Najiweka pembeni juu ya huu Unafiki na Kuonewa wazi wazi kwa KMC FC ili tu Simba SC yangu itengenezewe Mazingira ya Kimagumashi iwe Mshindi wa Pili

Ila Simba SC inayotaka Kubebwa waziwazi na TFF pamoja na TPLB ndiyo inaweza na huko ndiko kwenye Usalama Kwake?
Natetea team Yako braza kaduguda na inabidi kwa Sasa tuwatetee na kuwasaidia kama kipindi kile mlipotaka kushuka daraja
 

Sasa kama mnajua ili kufanikiwa lazima upitie mawimbi, milima, mabonde, giza, n.k kwanini unaleta akili za kuikandamiza Azam au timu nyingine wasishiriki klabu bingwa ili na wao wapitie hizo njia ngumu wajifunze na kupata uzoefu? Yaani unawaza Azam imwachie Simba au Simba ibebwe tu eti kisa Azam hatoweza kufanya vizuri klabu bingwa hizo ni mawazo na upeo wa wapi? Hata Azam anastahili kupitia hizo njia ngumu ili na wao wapate kujifunza na kupata kujua wanapokosea ili na wao wapate mafanikio kama timu zingine na wala sio eti kuifanyia figisu Azam wasishiriki klabu bingwa ndio kuisaidia.

Halafu kingine tunapozungumzia mafanikio au kukua ni hali ya muendelezo wa kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa sio kucheza fainali mwaka mmoja kisa unakuja kuibukia baada ya miaka 20 kwenye robo fainali.
Je hiyo miaka ya 70 unayosemea hivyo vilabu vya Simba na Yanga zilizokuwa zinamuendelezo wa kufanya vyema kila msimu?
Simba tokea msimu wa 2019 hadi sasa hakosekani kwenye robo fainali akisosekana klabu bingwa utamkuta kwenye shirikisho hiyo ndio inaitwa ni muendelezo na ndio mafanikio kinyume na hapo ni kubahatisha. Kama ilivyo kwa Yanga kufanya vyema kwa misimu miwili mfululizo.

Sasa embu nikumbushe hiyo miaka ya 70 ni miaka gani Simba na Yanga zilikuwa na muendelezo kama ilivyosasa?
 
Azam atacheza cafcc hakuna anaepambana kuwapa hiyo nafasi angetaka kucheza Cafcl angeshinda game zake na simba
 
Reactions: 511
Kanuni zinasemaje?
Ukisha notify within muda uliotajwa kwenye kanuni uko safe. Huwezi kumpangia mwenyeji sehemu ya kuchezea game yake. Mwenye maamuzi ya kutumia uwanja ni mwenyeji. Hata akisema anaipeleka game yake Zanzibar utaenda tu ili mradi notification ifanyike kulingana na muda uliowekwa kwenye kanuni.
 
Msimu uliopita huo. Al ahyl alienda CCL Kwa sababu Gani ????? Kama unajua Tena alienda kuchukua ubingwa mbele ya wydad ???? Alimaliza nafasi ya 3 huku pyramid akimaliza nafasi 2 lkn waliona hata akienda pyramid asingeweza kutetea kombe Hilo Kama alivyofanya Al ahly
 
Kwan nan yupo nyumban na nani anatakiwa apange uwanja wa kucheza au ni nje ya hapo maana bado sijaona wap kuna shida
 
Kwan nan yupo nyumban na nani anatakiwa apange uwanja wa kucheza au ni nje ya hapo maana bado sijaona wap kuna shida
Kinacholalamikiwa ni kwamba KMC wanasema kuwa kubadilishwa kwa uwanja haukufuata kanuni kuwa lazima iwe siku 7 kabla ya mchezo
 
Wewe unadhani ligi ingeisha kwa wakati huku Al Ahly akawa ni wa tatu, je wangefosi Al Ahly kwenda kucheza CAFCL?
Kilichotokea ni kwamba ligi ya Misri ilikuwa nje na calendar ya CAF, CAF walikuwa wameanza kusajili vilabu vitakavyoshiriki michuano ya CAFCC na CAFCL msimu mpya na walishaweka ratiba ya mechi za raundi ya awali na raundi ya pili lakini ligi ya Misri ilikuwa bado haijamalizika. Hivyo kilichofanyika ni kwamba shirikisho la soka Misri liliamua kupeleka timu kwa matokeo ya raundi ya kwanza.

Kwanza kitendo tu cha Al Ahly kumaliza ligi nafasi ya tatu ni funzo kubwa sana hata kwetu, ni bahati mbaya tu ligi yao imeshindwa kuisha kwa wakati ili kuendana na ratiba ya CAF.

Usidhani shirikisho za soka zinajiamulia tu kuwa timu fulani iende fulani isiende kwavile hana uzoefu, sheria ni za CAF na imewekwa wazi kuwa bingwa wa ligi kuu na mshindi wa pili ndio wanaotakiwa kucheza klabu bingwa kwa mashirikisho yanayoingiza timu 4. Hivyo hiyo msimamo ndio ungebakia hivyo na wako ndani ya muda wa calendar ya CAF basi Al Ahly ingecheza CAFCC badala ya CAFCL.
 
Kinacholalamikiwa ni kwamba KMC wanasema kuwa kubadilishwa kwa uwanja haukufuata kanuni kuwa lazima iwe siku 7 kabla ya mchezo
KMC FC wako sahihi 100% sema tu kwakuwa Serikali, BMT, TFF na TPLB wanataka Simba SC iwe ya Pili ili wazitumie Kisiasa mwakani kwa Mgombea wa CCM na pia wapige Hela kupitia Uwakilishi wao huko CAFCL. Azam FC ikiwa ya Pili mvuto wa Kisiasa kwa Mama kuzichangia hivi Vilabu Vikongwe na vyenye Ushawishi utapungua na Kuathiri kidogo nia yake ya Kuzitumia katika Kumpaisha zaidi Kisiasa hasa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani ( 2025 )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…