Najaribu kuwaza Jakaya Kikwete aliwezaje kuajiri Walimu na Madaktari wote katika kipindi chake wakati Hayati Magufuli hata mwaka mmoja alishindwa

Najaribu kuwaza Jakaya Kikwete aliwezaje kuajiri Walimu na Madaktari wote katika kipindi chake wakati Hayati Magufuli hata mwaka mmoja alishindwa

Hawa watu hawajui kuwa kadiri siku zinavyokwenda ndiyo nchi inavyozidi kuwa ngumu. Watu hawajui kuwa hata wanaopiga kelele sasa hivi wanaitakia nchi salama siku zijazo. CCM haina tena ujanja sasa hivi imebaki ku-hang up kama timu inayojihami dakika za mwisho isifungwe goli. Tatizo ni kuwa huu ''mpira'' wa CCM vs wananchi hauishi. Siku nchi itakapolipuka kwa fujo za watu kuchoka na maisha magumu kila mtu ataathirika na kujuta.
Well said
 
Hizi nchi zote mnazoziona zimeendelea... wananchi wake wameuawa haswa... tena kwa sheria kali haswa... Watanzania mnapenda kudeka sana.. Jk nchi ilimshinda kabisaa.. sema alikuwa na mahusiano mazuri na wafanyabiashara na wahisani kutoka nje... JPM wananchi tulipigika lakini kuna vitu tuliviona... tena kwa muda mfupi... sasa hali ni mbaya kuliko unavyofikiria...
Mawazo yako yaheshimiwe.
Lakini kama maendeleo ya vitu kilikuwa ndiyo kigezo cha uongozi bora, basi kheri tungebaki na mkoloni wa kijerumani.
Maana ametujengea mtandao wa Reli, Bandari na kutoboa milima ili kujenga barabara.
Lakini pamoja na hilo waliwafanya babu zetu kama wanyama.

Baba mwema ni yule anayewapa chakula watoto wake huku akiendelea na ujenzi wa nyumba.
 
Aliajiri na kuongeza mshahara yaani ile salary incriment na annual incriment.
 
Miradi inakula Sana hela

Kama umewahi kujenga nyumba utaelewa kuwa ujenzi unatumia gharama kubwa Sana

Sasa JPM alizidiwa imbalance ikatokea.
Jakaya alijenga 6000km Barbara za lami,udom,chuo kikui Cha jeshi,pandisha mishahara kila mwaka,boresha muhimbili na Jenga mloganzila,ruzuku pembejeo kilimo,kilimo kwanza,mikopo elimu ya juu bila ukakasi,kumbuka lami kilomota moja ni zaidi ya bilioni mbili za kitanzania,Sasa piga hesabu hiyo miradi ya ujenzi ya magu pesa iliyotumika mpaka anakufa na miradi ya jakaya,Fanya lami tu
 
Barabara ni kitu kidogo sana haili hela nyingi kama bwawa la umeme . Ujenzi wa reli.

Bei ya kununua Ndege moja tu ni kubwa sana kuliko kujenga barabara
Barbara kilomita moja ni bilioni mbili unusu,jakaya alijenga kilomita elfu sita,linganisha na mradi wa jnhp ambao magu aliuacha ukiwa 30%
 
Huyu wa sasa haajiri hata nyau.

Kaangalie sekretariet ya ajira inapita miezi mitatu kuna kada unakuta ajira ni 0.
 
Mimi ni mwalimu ambaye niliajiriwa kipindi Cha kikwete lakini najuta kuajiriwa kipindi hicho maana kulikuwa na mfumuko wa bei kiasi kwamba mshahara wote uliishia kwenye mahitaji.mshahara ulikuwa mdogo sana yaani ilikuwa hakuna tofauti na jobless angalau kipindi Cha Magufuli mfumuko wa bei ulitulia na sisi walimu tukawa tunatembea vifua mbele maana mshahara ulitosha Kwa mahitani yetu.
Mfumuko wa Bei kipindi Cha jakaya ulikua asilimia ngapi na magu ngapi?..unga,mafuta,sukari wakati wa jakaya kilo ilikua Bei gani na magu Bei gani?
 
J - yani hii nchi tutaibiwa mpaka tunakufa.

Kitwanga - Chukua form basi

J - MIMI WATU WATALIMIA MENO.
 
Usiwe kama kiande, hakuna awamuam ambayo watu hawakuajiriwa

Usibishe kwa pumba sisi wenyewe tunaona huko makazini kuna raia kibao waliajiriwa zama hiyo ya Magu na shuhuda zipo
Acha kukaza fuvu mkuu, katika halmashauri nayofanya kazi watu wioajiriwa kipindi chote cha Magu ni 12 tu na watu zaidi ya 180 waliajiriwa kipindi Cha miaka miwili ya mwisho ya JK (14/15)
 
Jakaya Kikwete alitumia miujiza gani kuajiri almost wote waliohitimu kipindi chake hasa ualimu na udaktari kiasi ambacho watu walikuwa wanapangiwa bila hata kuomba unajikuta umepangiwa mkoa fulani

JPM hata mwaka mmoja tu alishindwa na kuleta visingizio kibao eti hakuna nchi iliyoajiro graduate wote. Sasa swali linakuja JK aliwezaje?

Mass unemployment aliyoicha JPM mpaka sasa inamtesa Samia sijui ataimalizaje. Ndio maana anastruggle sana kuifanya sector binafsi ikue ili angalau kuwapunguza graduate waliopo mtaani. Hali ilikuwa mbaya sana enzi za JPM.

JK tunakukumbuka sana.
Vitu vidogo,Nyerere aliwezaje kusomesha vijana vyuo vikuu, ndani na nje, bure, serikali iligharamia,
Aliwezaje kutoa ajira kwa kila kijana aliyemaliza kuanzia LA saba na kuendelea?
Ni Mambo ya idadi ya watu tu,
Kwa kikwete, shule zilikuwa chache,vyuo vya ualimu vichache pia, kwa hiyo Kuajili ilikua raisi, kila mhitimu alipata nafasi,
Shule za kata zimeanza kujengwa kipindi cha kikwete, 2005-2015, zilipokqmirika idadi ya wanafunzi, ni wengi, na mahitqji ya waalimu ni makubwa, na wahitimu wa ualimu ni wengi, shida, mfuko wa serikali hauwezi, Kuajili wote, pesa haitoshi,
 
Does it mean kwamba kipindi cha jpm hakukukuwa na mahitaji ya walimu? Hivi ukisoma marthus theory of population inavyokuwa. Rudi shule
 
Barbara kilomita moja ni bilioni mbili unusu,jakaya alijenga kilomita elfu sita,linganisha na mradi wa jnhp ambao magu aliuacha ukiwa 30%
Naomba nitajie barabara iliyojengwa kwa shilingi bilioni mbili na nusu kwa 1 km kipindi cha Jakaya?

Kama kwa sasa pamoja na mfumuko wa bei kilomita moja ya barabara ya lami yenye viwango inagharimu bilioni 1 tu.

Miaka zaidi ya kumi nyuma ujenzi na zana zake kiujumla gharama zilikuwa chini sana milion 250 ilikuwa inatosha kabisa kujenga km 1 ya barabara ya lami kwa kipindi cha kikwete.
 
Naomba nitajie barabara iliyojengwa kwa shilingi bilioni mbili na nusu kipindi cha Jakaya?

Kama kwa sasa pamoja na mfumuko wa bei kilomita moja ya barabara ya lami yenye viwango inagharimu bilioni 1 tu.

Miaka zaidi ya kumi nyuma ujenzi na zana zake kiujumla gharama zilikuwa chini sana milion 250 ilikuwa inatosha kabisa kujenga km 1 ya barabara ya lami kwa kipindi cha kikwete.
Kwa mujibu wa nani,wewe!?..mzee mkapa alijenga kilomita moja kwa bilioni moja,kipindi hicho Dola moja buku,vifaa/malighafi gani za ujenzi zilizoshuka mkuu!?..lami,vifusi,kokoto,mafuta ya mitambo, really!?..kwamba Sasa Bei zipo relatively chini kuliko miaka 18 iliyopita?
 
Barbara kilomita moja ni bilioni mbili unusu,jakaya alijenga kilomita elfu sita,linganisha na mradi wa jnhp ambao magu aliuacha ukiwa 30%

Weka ushahidi kama kikwete alijenga barabara za lami kilomita 6000.

Tatizo mnaona kila mtu ni zuzu humu jamiiforums. Sababu hatujuani.

Kuanzia wakoloni , awamu ya kwanza mpaka leo awamu ya 6. TANZANIA KM ZOTE JUMLA YA BARABARA ZA LAMI HAZIJAFIKA HATA KM 4000.

Je hizo km 6000 kikwete amezijenga wapi ?
 
Barbara kilomita moja ni bilioni mbili unusu,jakaya alijenga kilomita elfu sita,linganisha na mradi wa jnhp ambao magu aliuacha ukiwa 30%

Weka ushahidi kwamba kikwete alijenga km 6000.

Na aliijengea wapi maaana mtandao wa barabara za lami Tanzania nzima kuanzia wakoloni, akaja nyerere mpaka leo hii bado km za kami hazijafika hata km 4000.

Weka ushahidi wa hizo km 6000 za lami zilizojengwa na kikwete
 
Kwa kweli , ingekuwa tunaonana tena baada ya kufa ,,, nisiwe muongo mimi ningeonana na magu ,, ningemzaba kofii ,,,
 
Jakaya alijenga 6000km Barbara za lami,udom,chuo kikui Cha jeshi,pandisha mishahara kila mwaka,boresha muhimbili na Jenga mloganzila,ruzuku pembejeo kilimo,kilimo kwanza,mikopo elimu ya juu bila ukakasi,kumbuka lami kilomota moja ni zaidi ya bilioni mbili za kitanzania,Sasa piga hesabu hiyo miradi ya ujenzi ya magu pesa iliyotumika mpaka anakufa na miradi ya jakaya,Fanya lami tu
Umesahau kuanzisha mradi wa umeme vijijini REA.
 
Back
Top Bottom