Najaribu kuwaza Jakaya Kikwete aliwezaje kuajiri Walimu na Madaktari wote katika kipindi chake wakati Hayati Magufuli hata mwaka mmoja alishindwa

Watu kama wewe mlikimbia umande
 
Ongezea nyama kidogo chief, una hoja nzito
Alikuwa anahujumiwa, angeweza kuajiri walimu wengi zaidi. Watu walikuwa wanahitaji zaidi basic needs kuliko flyovers ambazo ziko Dar es salaam tu. Ndege pia zilikuwa zinahitaji ila si kwa uwingi huo
Walimsoma wakamuweka kwenye kiganja, wakaanza kumuongoza
Hii nchi ukiwa na nia njema, inabidi utumie akili sana kuweza kuiongoza. Waangalie pia Lowasa na Kikwete kwenye nia yao njema ya miradi yao zikiwemo shule za kata.
 
Mbona jk aliweza vyote. Wakati wake ndo uliongoza kwa mtandao wa barabara.

Barabara ni kitu kidogo sana haili hela nyingi kama bwawa la umeme . Ujenzi wa reli.

Bei ya kununua Ndege moja tu ni kubwa sana kuliko kujenga barabara
 
Magu hakuwa na hela za kuajiri.
 
Ukweli mchuku kwa walinda legacy uchwara
 
Barabara ni kitu kidogo sana haili hela nyingi kama bwawa la umeme . Ujenzi wa reli.

Bei ya kununua Ndege moja tu ni kubwa sana kuliko kujenga barabara
Kulikuwa hakuna sababu ya kufanya hivyo wakati anajua bajeti ya serikali ndogo. Hivyo alikurupuka na hii ni shida ya kumpa mtu uraisi wakati hana uwezo nayo
 

Tuache maneno..tuitishe kura za maoni tujue nani ni nani? πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ . watanzania sio wajinga tena
 

Kura za maoni tafadhali ili watanzania waamue. Sio watu wawili ndani ya JF waamue kwa niaba ya watanzania wote ili tutoe maneno maneno.
Waswali tunaongea sana mpaka uongo uwe ukweli
 
Tuache maneno..tuitishe kura za maoni tujue nani ni nani? πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ . watanzania sio wajinga tena
Si unajua tanzania wapumbavu ni wengi wale waliokuwa wanafurahia kutumbuliwa kwa wafanyakazi ili waje uraiani kufanana na hawa wajinga. Mjinga anafikiri siku zote watu wote wafanane naye ili apate relief
 
Upuuzi tu. Vitu gani?
Mradi wenyewe wa umeme akamwachia Msala Samia. Hongera sana Mama sasa umeme unawaka kutokea Bwawa la Nyerere
 
Magu hakuwahi kuwa kiongozi, alikuwa na ajenda zake, moja ubaguzi na kuua wapinzani wake. Hela iliyojenga uwanja wa ndege Chato, hospitali ya kitalii, daraja la Busisi-Kigongo kwa uchache ingeajiri watanzania wangapi. Yule alikuwa shetani asiye na mfano
 
Duh!...una maana gani mkuu unaposema 'kuongozewa ?
 
Waliokuwa wanahitimu walikuwa wachache.

Mwendazake asingezingua Kuajiri hata Sasa walau 3/4 ya wahitimu wangeajiriwa .

Mama amekuwa anaajiri kati ya 8,000-12,000 Kila mwaka.

Hawa nyumbu waliokuwa.kwenye msoto eti nao wanadai kikokotoo na kusema mama hafai 😁😁
 
vp hamjaalikwa kusimamia uchaguzi Afrika Kusini nini? mwenzenu uhuru kenyata anasimamia uchaguzi Afrika Kusini sasa hivi, alialikwa …
 
Vipaumbele. Wakati wa JPM pesa ilielekezwa kwenye miundombinu ya reli, umeme na madaraja makubwa ya juu na chini. Hapo mbona ni rahisi tu kuelewa
Sawa ila pia hakua mkweli, saundi zilikua Mungu,chuki,uongo na visasi vilimjaa pia kiburi cha mamlaka na kufuru juu
 
Si unajua tanzania wapumbavu ni wengi wale waliokuwa wanafurahia kutumbuliwa kwa wafanyakazi ili waje uraiani kufanana na hawa wajinga. Mjinga anafikiri siku zote watu wote wafanane naye ili apate relief

Na nyinyi wenye akili ndio mnatupiga kwa kutumia ofisi za umma na kutudharau sisi tusio na akili. Acha tujichagulie tunayempenda, hata kama hatuna akili.
Kura za watanzania zitaamua nani ni bora kati ya JK na JPM. Sio porojo zetu za kiswahili swahili mitandaoni 🀣 🀣 🀣 🀣 😎 😎 😎 😎 😎
 
Ndugu umepuyanga,suala la kikokotoo ni kaa la moto kwa watawala kwasabu mifuko ya hifadhi ya jamii imefanywa chanzo cha mapato ya serikali,ile percentage inayochangiwa na mwajiri ni geresha,we have to be realistic kwenye hii hoja,km ww ni mserikali ondoeni acheni geresha na ujanjaujanja.Siasa mingi wkt mnajua kiini cha tatizo
 
Wafuasi wa"jiwe" mnateseeeka, Mungu hadhihakiwi, he was a real saddist
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…