza form 4,majibu yakatoka. Nakumbuka nilipata 3 ya mwisho mwisho huko. Nilikuwa napenda sana hesabu,ila cha ajabu nilipataga D. Na post zilivyotoka nikapangiwa HKL. Afadhali History,sikuwahi kulipenda somo la Kiswahili wala English,leo hii nikasome vishazi na ngeli shurutia ambazo nilivutwa sana masikio lakini sikuzielewa? Nikampanga faza anipeleke private Advance, akagoma. Msimamo wangu ukabaki me HKL siwezina sitaki. Faza akakausha. Baada ya wiki akaniita, akaniambia kati ya vitu viwili kimoja lazima nikiweze "KUSOMA HKL AU KUJITEGEMEA". Kikao kikaishoa hapo, nikaambiwa nikafikirie.
Nikiwa peke yangu chumbani, nikawa natafakari mavitabu, tamthilia, riwaya, ushairi ntakayoenda kusoma Advance, nikaona ngoma nzito ikiwa Mabala the Farmer kilikuwa kinanitoa jasho. Wiki moja baadae mshua akaniita tena, akanipigia hesabu zote za gharama zinazohitajika kuanzia nitakapoenda shule, alaf akanikabidhi cash pamoja na joining instructions ya shule. Akasema
"Vitu vyote utakavyohitaji kununua vimeandikwa humo na hela hii hapa, shule inafunguliwa tarehe 21,itakapofika siku hiyo nisikuone hapa kwangu, either uende shule au hiyo hela iwe mtaji wako wa kuanzia maisha"
Kikao kikaishia hapo. Ndani naona hapakaliki, nikaenda uwanjani kuangalia mpira ili kupoteza mawazo. Siku kama mbili mbele nikiwa nimekaa na washkaji, zikaanza story kuhus Dar es salaam. Kwamba ukijituma, na kuwa mjanja mjanja unafanikiwa. NIKAPATA WAZO LA KWENDA DAR.
Tarehe 15 /05 nikapanda bus kwenda Dar. Kabla sijatoka toka, Maza aliniuliza kama naenda shule, nikamwambia hapana, nachukua uelekeo mwingine.
Nakumbuka Dar es salaam tuliingia mida ya saa tano usiku. Bus ilisimama nikaona watu wanawahi kushuka, na mimi nikabeba vitu vyangu nikashuka. Kufika chini nauliza hapa ndio ubungo? ( Ndio sehem pekee niliyokuwa naijua) . Jamaa akanijibu "Hapa Mbezi dogo". Nikapaniki. Ikabidi nitafute sehemu nikae chini nitafakari vizuri. Kuna gari ilikuwa imepaki, nikakaa kwa chini, nikijiuliza nafanyaje.
Nilikuja kugundua badae chini ya lile gari kumbe kuna watu ndio sehemu yao ya kulala, na niligundua baada ya kile kifurushi changu nilichoweka chini kutoweka "NILIDATA"
•••••••• •••••••••• •••••••• •••••
Kwenye kile kifurushi ndio kulikuwa na nguo zangu pamoja na hela. Nikajaribu kuulizia, hakuna aliyenijali, naishia kutukanwa tu kuwa nawarushia stimu.
Mpaka kuna kucha, sikuupata mzigo wangu. Kuna Mzee mmoja ndio alinionea huruma akaninunilia chai na kunipa nauli ya kunifikisha ubungo, maana jamaa aliyetarajia kunipokea ilibidi nikutane nae ubungo. Kwavile namba zake nilikuwa nazo kwenye karatasi, niliongea nae kwanza kupitia simu ya yule mzee na kumuelezea kwa ufupi yaliyotokea.
Nikapanda daladala hadi ubungo. Kufika, nikaingia hadi ndani mule, nikaazima simu ya mtu, nikampigia tena jamaa yangu kumwambia kuwa nimefika. Wakati namsubiria, nikajiegesha sehemu.
Nikiwa pale, nilishuhudia tukio ambalo siwezi kuja kulisahau. Mbele yangu kulikuwa na Mwanaume wa makamo, kwa mavazi yake ni kama mchunganji, alikuwa anaongea na simu. Akatokea mtu mwingine kwa nyuma yake amebeba makaratasi kibao,ameyabana kwapani huku akiwa anakunywa maji ya uhai, yalipobaki nusu akaenda na kuyamwaga nyuma ya yule mchungaji, kisha akasubiri. Mchungali alipomaliza kuongea na simu, lile jamaa likamuuliza "Nani aliyekuruhusu kukojoa eneo ili?"
Mchungaji akashangaa, nahisi akumuelewa jamaa, ila alipotaka kuondoka, wakaongezeka wengine. Kuna mmoja akampiga kofi, yule aliyemwaga maji akamuuliza " Yani unakojoa eneo la wazi alafu unakuwa mkali?, Twende nae ofisini" Mchungaji akapaniki, wakamwambia atoe faini au akalale ndani. Mchungaji kujisachi, hela hana, atoe simu ili ampigie ndugu yake, simu hakuna. Mchungaji akalia. Ikabidi waazime simu, akampigia ndugu yake ili aje na hela ya faini.
Japo mchungaji alidata, ila mimi nilidata mara 100 zaidi yake. Ikabidi niweke vocha kwenye simu ya mtu tena, piga sana namba ya mwenyeji wangu ila haipokelewi, mwisho wa siku ikawa haipatikani tena. Kucheki muda,saa moja kasoro usiku. Nikazidi kudata.....
***** ***** ******* ******* ******
Imeendelea post #27
Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...
Du baada ya kudata kilitokea Nini?Nitakwambiawww.jamiiforums.com
Imeendelea tena post #68
Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...
Okkky, lakini umesema bomba lilikuwa limefukiwa Presha ya kuna muda ilizidi kwa hiyo sehemu yenyewe ikawa na maji, lakini cha ajabu uliweza kupitisha moto kutanua bomba! Pia kama tunavyojua hata kwenye maisha ya kawaida bomba haliwezi kukatika hapo hapo halafu uunganishe hapo hapo, i mean ni...www.jamiiforums.com
Imeendelea tena post #137
Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...
Hi chai hii Akaweka vocha na wakati aliibiwa mbezi hela[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] hela aliyonipa mzee baada ya kuninunulia chai asubuhi itakuwa uliichukua ww. Anyway shukrani.www.jamiiforums.com
Imeendelea tena post #177
Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...
Tiririka mkuu nakufuatilia kwa umakini sanawww.jamiiforums.com
Imeendelea tena post #208
Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...
Mabaharia hua hawafeli hata siku mojaNi kweli mkuuwww.jamiiforums.com
Imeendelea tena post #306
Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...
Kwa uandishi huu ungeenda HKL ungekuwa T.OHahahawww.jamiiforums.com
Imeendelea tena post # 386
Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...
Story nzuri ila ya uongo...huyu mchizi story zake za nyuma alishasoma tuition kwa mudy mchikichini na kasoma azania kama sijakosea hapo hapo leo hii alikuwa hapajui dar...all in all muandishi mzuri...big up brodawww.jamiiforums.com
Imeendelea tena na kuisha katika post #486
Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...
Yangu je??Yours is absolutely fantabulous!! There is nothing to compare with....www.jamiiforums.com
3Sehemu ya 3:
Tuendelee sasa..
.....Maana yule Mzee aliporudi, kabla hata sijamsalimia aliniuliza namdai kiasi gani? Tukapigiana hesabu akanipa changu alaf akaniambia "Fanya haraka utoke nataka kufunga geti tulale"
Sikujifikiria sana, kama niliweza kuondoka kwetu sembuse hapa? Nikabeba vyangu nikatoka. Hapo ilikuwa majira kama ya saa tatu usiku. Nikajichanganya mtaani. Niwe muwazi, pamoja na kukaa sana Dar ila watu wake sijawahi kuwaelewa. Kila mtu ni mjanja mjanja na anajua kila kitu,hakuna siku niliyotoka nje usiku nikakuta watu wamelala,mda wote wanapirika pirika tu. Pia hata mtu usiyemdhania anaweza akakuibia au kukudhurumu. Nasema hivi kwasababu ya kilichonikuta nilivyorudi mtaani. Nilikuwa natembea mdogo mdogo lengo ikiwa nielekee sehemu inaitwa Kariakoo maana niliambiwa huko kuna kila kitu japo sikuwahi fika. Kutokana na kubana bajeti sikutaka kupanda gari maana hela yenyewe ya ngama.
Kuna sehemu kule Dar panaitwa kwa Mnyamani. Maeneo yale nilikutana na watu kama wa 5 wakiwa wameshika fimbo, wanajiita sungusungu. Walinisimamisha na kuanza kunihoji, muda ule. Nikajaribu kutoa maelezo yangu, ila hawakutaka kunielewa. Watu wa Dar wanaongea haraka haraka sana hadi wakaanza kunichanganya. Naongea neno moja, wao washao gea 10.
Sijawahi kuona sungusungu anamsachi mtu, wala kumpiga mtu. Wakachukua hela zangu, bahati nzuri sikuziweka zote pamoja, nikabaki na kiasi kidogo. Waliponiacha, nikatembea hadi sokoni buguruni, nilipoona watu wengi wengi, nikaweka kambi pale kwa mzee aliyekuwa anauza kahawa. Kulipokucha nikapata kibarua cha kushusha matikiti. Hapo kidogo nikapata vijihela. Sikwenda tena kariakoo, nikaweka kambi hapo. Mida ya mchana, kazi hakuna ikabidi nitulie kwenye kijimgahawa cha mama mmoja hivi huku nakunywa soda maana hawaruhusu kukaa bure. Wakati nainywa soda yangu taratibu ili isiishe, kwenye tv kulikuwa na kipindi cha maswala ya shule (nishakisahau jina) ila channel ni Star Tv. Yani kile kipindi cha siku hiyo kama kilinilenga mimi, maana somo lilikuwa Kiswahili, maswala ya sentensi sentensi. Yule ticha alikuwa anafundisha maswala ya kutunga sentensi za "...nge..." Mara nikamsikia ametoa mfano "Ningejua, nisingeondoka" . Ile sentensi ikanishtua sana. Nikamwambia yule mama mwenye mgahawa abadili channel "Maliza soda uende" ilo ndio jibu alilonipa
Kimoyo moyo nikafikiria " Ningeenda kidato cha tano, nisingekuwa hapa" Nikajikuta napakumbuka nyumbani kwa wazee. Ikanipelekea kulikumbuka tukio moja ambalo lilitaka kuwagombanisha mama na baba. Ilikuwa ni kama wiki mmoja baada ya kudondosha kibox cha kondom darasani, kwavile nilipewa suspension ya wiki 3. Nilivyorudi nyumbani mzee alisema kwa wiki 3 zote itakuwa zamu yako kuchunga mbuzi.
Sasa siku hiyo tuko machungoni na na watoto wengine, tukaokota kiberiti cha gesi. Kule machungoni tukawa tunawasha majani alafu tunazima kwa kukanyaga. Sasa kuna muda tukawasha, ile tunazima, kukanyaga jani likapeperushwa na upepo, moto ukawaka na kwingine. Kila tukijitahidi kuzima, moto unapepea. Moto ukatanda kote, mbuzi zikaanza kukimbia ovyo. Kuona vile na sisi tukakimbia kuzifata mbuzi huku tunarudi nyumbani. Wanakijiji wakaitana, wakaushambulia moto na kufanikiwa kuuzima japo ulishaunguza eneo kubwa kiasi. Mzee mzima nikarudi nyumbani, moja kwa moja chumbani nikazuga kulala. Kumbe wakati tunakimbia na mbuzi kuna bibi mmoja alikuwa anaokota kuni alituona. Kwenye mkutano wa kijiji akatutaja tuliosababisha moto. Siku hiyo mzee alinipiga fimbo sio za nchi hii. Baadae namsikia anamuuliza mama " Hivi mama nanii, huyu ni mwanangu kweli??" Bi mkubwa nae akawaka "Nitolee wehu wako hapa, angalia lipua la mwanao alaf nenda kajiangalie kwenye kioo kama hujawahi kujiangalia" faza akawa mpole, maana kama ni pua tu, kweli tunazo.
Pia wakati nasubiria majibu ya kidato cha nne, kuna demu nilikuwaga nae ila akaja kunipiga chini baada ya kumpata mwenye hela. Miezi kadhaa akadaka mimba, ila yule jamaa akaikana. Kijiji chote kilikuwa kinanionaga na yule dem, habari zikasambaa mimba yangu. Demu nae akashikiria pale pale kuwa mimba yangu. Nilijitahidi sana kukataa , ila watu akiwemo faza hawakunielewa. Japo baadae sana ilikuja kugundulika kuwa mimba haikuwa yangu.
Hayo matukio yote nilikuwa nayakumbuka wakati nipo kwenye ule mgahawa pale buguruni. Nikamalizia soda nikatoka.
** *** ***** *****
Nilikomaa sana pale buguruni kwa muda mrefu, nafanya kazi pale na kujiegesha mule mule. Nakumbuka siku moja nilikuwa nimekaa na wabeba mizigo wenzangu tunapiga story. Akatokea jamaa akawa anatupa story za migodini, kuwa unafanya kazi kwa tabu ila ukitusua unasahau msoto. Jamaa alikuwa anafanyia kwenye migodi za Msumbiji, kuna eneo linaitwa Mtipweshi (kama sijakosea kulitamka). Story yake ilinivutia, nikajisemea, sibebi mizigo tena hapa, naenda Msumbiji
...............
NarudSehemu ya 8:
.... Tofauti na wengi wanafikiria, leo hii ukiniuliza shujaa wangu ni nani katika dunia hii,au ni nani namkubali sana katika ulimwengu huu, kwa kujivunia kabisa nitasema "BABA YANGU" . Huko mbele nitakwambia kwanini au hata wewe utagundua sababu.
Msimu wa kilimo ulipofika, sikuwa na hela ya kutosha kusema iniwezeshe kulima eneo kubwa sana. Nilifanya ushirikiano na jamaa mwingine mmoja, kwa pamoja tukafanikisha kulima heka tano za mbaazi. Shamba tulipata eneo moja lipo manispaa ya Songea, linaitwa Mlilayoyo. Tuliweka juhudi zote na usimamizi wa hali ya juu. Zao lilistawi vizuri sana. Naweza sema kati ya watu wote tuliokuwa tumelima maeneo ya pale, mimi na jamaa ndio tulikuwa na matokeo mazuri. Nakumbuka wakati tunaanza kilimo, bei ya mbaazi ilikuwa juu na nzuri. Kilo moja kuna sehemu ilikuwa inafika hadi 2500.
Msimu wa mavuno wakati unakaribia, ndio zikaja zile tetesi za kushuka kwa mbaazi. Tetesi zikawa kweli, soko likapotea. Ikafika kipindi kisado kinauzwa shillingi 500. Tukashauriana na jamaa tusivune, tusubirie hadi soko likae vizuri kwanza. Siku zikaenda, soko halikai sawa, mpaka mbaazi zetu zikakutana na msimu mpya wa kilimo. Gharama ya kuzivuna ilikuwa kubwa kuliko hata hela ambayo ingepatikana baada ya kuuza, achilia mbali gharama za kuendesha shamba mpaka kufikia hapo.
Mwenye shamba lake anatuuliza, tunampango gani msimu ujao? Tunalikodi tena shamba lake au la? Kama hatukodi, basi tuvune mbaazi tumuachie ardhi yake. Mshirika wangu ananiuliza, tunafanyaje? Nikamwambia me sina cha kufanya , we amua chochote utakachoona nakuachia shamba lote, siwezi kuingia tena gharama za kuvuna. Jamaa nikatemana nae kwa mtindo huo. Nikarudi ghetto pale moonlight.
Kwavile hela niliingiza zote kwenye kilimo, nikawa nimefulia tena. Hapo nilipata somo kuwa kama bajeti ya unachotaka kufanya ni laki 3,alaf na wewe una laki 3 hiyo hiyo, acha. Tulia kwanza mpaka upate hela ya ziada walau mara mbili ya hiyo au hata nusu yake, vinginevyo utakuja kuona watu wanakuchawia huko mbeleni.
Nilianza upya vibarua, hapo nipo choka mbaya. Baada ya kudunduliza na kupata hela kadhaa, sikutaka kujiuliza mara mbili wala kuzurura sana mitaani maana naweza nikakutana na mtu mwingine akanipa fursa. Nikaamua kurudi nyumbani.
* **
Nilifika nyumbani majira ya usiku. Kabla sijaingia kwenye himaya ya nyumbani kabisa, nilipaangalia kwa muda mrefu sana. Kwa muonekano palikuwa panavutia na maisha hayakuwa mabaya. Nikagonga mlango baada ya kuvuka fensi ya maua na geti kubwa la mbao. Baba ndio alifungua mlango, alivyoniona akaniambia karibu. Yani hakuonesha kama ameshangaa, amefurahi au kushtuka, kiufupi alichukulia kama nilienda dukani sasa ndio narudi.
Asubuhi ya siku hiyo, naskia mama alijichoma na msumali wakati anapalilia maua pale nyumbani, toka hapo hakuweza kukanyaga vizuri chini, alikuwa anachechemea, ila aliponiona nahisi alipata ganzi ya mguu, maana sio kunikumbatia tu, bali pamoja na ndevu zangu alinibeba. Nikapata faraja niliyoitaka, faza nikampotezea. Pale mezani alikuwa ndio anamtengea mzee chai na maandazi (siku zote baba hupenda kunywa chai usiku hata awe ameshiba vipi). Basi ile chai akanipa mimi, Mzee anauliza vipi mbona unagawa chai yangu? Mama hana hata habari nae. Mara kaniletea hiki, mara kile, ilimradi ukarimu. Nilipoenda kulala, kila mara anakuja kunichungulia. Sina uhakika kama yeye alilala usiku ule.
Asubuhi ndio tuliweza kuongea vizuri kama familia. Hapo mama ameshawaambia ndugu zangu wote kuwa nimerudi. Baada ya chai ndio niliweza kukaa na kuongea na mzee. Kitu cha kwanza kuniuliza "Umefata ada?". Nikamwangalia kwa mshangao, ila kilichonishangaza zaidi nilipogundua kuwa hakuwahi kuwaambia nyumbani kuwa tulikutana Madaba, Songea. Ilo lilinishangaza.
Ila aliniambia, "Ulitaka nimwambie mama yako kuwa baada ya kupotea miaka mingi tulikutana ukiwa kibarua ambae maisha bado yamekupiga? Au baada ya miaka mingi kutoonekana, tumeonana ila bado ukaniomba hela? . Nilijua hutorudi ndio maana sikumwambia chochote mama yako kwa kipindi kile, na pia sitoshangaa kama utaondoka tena. Najua tulipoachana maisha yako yaliendelea kuwa magumu na ndio maana hata hela niliyokutumia wala hukunirudishia. Nikajiuliza hela gani alinitumia huyu mzee? Nahisi alijua ninachowaza, akaniambia siku tuliyoachana alichukua namba yangu toka kwa wale vibarua niliokuwa nafanya nao, na alipoona imepita zaidi ya miezi 6 sijaonekana nyumbani alinitumia laki 3 kwenye simu. Nikakumbuka kuna siku iliingia hela, nikajua mtu kakosea kutuma, nikaitoa kwa wakala alaf nikakausha. Mtumaji nae hakunicheki tena. Niliona aibu kichizi.
Baba akaniambia "Ikitokea leo hii Mama yako aseme nyie wote 7 sio wanangu, nitakubaliana nae kwa hao 6 wengine lakini wewe nina uhakika wa asilimia zote ni mwanangu. Mimi na wewe ni mapacha tuliozaliwa katika miaka tofauti, kwa kifupi ww ni mimi". Maneno ya mzee yalinigusa sana kwa mbali machozi yakawa yananilenga hivi. Faza akaniambia "Kama unalia nenda jikoni kwa mama yako" . Mzee wangu kauzu kichizi yani,kwanza toka nakua sijawahi kumuona anasikitika. Nikabaki nashangaa tu maneno yake. Akazidi kuniambia " Tofauti ya ww na mimi, ni kwamba mimi nilirudi baada ya safari yangu kuelekea mwishoni,nilirudi nikiwa shujaa. Wewe ni shujaa lakini safari yako haijaisha,umerudi ikiwa kati"
Kuna mengi sana hatuyajui kuhusu wazazi wetu ambayo yangetufunza na kutujenga, hii inatokana na kwamba tuko bize sana kiasi tunakosa muda wa kuzungumza nao. Misukosuko tunayokutana nayo leo hii, majibu yote yapo kwenye maisha waliyopitia wazazi wetu. Tunatafutaga majibu, lakini majibu sahihi yapo tulipotoka. Baba yangu ni Shujaa wangu,Mimi ni Baba yangu,na Baba yangu ni Mimi, unajua kwanini? Ni kutokana na stori fupi ya safari ya maisha yake aliyonisimulia.
* *
Kwa ufupi tu ilikuwa hivi. Anasema "Sikuwa na uwezo mkubwa wa kuelewa darasani, shule niliishia elimu ya msingi hata mtihani wa mwisho sikufanya, nilifukuzwa kwa kosa la kuchoma ofisi ya walimu. Tokea hapo nilikuwa naonekana kama mtoto mtukutu nyumbani, babu yako aliniwekea zamu ya kuchunga kila siku, alaf nyumbani sikuwa napewa upendeleo wowote. Kuna siku nilienda kuchunga,jioni nikarudisha ng'ombe ila nikasepa na mbuzi wote. Nikauza na kufanya mtaji. Heri yako unaondoka nyumbani umepewa hela, tena tukijua kuwa utaondoka. Sijui msoto uliopitia ww, lakini msoto niliopitia mimi baba yako ndani ya miaka minne ya mwanzo nadhani ww ungekufa. Ndani ya hiyo miaka minne ya mwanzo kuna siku niliamua kabisa kurudi kwa babu yako nikaombe msamaha, nilifika mpaka pale, nikaiangalia sana nyumba ila nikaona siwezi kurudi nikiwa hivi, nikageuza na kuondoka. Ndio maana sikuile tuliyokutana Songea, nilijisemea kimoyo moyo, kama huyu ni mwanangu hatorudi nyumbani.
Tokea ile siku niliyogeuza, nilijituma sana kiasi kwamba siku niliyorudi nyumbani, nilirudi na idadi ile ile ya mifugo niliyoondoka nayo ila badala ya mbuzi nilirudi na ng'ombe. Ila pamoja na hayo babu yako aligoma kunisamehe hadi kikafanyika kikao na wazee wa kijiji, ndio nikasamehewa,tena baada ya kuchapwa bakora pamoja utu uzima wangu.
Aliendelea kunisimulia vitu vingi sana, hapo ndio nikajua nilidhani nimesota na kupitia tabu nyingi sana, kumbe ningezifananisha na za mzee, basi zangu zingekuwa ni utangulizi tu. Mgodini niliposhindwa kwenda, yeye alishaenda na alishawahi kufukiwa hadi na kifusi. Baba yangu akitembea huwa anachehemea,mguu mmoja ni kama mfupi. Ananiambia ule ulishavunjika mara mbili kutokana na mbilinge za migodini.
Tokea siku hiyo, kila nnapopitia ugumu wowote, lazima nijiangalie kwenye kioo. Baba yangu ni kioo changu.
* * *
Kurudi kwangu kulirudisha furaha sana nyumbani. Usiku kabla ya kulala, mshua aliniuliza "Una watoto wa ngapi mpaka sasa? Nikamjibu mmoja wa kiume. Akasema namuhitaji, fanya mpango aje hapa nyumbani.
Najua kuna wadau watashangaa kuona nimesema nina mtoto mmoja wa kiume, wakati katika stori yote sijawahi kuongelea ili swala. Katika hii stori ya safari yangu, nimegusa baadhi ya matukio ya kwenye maisha yangu ila sio yote. Na sijagusia mapenzi kwasababu yamenitesa kichizi, nadhani mwanaume akiwa hana hela mwenendo wake wa mapenzi unajilikana tu,mapenzi yanatesa sana Me kuliko Ke. Kuna msemo mmoja nimeuona juzi kuwa "Mwanaume kama huna hela, kazi ya kulinda mahusiano yako muachie Mungu" hii ni kweli kwa asilimia zote. Kwa ufupi kwenye hii safari yangu, mtoto ninae tena wa kiume.
Nikafanya mpango na taratibu zote, nikapewa yule mtoto. Sasa hivi anaishi na babu yake.
Siku ambayo mtoto alifika pale nyumbani, kesho yake mzee aliniita tukawa na mazungumzo ya hapa na pale. Kisha akatoa bahasha na kunikabidhi, kuhesabu ni milioni mbili. Nikamuuliza za nini. Akasema "Babu yako alinipokea baada ya kufanya kikao na wazee kisha nikachapwa bakora,nimekupokea nyumbani ila sitokuchapa...Safari yako bado haijaisha, nenda kapambane". Nilimwangalia yule mzee sikummaliza.
Wiki moja badae nilikuwa ndani ya bus naelekea Songea. Nikarudi rasmi kwenye kilimo. Safari hii nikalima tangawizi..
Nitarudi kukwambia jambo zuri lililotokea. Katika maisha,Baraka za wazazi ni kila kitu.
....
Analyse #Baharia wa nchi kavu.
juu hapa kwenye bar ya mama tarimoUpo moonlight ipi mkuu? Mpya au ile ya zamani kule chini? 😅😅
Asante Sana mkuu KWA muda wako.. Tumejifunza meeng mazuri kupitia ww na umekuwa daraja zuri kututia moyo wale tuliokata tamaaSehemu ya 9:
.. Katika ile Million mbili aliyonipa Mzee, miliona 1.7 yote niliweka kwenye kilimo. Kuanzia kukodi mashamba, kuyaandaa, mbegu n.k. Hiyo laki 3 iliyobaki ndio ilikuwa inanisogeza. Tangawizi nilipanda sehemu moja kule Madaba, Songea inaitwa Balali (ni milimani huko ndani ndani) . Nilipovuna na kuuza, nilipata faida ya milioni 1.5 (baada ya kutoa ile 1.7 niliyowekeza). Toka nianze kufanya biashara, hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza napata faida toka nianze hustling.
Nikaamua kurudi tena nyumbani kwa Wazee. Nilipokelewa vizuri tu. Kesho yake nikaongea sana na Mzee akitaka kujua maendeleo yangu, nikamuelezea hali halisi. Akatikisa kichwa kukuonesha amependezwa na matokeo. Ile siku ambayo alinikabidhi milioni mbili, ilikuwa makubaliano kwamba mambo yakikaa sawa nimrudishie. Kwahiyo baada ya mazungumzo ya hapa na pale nikamkabidhi bahasha ila hakuangaika kuigusa, aliuliza tu kuna nini. Nikamuelezea. Akatabasam tu, alaf akaniambia "Niliposema unirudishie mambo yakikaa sawa, lengo langu ilikuwa ni kukufanya usisahau ulipozitoa ili ikupe motisha ya kuzitumia vizuri, na uzee huu ukinipa milioni mbili napeleka wapi?
Nilimwangalia sana yule mzee ila sikummaliza. Mazungumzo yaliisha.
Baada ya wiki mbili nikaondoka nyumbani nikiwa na ile milioni mbili, pamoja na ile ambayo ilikuwa faida, nikajisemea moyoni "Safari yangu bado haijafika mwisho, ntarudi nyumbani nikiwa mshindi"
Pamoja na kupata faida kwenye tangawizi, ila sikutaka kuendelea nayo maana ilinisumbua pia mpaka kuja kufikia mavuno. Niliamua kuwekeza ile hela kwenye kitu tofauti kabisa na kilimo. Mungu ni mwema mambo yameenda vizuri sana. Badala ya kurudi nyumbani kishujaa, nikaamua kuwa natuma nyumbani msg za kishujaa. Kila mwisho wa mwezi huwa nawatumia Baba na Mama laki mbili kila mmoja kwenye account zao za simu. December 2018 niliwatumia mapema sana,Baba alinipigia simu "Christmas jitahidi huwe hapa nyumbani" .
Nikaenda.
Mazungumzo ya hapa na pale,Mzee akaniambia " Nashkuru kwa unavyotuhudumia mimi na Mama yako,yawezekana hujui uzito wa unachokifanya ila ni kikubwa sana. Ila ningependa kukwambia kitu kimoja,mwangalie sana Mama yako. Vitu vyote ambavyo nimefanya mimi kama baba yako,au magumu niliyopitiaga,yote ilikuwa ni kumtengenezea mazingira mazuri mama yako na wanae ambao ni nyinyi,kama unataka kunipa furaha Baba yako,basi mwangalie sana Mama yako. Furaha yake ni yangu. Nina uwezo wa kuvumilia matatizo 100 yanayonisumbua mimi,ila sitoweza kuvumilia tatizo moja linalomsumbua Mama yako. Kwa hali ya uchumi niliyonayo ningeweza kuwa na wanawake wengine,ila siku zote nilimuahidi sitofanya kitu cha kumuumiza,na kamwe sitoweza".
Nilimwangalia sana Mzee wangu,nikaona kumbe nina mzee jembe kiasi hiki? Ikabidi kama kijana nianze kuongea maneno ya kiustaarabu na mimi. Nikamwambia "Nashkuru Mzee kwa maneno yako uliyoongea,yamenigusa sana. Nitawaangalia siku zote wewe na Mama kwa kadiri niwezavyo. Maana hata ningesema nijaribu kuwarudishia fadhila zenu inagenichukua miaka mingi sana" Kabla hata sijamaliza Mzee akacheka. Ikabidi nimwangalie kwa mshangao. Akasema "Sio tu ungejaribu,ukitaka jaribu alafu hiyo miaka mingi unayosema ungetumia,ongezea na mingine 100 ila hutoweza kulipa fadhila yoyote aliyokufanyia mtu,achilia mbali sisi Wazazi wako. Maana hujui walipoteza nini katika kukufanyia wewe fadhila.Kitu pekee unachoweza kufanya ni kulipa wema kwa wema."....akaendelea " Nenda jikoni kwa Mama ako naona ushaanza kutia simanzi hapa,yeye ndio anaweza kuvumilia mazungumzo ya aina hiyo".
Kwa siku hiyo mazungumzo yaliishia hapo,tuliendelea kesho yake. Mzee wangu siku zote hapendi mtu anayeongea kinyonge nyonge au kutia huruma.
Turudi nyuma kidogo:
MWISHONI MWA MWAKA 2017
Hii ni siku ambayo mambo yangu yalienda ovyo sana. Ni siku ambayo niliamua rasmi kumsusia yule partner wangu shamba la Mbaazi. Hapo nilikuwa nimeshasota sana kwenye kilimo na ujasiliamali. Nishasota kitaa bila kazi baada ya kumaliza chuo. Dunia yote naona ipo kinyume na mimi. Nishasikiliza sana wale motivational speakers wote unaowajua ili kutafuta tumaini ila naambualia patupu. Ndipo nilipoamua kumpigia simu Baba. Naongea nae huku nikiwa na hasira inayotokana na ugumu wa mambo plus huzuni pia. Mzee akaniambia "Kama huwezi kuongea bila kulia, basi mpigie simu Mama ako, au la, kata simu, lia kwanza, ukimaliza nipigie tuongee" Mzee wangu ni shujaa wangu aisee. Nikajikaza tukaongea kidogo, akaniambia fanya mpango usafiri uje tuongee vizuri.
Nikawatembelea. Siku moja baada ya kufika mida ya jioni akaniita tuongee. Mama akatutengea chai, mshua akamimina kwenye kikombe kimoja alafu akamuita Mama. "Huyu mpe juice" Nikawahi kusema, na baridi hii ningependa chai zaidi kuliko juice. Baba akaniambia "Dogo ukishaoa utakuwa huru kutoa mapendekezo ya chakula unachotaka, kabla ya hapo chukua kilichopo". Alaf akamgeukia Mama " Mletee juice". Nikawa mpole. Najua alifanya vile kwasababu siku ambayo tuliongelea habari za mwanangu aliniuliza naoa lini, nikamwambia bado sana.
Anyway, nikakubali juice na kikao kikaendelea. Akaniambia najua una maswaibu yamekukuta, ila kabla hujaniambia na kuanza kutia huruma, ngoja nikuelezee ya kwangu. Akaanza kunipa story ya harakati alizopitia na ndizo ambazo nilikuwa nawasimulia tangia story inaanza Asilimia kubwa ya niliyowasimulia ni mambo aliyopitia Mzee wangu. Kati ya yote, yangu ni asilimia kama 5 tu, na hasa yanayohusu kilimo na Shule.
Alipomaliza kunisimulia, nilibaki namshangao. Nikamuuliza "Mbona hujawahi kunisimulia mimi au ndugu zangu wengine?" Akanijibu "Ningekusimulia sa ngapi na ww muda huna,pia naskia role model wako ni Ben Carson? Ambae unajua historia yake tokea anazaliwa hadi anakuwa Neuro Surgeon? " Nikakausha. Akaniuliza unajua leo tarehe ngapi? Nikajbu 8. Hapo ndio nikakumbuka kuwa ni siku ya kuzaliwa ya Mama. Nikajishangaa imekuwaje nikaisahau wakati miaka yote huwa naikumbuka? Sikuongea kitu. Akaniambia kuna maswahibu yamekukuta mpaka yamepelekeaa ww kuwa hapa, unaweza kuniambia?
Nikamwambia hapana, nipo sawa sasa. Nitamwambia nini wakati aliyopitia yeye ni kama bahari nzima, na yangu ni tone tu? Alafu pia nilijaribu kuielewa psychology ya Mzee kwann alianza kunisimulia story yake kabla hata hajasikiliza yangu.
Alivyoona sina cha kuongea akaniruhusu niondoke. Wakati natoka nikajigonga kwenye ncha ya kiti. Sikutaka kugeuka nyuma,ila nikamsikia anasema "Utapewa pole jikoni,ila najua ukifika mjini utapost kuwa umejigonga kwenye kiti" Alaf akaangua kicheko.
* *
Siku moja kabla ya kurudi mjini, Baba ndio alinipatia zile milioni mbili ambazo niliwekeza kwenye tangawizi. Japo sikumuelezea matatizo yangu, ila najua aliyahisi.
Aliniambia yafuataya "Dunia ya leo kila unayemuona anamatatizo yake kiasi kwamba anakosa hata muda wa kukuonea huruma ww. Hivyo unapoongea na watu tegemea sana msaada wao,ila usitegmee huruma yao.
Akaendelea "Huwezi kurudisha fadhila alizokutendea mtu,ila unachaweza kufanya ni kulipiza wema kwa wema.
Akamalizia "Najua utakuwa bize sana,lakini mimi na Mama yako kwa umri tulio nao hatuwezi tena kuongea na simu zaidi hata ya nusu saa,dakika 10 zako kwa siku ukitupigia simu zinatutosha".
Maneno ya mzee yalinigusa sana.
Tukaishia hapo.
Kesho yake niliongea na Mama kiasi,nikawa nagusia kuwa Baba kauzu sana. Mama akaniambia "Toka ujana wake yupo hivyo na ndio njia iliyosababisha akanipata mimi,ni mchekeshaji aliye serious"
Nikajikuta natamani kuijua story ya jinsi Baba na Mama walivyokutana. Kabla sijaondoka nikajaribu kumgusia Mzee ilo swala ,akajibu " Unataka darasa la kutongoza? We ukimpata nipe namba yake,nitamaliza kila kitu" baada ya kuongea hivyo akacheka saaana.
Aisee nilikuwa namiss vitu vingi sana toka kwa Wazazi.
My father,my hero
* *
Nimejaribu kushare na nyie story ya Baba yangu kwavile najua leo hii kuna mtu anapitia msoto,kuna mtu hana muda wa kuzungumza na wazee wake,anakaribia kukata tamaa,anasubiria miaka 3 ijayo ndio aweze kuongea na wazazi wake n.k
Ili niweze kuwagusa hao wote,imebidi niilete kwa mtindo wa story,kinyume na hapo kuna wengine wasingepata huu ujumbe japokuwa wanauhitaji.
Wazee wetu wanavitu vingi sana ambavyo vingekuwa funzo na mwangaza mkubwa kwetu, ila hatuvijui maana hatupati muda nao. Pata muda na wazee wako. Ongea nao kadri unavyopata muda, usisubiri mambo yawe tight kama ilivyokuwa kwangu ndio ukaongee nao.
Tunayopitia sasa, walishapitia. THE BEST MOTIVATION SPEAKERS ARE OUR PARENTS. THEIR LIFE IS OUR DICTIONARY TRUST ME GUYS.
Najuwa kuna madini mzee hajaniambia yote. Kwa jinsi nilivyokaribu nae siku hizi, ntajua kila kitu.
Mimi ni Baba yangu, na Baba yangu ni Mimi.
Naitwa Analyse ,na hiyo ndio ilikuwa safari yangu na Baba yangu.
See You.
#Baharia wa Nchi Kavu.
Pamoja sana mkuu. 👊Asante Sana mkuu KWA muda wako.. Tumejifunza meeng mazuri kupitia ww na umekuwa daraja zuri kututia moyo wale tuliokata tamaa
Maisha ni safari ndeefu Sana yenye milima na mabonde mengi...na Siri ya kutoboa kwa mtu ipo kwa aina mbalimbali... wazazi wako ni Moja ya daraja lako la mafanikio mpaka ulipo hapo leo
Nimejifunza utii, Uaminifu na wema unalipa Sana maishani...Unapopanda mbegu njema leo manufaa makubwa utayaona maishani (Malipo ni hapa hapa duniani)