Wakuu hata maandiko yamenena kuhusu hayo kwa siku za mwisho. Sasa hivi wanafanya hivyo kututamanisha na baadaye pale ambapo tutawapotezea aidha wanawake watatubaka au itakuwa kama yasemavyo maandiko haya:- Ukweli kwamba hakuna Kanisa leo linalofuata Biblia na Biblia pekee katika mafundisho wanayoyafuata umeelezwa katika unabii wa Biblia: ?Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.? Isa 4:1. Unabii huu unatuambia kwamba wakati wa mwisho ?saba? (7 kama alama humaanisha [huonyesha] ?wote?, ?ujumla? ,?kamili? mfano: siku 7 za uumbaji, mapigo 7 ya mwisho, miaka 7 ya njaa, n.k.) au YOTE, ?wanawake? (au Makanisa ? Makanisa mara nyingi huwakilishwa kama wanawake katika Biblia; Ufu12:1 dhidi ya Ufu 17:3) ?watamshika mtu mume mmoja? (watadai kuwa na uhusiano na Yesu?ambao Makanisa YOTE hudai kuwa nao leo) ?wakisema, Tutakula chakula chetu [wenyewe]? (Wanakataa Mkate wa kweli wa uzima?Yesu na mafundisho yake, angalia Yoh 6:51, na wanapendelea badala yake ?kula [kupokea]? mafundisho yao wenyewe ya uongo na mapokeo??angalia Isa 8:20), ?na kuvaa nguo zetu wenyewe? (pia wanakataa vazi jeupe na safi la haki ya Kristo na kupendelea mifumo yao wenyewe ya matendo na haki ya binafsi?angalia Isa 61:10; Ufu 3:4, 5, 18) lakini hapa ndipo lilipo jambo la kufurahisha, wote wanasema: ?lakini tuitwe tu kwa jina lako? (wanatamani kwa shauku, bila kujali uasi wao, kutambuliwa kama sehemu ya Kanisa la Mungu, kwa nini?) ?utuondolee aibu yetu.? Hawataki aibu yao na utupu uonwe kwa sababu ya ukweli kwamba wanafundisha mafundisho ya uongo na siyo sehemu ya Kanisa la Mungu, lakini kwa dhahiri ni mojawapo ya binti kahaba wa Babeli!