Najihisi kuchoka na haya maisha ila nigerudisha siku nyuma ningefanya hivi.

Mkuu
Hawana huo uwezo kufeli ni kawaida ila kufikria wamefanya hivyo kwa miujuzi ni imani mbaya .

Hakuna mtu mwenye uwezo huo.
Nilikuwa na misimamo kama yako ila nimeanza kuamin haya mambo yapo. Kuna ndugu nilipowin win nikawa nawaita kufanya nao mishe mishe ila wale watu ni full mambo ya waganga. Show inaanza niliota nitaporomka sana, baada ya hiyo ndoto kilichofuata sijaamini. Hadi leo nakukuruka kurud nilipokuwa. Kuna vitu nimevisikia wale ndg wakisema huko walipo. Haya mambo yapo japo sitakaa niyashiriki. Mungu alivyoniotesha kuanguka naamin ataniotesha tena mwisho wa kuanguka
 
Hayo mawazo ya kwenda mbali kwanini unajiwazia mwenyewe, kwanini usiende na familia yako?? Wewe ukale bata familia yako aangalie nani?
 
Mkuu sio hivyo kwamba wana nguvu ,sioni kama kuna ukweli basi wangetumia huo uchawi wafike juu...Kiasili kabisa bila ya uchawi usipende kutangaza mambo yako ,kama kipato na siri ya mafanikio yako... Inawezekana sio ndugu ila ni asili tu imeamua ,unaweza kufukuzwa kazi ukasema ndugu wameniroga.

Huyo jamaa huku ana ndugu inawezekana anapotesa physically ,kwani anapigwa vizinga na anatoa hilo ni kawaida hakuna uchawi...Tena unaweza kukuta pesa unamaliza kweny matatizo ya ndugu ,wazazi na familia.
 
Mungu akuguse
 
Kujitenga sio suluhisho bali iyo ni ishara moja wapo ya kwamba una matatizo ya akili.

Hebu jaribu kutafuta utulivu wa mwili, akili na roho...........kisha sali kimoyo moyo Sala hii.
"MUNGU NIJALIE UTULIVU NIKUBALI MAMBO NISIYOWEZA KUBADILISHA NA UJASIRI WA KUBADILISHA MAMBO NINAYOWEZA KUBADILISHA NA BUSARA ZA KUTOFAUTISHA, AMIN.

Basi yote yatakuwa sawa, Amin.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…