Najuaje kama imani ninayoifuata ni ya ukweli?

Tafuta kitabu kinaitwa "TUMWABUDU MUNGU WETU", humo kuna Tenzi za Rohoni na Liturgia,kitakusaidia sana kuna maombi mengi mule yametoka kwenye kitabu cha Zaburi na wameonesha kabisa. Kwa Mkristo lakini
 
Kama ni Mkristo, ipime kwa maandiko, yaani biblia. Kama inaendana na vile neno linasema basi ni ya kweli. Ikiwa inakinzana na biblia, si ya kweli.
Kwanza elewa maana sahihi ya neno "Imani", hii ni kusadikisha yale yasioonekana kwa macho. Sasa maana ya imani sahihi itakuwa ni usahihi wa hicho kinachosadikishwa kutoka katika yaliyopotoka mithili yake. Hapa ndo utapata kuna mtu anaamini Mungu ni Sanamu na analiomba limsaidie/limsamehe wakati yeye ana nguvu iliyo wazi dhidi ya hicho anachokinyenyekea. Wengi tutakubaliana hii sio imani sahihi hata kama inafundishwa kutoka kwenye vitabu wanavyovidai wenyewe kuwa ni vitukufu.

Kulingana na tafsiri hiyo hapo juu then utakubaliana na mimi kuwa Imani ya kweli haithibitishwi kwa uwepo wa maandiko kwa kuwa imani potofu pia inaweza kuwa imeandikwa na ikafanyiwa rejea. Bali Imani ya kweli huthibitishwa kwa content yake ambayo hufafanuliwa kwa kile kilicho dhahiri kwa mwanadamu, either kwa kuona ama kusikia mwenyewe kutoka katika source. Hapa pia lazima tuelewane, muujiza ni kwa yule anayeushuhudia muujiza na sio yule anayehadithiwa hadithi ya kuwepo muujiza hapo zamani. Mmoja ameona muujiza na mwengine amehadithiwa muujiza. Ithibati ipo kwa yule aliye shuhudia sio aliyehadithiwa.

Fimbo ya Musa iligeuka nyoka mkubwa na ikawameza wale nyoka wadogo wa kichawi, halkadhalika mitume wengi walifanya miujiza kwa idhini ya Mungu aliyewatuma. Yote haya waliyafanya sio kwa entertainment au kuonyesha umwamba bali kuthibitisha superiority na usahihi ya hiyo imani juu ya huyo Mungu wanaomhubiri.

So imani ya kweli huthibitishwa katika yale yaliyobeba imani, sasa jiulize kilichobeba imani yako ni nini? je wewe umeshuhudia uthibitisho wake ama umehadithiwa?, pia jiulize maandiko matakatifu unayoyaamini yametoka kwa nani (kwa kiwango cha yenyewe hayo maandiko yanavyo jielezea asili yake) na how superior are they compared to other imani zinazodai kuwa na zenyewe ni za kweli pia? kama ile fimbo ya Musa ilivyomeza wale nyoka wa kichawi!

Ila hili linahitaji uwe open minded
 
Hutajua, ni mpaka siku ya kufa utakapokutana na mababu zako wakujulishe imani yao ya jadi ndipo Mungu wa kweli alipo.
 
Eti wakuu?

Majibu yawe mafupimafupi

Fundamentals za dini zote

We tenda haki ishi vizuri na watu na viumbe vinavyokuzunguka. tunzaazingira kwa ajili yako na ya viumbe wengine

Hiyo ndo dini ya kweli
Na Kila miungu itakukubali
 
Asante kwa tafakuri hii kuhusu imani
 
Fundamentals za dini zote

We tenda haki ishi vizuri na watu na viumbe vinavyokuzunguka. tunzaazingira kwa ajili yako na ya viumbe wengine

Hiyo ndo dini ya kweli
Na Kila miungu itakukubali
upo sahihi
 
Back
Top Bottom