Najiuliza kwanini badala ya kulaumu watu tunalaumu vyama

Najiuliza kwanini badala ya kulaumu watu tunalaumu vyama

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
7,875
Reaction score
12,665
Chama ni jina lililosajiliwa tu ila wahusika wakuu ni watu ambao ndio watendaji wakuu wa hilo jina au taasisi iliyosajiliwa ili iwe na utajo au utambulisho maalum

Kimsingi CCM na CHADEMA sio tatizo ila watu kwa ujumla ndio tatizo. Ufafanuzi ni kuwa watu huzaliwa na kufa pia huhama hama kutoka taasisi moja kwenda nyingine ni kama timu za mpira usajili ukifanyika vizuri timu inafanya vizuri ila ukifanyika vibaya timu inayumba

Kwenye vyama shida sio chama shida ni watu wanaoshiriki katika chama husika na kwa aina ya watanzania tulionao ni bora tukadeal na fikra za watu zaidi ndio tuje kwenye uchama tusiposhughulika na fikra za watanzania hata kikiingia chama kingine mambo yatakuwa yaleyale;

Uchawa ili mtu achaguliwe kugombea au kuteuliwa katika nafasi fulani, Rushwa hasa kununua wabunge ili Raisi apate support bungeni ili kupitisha agenda za Serikali kama kule Kenya, upigaji utaendelea kama kawaida kwakuwa gharama za kuingia kwenye uongozi kutokana na msururu wa Rushwa ni kubwa kwahiyo kila kiongozi atataka kurudisha gharama zake kama sasa na mambo mengine mengi

Kwahiyo ili tupate reforms za maana tuanze na reforms katika fikra za watu tujenge uadilifu, uzalendo na uaminifu kuanzia kwenye familia hadi kwenye jamii ndio tutapata viongozi bora hata wakiwa chama gani

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom