Uchaguzi 2020 Najiuliza, ni Mwananchi wa aina/fani gani atampa kura Magufuli mwaka huu

Uchaguzi 2020 Najiuliza, ni Mwananchi wa aina/fani gani atampa kura Magufuli mwaka huu

Kabisa Mkuu hawa ni wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara na wahitimu wasiokuwa na ajira ambao pamoja na kudhulumiwa kwa miaka mitano na kuwa benchi lakini bado watampigia kura.
Tumkatae KICHAA
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Watanzania tumeshuhudia maiti za watanzania wenzetu zikiokotwa kwenye fukwe zikiwa zimefungwa mawe na vyuma na nyingine zikiwa kwenye viroba.

Watanzania, tumeshuhudia wenzetu wakitekwa na kupotezwa, wafanyabiashra wakifilisiwa,.

Tumeona ndugu na jamaa zetu wakifunguliwa makesi makubwa na yasiyo na dhamana.

Huyu mtu hatufai kabisa.
 
Wapo wengi tu watakaompigia kura JPM.

Ile hulka yake tu ya kutokuwa mbali na jamii mbali mbali za ndani ya nchi ni sifa tosha ya kupata kura.

Siku zote haweki daraja kati yake na anaowaongoza, anataka aonekane kama ni mwananchi wa kawaida.

Kwa nchi za Afrika ile tabia ya kiongozi kuonyesha kwamba kama ningekuwa na uwezo basi hizi shida zenu zote ningezitatua inatosha kabisa kumuweka karibu na mioyo ya watu.

JPM kaishi maisha yenye ukaribu na watu. Na watu wanayo busara ya kumpima mtu na busara hiyo ndio inayotumika ndani ya chumba cha kupiga kura.
 
Yaani nipo hapa najiuliza sipati jibu ni mwananchi wa fani/aina gani atampa kura Magufuli mwaka huu.
Maana kama;-

WAFANYA BIASHARA.
Hawa wamenyanyaswa sana ndani ya miaka 5 hii iliyoisha, refer msoto wa Manji alioupitia toka Magufuli aingie madarakani na wafanya biashara wengine kedekede, mwenyewe ni mashahidi.

WAFANYAKAZI.
hapa nazungumzia waajiriwa serikalini sekta mbalimbali jinsi walivyovuka kwa shida hii miaka 5 pasi na nyongeza yoyote ya mshahara tena na vitisho au maneno ya kebehi kana kwamba kama umechoka kazi basi acha. Hapa kumbuka kuna wale waliofukuzwa kazi kuanzia ile 2016 (vyeti feki) sijawazungumzia ila naomba niishie hapa.

WAHITIMU WA ELIMU ZA JUU NA KATI.
Hawa ndo hatari tupu, naamini wahitimu walio wengi waliohitimu toka 2015 hawana kazi rasmi labda awe na connection ndo anaweza akaja hapa na kutuambia kuwa amepata permant job serikalini.

WAOMBAJI MIKOPO ELIMU YA JUU.
Hawa nao ni majanga tu mikopo ya elimu ya juu imekuuwa kama betting tu kama huna kismart basi kwisha habari yako.
Hao wanaendelea na masomo na walibett na kupata zali LA mkopo show wameiona mwaka huu kwa kupunguziwa mabomm yao eti kisa Corona.

WAKULIMA.
Huku nako ni chenga tu. Jaribu kwenda Lindi na Mtwara ukaone watu wanavyoteseka na zao la korosho na wengine walidirika mpaka kujinyonga..eti wanaambiwa korosho hawajalima wao wao ni Kangomba.

Heeeeee, hadi nimechoka kuandika jamani ongezeeni na mengine naamini ni mengi sana. Ndio maana najiuliza hapaa huyu Magufuli mwaka huu atapata kura ya mtanzania gani?
Utashangaa jembe na nyundo vitakakavyo ng'ara safari hii. Chadema, tena hii ya Lissu ni nyepesi kama unyoya.
 
HUYU KIUMBE HAFAI KUPEWA TENA NAFASI YA URAIS WA TANZANIA HATA BURE.....ARUDI KWAO AKAMUUGUZE MAMA YAKE MZAZI....KWANI NI LAZIMA AENDELEE KUWA RAIS? KAZI ZIPO NYINGI HATA UGANGA WA JADI UNAMFAA LAKINI SIO URAIS WA TANZANIA.
Ha ha sioni mbadala wa Ccm, kwa miongo kadhaa ijayo. Ukubali ukatae.
 
Wapo wengi tu watakaompigia kura JPM.

Ile hulka yake tu ya kutokuwa mbali na jamii mbali mbali za ndani ya nchi ni sifa tosha ya kupata kura.

Siku zote haweki daraja kati yake na anaowaongoza, anataka aonekane kama ni mwananchi wa kawaida.

Kwa nchi za Afrika ile tabia ya kiongozi kuonyesha kwamba kama ningekuwa na uwezo basi hizi shida zenu zote ningezitatua inatosha kabisa kumuweka karibu na mioyo ya watu.

JPM kaishi maisha yenye ukaribu na watu. Na watu wanayo busara ya kumpima mtu na busara hiyo ndio inayotumika ndani ya chumba cha kupiga kura.
Twenzet octoba 28 [emoji3577]
 
Magufuli atapigiwa kura na wale anaopenda kuwaita wanyonge.

Wanyonge = wananchi wasiojitambua.

Mimi nilishakataa kuwa mnyonge wa ccm tangu Magufuli akiwa waziri hivyo asitegemee kupata kura yangu.
Tukatae kuitwa wanyonge maana Sisi Watanzania hatustahili kuwa/kuitwa wanyonge ndani ya nchi Huru kwa miaka 59.Unyonge haukubaliki,hata Mwl.JK Nyerere alisisitiza kuukataa unyonge wakati anawasha Mwenge wa Uhuru.
Unyonge sasa basi!
 
Back
Top Bottom