Najishangaa kwanini ninakuwa na hii roho ya huruma kiasi hiki. Najiona mjinga asee

Najishangaa kwanini ninakuwa na hii roho ya huruma kiasi hiki. Najiona mjinga asee

Ni kweli ndugu, ila kinachokuwa kinasumbua ni kutokua na msimamo juubya maamuzi yangu. Kuna watu huwa wanajiongeza wakati mwingine akiazima akirudi anakuweka mafuta ila kuna raia wagumu asee akiweka wese labda elfu 15 imetoka na unakuta kaenda umbali kabisa. Sasa watu aina hiyo nataka nisiwe nawapa ili watumie usafiri mwingine maana wanpenda mserereko
Hii inaitwa roho ya kinafiki unatoa kitu ila moyoni hupendi .

Basi kuitoa kwako anza kuwa real acha mara moja unafiki haitakuwa shida kuwaeleza ndugu na marafiki kuwa hiki napenda au sipendi .

Pole sana ila uwa hii roho mara nyingi inapona maana kuna matukio yanakufikisha kwenye climax kumwambia muhusika yeyote kuwa sitaki haitakuwa shida tena
 
Ila naona kama nimepitiliza asee!
Ndo ivo mkuu tufanyaje sasa,,,ila kuna watu ukiwasaidia huwa haiumi ni watu ukiwasaidia unajisikia proud ya moyo wako ila kuna watu wanakuwa vichomi sana,,,,mimi niko hivi kumsaidia mtu ambaye namuona anapambana ila katika mapambano yake ndo hali yake imefikia apo bado anahitaji msaada huwa nafeel good sana kumsaidia,,,ila kunahawa ni marafiki nyoka unakuta mko na kazi sawa wewe unajibana unanunua kiusafiri ila yeye zake anatumia mwenyewe kwenye vitu binafsi alafu anataka wewe umsaidie hawa nao huwa nawasaidia ila huku nikifikiria kabsa huyu ni rafiki mnyonyaji
 
Kasome japo basics za Human pyschology, utaona hiyo tabia yako ni mojawapo ya personality traits zako, na ndio zinakufanya wewe uwe wewe na mimi niwe mimi. Wala usijilaumu hata kidogo ndivyo ulivyozaliwa, cha msingi jitahidi kuwaazima wale unaowaamini na wana leseni za udereva.

Mimi nina tatizo hilo hilo, yaani kumsaidia mtu huwa nashindwa kabisa kukataa, mpaka kamkweche kangu kakazungusha injini nikiwa nimewaazima jamaa waende msibani.
tabia ya ovyo hiyo itakupa umaskini usiihalalishe
 
Ungekuwa dem ingekuwa hatari sana.
Vidume vingekuwa vinashika mkono tu
 
Iyo kawaida pia wape tu lift majirani usiwapite njiani utajenga ujirani mwema, ktk kuazima gari hakikisha unaemuazima anakizi vigezo awe na lesseni, awe mzoefu wa gari ajaze mafuta kwa ajili ya misele yake, usimwazime mtu tu ilimradi sio baskeli iyo
Ongea tu kiutani ila ujumbe umfikie siku ya kwanza asipofanya ivo kujaza mafuta tumia fimbo iyo kumchapia
 
awapi kitu easy sana hicho just train yourself to say no bila kuogopa watu watakuchukuliaje
Ngumu sana mkuu, kuna wakati namsaidia mtu wakati unakuta balansi niliyobaki nayo si nyingi sana, ila unakuta mtu ana shida seriuous kabisa.
 
pole hata mimi nipo hivyo nasema simkopeshi mtu lakini hata aliyenirusha bado naenda kumpa
 
Jifunze kusema hapana bila kutoa sababu. Huo sio usafiri wa umma. Na Kama una mpa mtu Basi ni Yule wandani kabisa mnae heshimiana kwa sbb anakueshimu na Mali yako ataieshimu.
 
Habari za kwenu ndugu zangu! Niende kwenye maada moja kwa moja.

Siku za hivi karibuni nimenunua kausafiri ambako kananisaidia kwenye shunting zangu za hapa na pale hapa mjini. Lakini nimenunua huu usafiri baada ya kununua nimekuwa nikipata udhoefu tofauti tofauti ikiwemo kumwazimisha mtu ambapo baada ya kumwazimisha roho yangu inaanza kujutia kwanini nimemuazima na wakati anapokua anaomba naku nataka kukataa ila roho ya kukataa inashindwa na roho ya kumwazimisha. Ila baadae najutia kwanini nakua mrahisi hivi kumwazimisha mtu wakati sina imani naye.

Na hii hali imekua ikinisumbua sana na najiona kama mjinga na hapo unakuta unamuazimisha mtu akirudi hajaweka mafuta anakurudishia funguo ila akili hii haija aacha kubarimdlika nataka niwe nawanyima sijui inatokeaje daah!

Najua hii kitu mnaweza mkaniona kama natania ila deep down najiona fala kabisa. Na kuna wakati najua huyu mtu nimnyime tu maana hawekagi mafuta ila akiniomba muda mrefu nampa roho ya kukataa haipo.

Hii imekaaje au ndio roho wa umasikini ananiandama ? Hapa kuna jamaa nimemuazima ameondoka tu nimeanza kujilaumu sasa hata sijui nikoje. Hii imekaaje aseee kudadeki, najichukia kijinga sasa hivi.
Mie gari siazimishi aisee maana kila mtu ana uendeshaji wake pia mafuta yamepanda bei mno mm huwa napiga full tank mwisho wa mwezi najua nisipotoboa basi angalau siku 20 hadi 25 zinafika nikiwa sijaishiwa mafuta sasa kuna watu wahuni kweli anakwambia hebu naomba gari yako niende mahali flani ukimpa sehem ambayo angeenda kwa mafuta ya elf 20 yeue anaweka ya 10 elf.
Kingine huwa hawajui kuna tyre wear, oil na vingine yeye anakwambia nitaweka mafuta
 
Back
Top Bottom