Hata mimi mnanichosha pia kwa kutokunielewa; labda nibadilishe tune na hoja iwe hivi:- je kutoa mimba (zygote) kutoka kwa mama mjamzito ni sawa na kuua MTU aliyekuwa hai???--- hii hasa ndiyo mada.
Tumbo la mama ni sawa na kiwanda cha kutengeneza bidhaa, bidhaa ikishaundwa na kukamilika na kukidhi viwango hapo inapata sifa ya kuwa bidhaa kamili, sasa utasemaje mimba iliyotolewa ambayo sio KAMILI IWE NI MTU, Kwani MTU ni nini???---Tafuta definition ya mtu kwanza ndipo uje useme mimba ni MTU.
Maana ya independence in this regard mfano wake ni huu:- Mama mjamzito kwa bahati mbaya akifa na ujauzito je huo ujauzito nao utabaki kuwa hai???, na anapozikwa je husemwa wamezikwa watu wawili au huwa anapasuliwa halafu mimba inazikwa peke yake na mama peke yake???--- nauliza maswali hayo ili uvute fikra zako kwa ukaribu, halafu tugeuze sarafu upande wa pili; kama mimba itakufa na ikatoka (miss carriage) je hiyo mimba itazikwa kwa taratibu zote za mazishi kama anavyokufa mtu independent??, je mbeba mimba naye anaweza kufa katika hali ya kawaida baada ya misscarriage???
Ukimpiga mtu risasi na akafa sio sawa na kuipiga mimba risasi, hiyo itasemwa umempiga mjamzito risasi au mjamzito katolewa mimba yake kwa case hiyo mimba inakuwa ni part ya mwili wa mbeba mimba, na hiyo huwezi kukanusha, huwezi kuitaja mimba bila kumtaja mbebaji na huwezi kutoa mimba hewani ni lazima itolewe kutoka kwa mbebaji.
Nataka andiko kutoka kwenye vitabu vya dini linalosema kutoa mimba ni sawa na kuua mtu, au Mungu alisahau kuleta andiko au hakujua kwamba utoaji wa mimba utakuwepo duniani??
Najua kwamba ili mimba itunge ni lazima sperms zikutane na yai la mama, mimi nilikuwa namjibu mtu mmoja aliyeniuliza kama mimi ningetolewa nikingali mimba ingekuwaje ndipo nikampa mfano wa Sperms za nduguze walioachwa kipindi yeye akiingia ndani ya yai ili aje duniani kama Mtu, hapo tofautisha kati ya Mtu na Zygote.
(Find the difference between man and Zygote.)
Ninaposema independence maana yangu ni independence katika 1---Chakula nje ya womb,2-- Hewa nje ya Womb, 3--- kujitambua nje ya womb, 4--- Hisia nje ya womb nk, hapo sasa huyo ndiye Mtu ambaye ukimuua unayo hatia hata siku ya kiyama atasimama kutoa ushahidi kwanini ulimuua, siku hiyo ya Qiyama naye atakuwa na daraja kama mtu, je siku ya Qiyama mimba zilizotolewa zitakuwa na daraja kama WATU???
Ndicho hicho ninachosema kwamba mimba ikizaliwa tu awe njiti au katika hali yoyote ukiua tu basi wewe unayo hatia ya kuua MTU kwasababu huyo tayari alikuwa na independent life.
Hitimisho:-
Narudia kusema; kutoa mimba bila sababu za msingi ni kosa mbele ya Mungu lakini sio kosa linalolingana na Mauaji ya Mtu.---Haiingii akilini kusema kwamba kutoa mimba ni sawa na kuua mtu anayetembea barabarani.