Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #41
Ni wewe jinsi unavyojiona ndani mwako. Ni ishara ya utoshelevu wa ndani pia yawezekana ni ukomavu mkubwa lakini pia malezi. Umelelewa kwenye typical Swahili culture iliyojaa mzaha na mchangamano mkubwa na watu tangu utoto? Ni tabia za extroverts watu wasiojiangalia sana na wenye michangamano mikubwa na watu. Umezoea utani kutania na kutaniwa. Kwa ujumla hii ni personality nzuri sana inakupa urahisi wa kuishi na watu na kuwatawala pia kuwa na amani na watu hata kupendwa pia. Watu wa jinsi hii huonekana wenye bahati, huwa na marafiki wengi na huweza kuwa viongozi bila kuchoshwa au kuudhiwa na maoni anuai ya watu. Hongera kama upo hapo ila kuwa mwangalifu usiwe easygoing na insensitive kwa masuala ya msingi.
Kwa sehemu kûbwa umepatia. Ila kipengele cha Malezi Hapo nimelelewa kwèñye familia ya kisabato kikamilifu. Mizaha, matani, masikhara, ushabiki NI mambo àmbayo hayakuwepo.
Mimi ni introvert na mûda mwingine NI Extrovert.
Mimi tangu nikiwa Mtoto sijui Kwa nini siumizwi na maonî ya Watu Wengine kunihusu Mimi.
Kwa mfano, Mimi siwezi kuchukia Waislam Kwa sababu Mimi NI Mkristo ingawaje nililelewa kwèñye mazîngira ya kuchukia Watu wa Dini zingine.
Au darasani Mtu akiwa Mpiga kelele Wengine wakiwa wanamchukia Mimi huwaga sihisi hivyo Moyoni.