Najishangaa kwanini ninakuwa na hii roho ya huruma kiasi hiki. Najiona mjinga asee

Ni kweli ndugu, ila kinachokuwa kinasumbua ni kutokua na msimamo juubya maamuzi yangu. Kuna watu huwa wanajiongeza wakati mwingine akiazima akirudi anakuweka mafuta ila kuna raia wagumu asee akiweka wese labda elfu 15 imetoka na unakuta kaenda umbali kabisa. Sasa watu aina hiyo nataka nisiwe nawapa ili watumie usafiri mwingine maana wanpenda mserereko
 
Kosa kubwa kuazimana gari....au pikipiki...akiharibu atasema ulimpa ikiwa hivyo....ugomvi huanzia hapooo
Afadhali hilo kuliko agonge na ukute hata leseni hana
 
Ila naona kama nimepitiliza asee!
Ndo ivo mkuu tufanyaje sasa,,,ila kuna watu ukiwasaidia huwa haiumi ni watu ukiwasaidia unajisikia proud ya moyo wako ila kuna watu wanakuwa vichomi sana,,,,mimi niko hivi kumsaidia mtu ambaye namuona anapambana ila katika mapambano yake ndo hali yake imefikia apo bado anahitaji msaada huwa nafeel good sana kumsaidia,,,ila kunahawa ni marafiki nyoka unakuta mko na kazi sawa wewe unajibana unanunua kiusafiri ila yeye zake anatumia mwenyewe kwenye vitu binafsi alafu anataka wewe umsaidie hawa nao huwa nawasaidia ila huku nikifikiria kabsa huyu ni rafiki mnyonyaji
 
tabia ya ovyo hiyo itakupa umaskini usiihalalishe
 
Ungekuwa dem ingekuwa hatari sana.
Vidume vingekuwa vinashika mkono tu
 
Iyo kawaida pia wape tu lift majirani usiwapite njiani utajenga ujirani mwema, ktk kuazima gari hakikisha unaemuazima anakizi vigezo awe na lesseni, awe mzoefu wa gari ajaze mafuta kwa ajili ya misele yake, usimwazime mtu tu ilimradi sio baskeli iyo
Ongea tu kiutani ila ujumbe umfikie siku ya kwanza asipofanya ivo kujaza mafuta tumia fimbo iyo kumchapia
 
Ukiombwa kataa mambo ya huruma waachie wakina mama.
 
awapi kitu easy sana hicho just train yourself to say no bila kuogopa watu watakuchukuliaje
Ngumu sana mkuu, kuna wakati namsaidia mtu wakati unakuta balansi niliyobaki nayo si nyingi sana, ila unakuta mtu ana shida seriuous kabisa.
 
pole hata mimi nipo hivyo nasema simkopeshi mtu lakini hata aliyenirusha bado naenda kumpa
 
Jifunze kusema hapana bila kutoa sababu. Huo sio usafiri wa umma. Na Kama una mpa mtu Basi ni Yule wandani kabisa mnae heshimiana kwa sbb anakueshimu na Mali yako ataieshimu.
 
Mie gari siazimishi aisee maana kila mtu ana uendeshaji wake pia mafuta yamepanda bei mno mm huwa napiga full tank mwisho wa mwezi najua nisipotoboa basi angalau siku 20 hadi 25 zinafika nikiwa sijaishiwa mafuta sasa kuna watu wahuni kweli anakwambia hebu naomba gari yako niende mahali flani ukimpa sehem ambayo angeenda kwa mafuta ya elf 20 yeue anaweka ya 10 elf.
Kingine huwa hawajui kuna tyre wear, oil na vingine yeye anakwambia nitaweka mafuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…