Sijasema watu wavae hivyo nimejaribu tu kuangalia point ya huyo ndugu kuhusu watu kubaka ndugu zao kisa mwili unaonekana! Maana kama ni kweli anachosema itakua hamna aliyesalia enzi hizo!!Tatizo kubwa ni watu kuvaa nguo zisizoendana na sehemu husika....tukiambizana vizuri wahusika watapata msukumo wa kubadilika!Ila tukiendelea kutupiana lawama kama wengi wanavyofanya hatutafika popote!Wanaume watasema wanawake ndo wasababishi wa matamanio yao ya ngono yaliyokithiri wakati wenyewe wanashindwa kujidhibiti!!Wanawake nao japo sio wote watasema wanavaa kwasababu ya wanaume.....Nani hapa atakubali kubadilika wakati anaona sie mwenye kosa???Punguzeni tamaa na kukodolea hao wavaaji macho kama hawatapoteza interest ya kuvaa hivyo!!
Hilo suala la mtu kubaka ndugu yake lina muingiliano na mambo mengine na wala sio kuvaa nguo za kuonyesha mwili pekee.
Linaweza kuwa na mchango mkubwa wa matatizo mengine kama ya akili, malezi mabaya n.k.
Nikirudi ktk maana ya post, bado napenda nisisitize kwamba uvaaji wa nidhamu lazima uzingatiwe.
Wewe unasema tupunguze tamaa, tusiwaangalie hao wanaovaa vinguo vya kubana na kuonyesha mwili, hivi hawa wanawake wa aina hii huwa tunawatafuta ili tuwaangalie au unaweza ukakutana nao popote????
Isitoshe sio kila mwanaume anaweza kujizuia na tamaa zinazotokana na uvaaji wa nusu uchi.
Mtu makini huwezi kufanya kitu unachojua wazi kwamba kitamletea matatizo.
Kama unaweza kuona night club ndio sehemu muafaka kuvaa kihuni basi vaa.
Ila maudhi utakayopata (hutatofautishwa na malaya au changudoa) yasiwe sababu ya kulalamika maana matatizo yake unayafahamu fika.
Kama harusini ndio sehemu ya kuvaa nusu uchi, vaa.
Ila pamoja na yote, mvaaji na aliyetamani wote wana matatizo sawa.