Pole sana mkuu!
Ila unavyoenda mashariki sijui wapi una watoto wa umri gani? Je mawasiliano ukiwa huko itakuwa vipi?
Hata wazazi kwann usiwasaidie ?
Kibaya ni kutokuishi kwenye mipaka yako! Na kutunza Siri zako!
Tambua hili mbali na kuzaliwa ndugu ama kuwa na wazazi ukitoa huo uhusiano Kuna kitu inaitwa binadamu...
wanakuwa na tabia za kibinadamu kama wizi, uchoyo wivu, roho mbaya regarding na uhusiano ulio nao kwao,
Ukiweza elewa Hilo utajua namna ya kuishi na kila mmoja vizuri,
waelewe ndugu zako, wazazi wako, jua kusema hapana au Nina hiki kidogo
Mkizaliwa ndugu haimaanishi msishirikiane au kusaidiana hapana lakini mkifikia hatua ya kuwa kila mtu na maisha yake hakuna atakayetaka kuwa chini, kama mna familia kila mmoja ataipambania familia yake!
waelewe watu wako, wasamehe walipokukosea, achilia visasi, anza upya!
Ipende familia yako ndo kimbilio Bora na imara wakati wote, wapende wazazi wako maake inaonyesha wewe ndiyo chanzo Cha wao kukuzoea kupitiliza