Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Mkuu Kuna mambo watu hawayaelewi wanahisi mtu anaamua tu kutokulipa. Nakushsuri ukipata uwalipe. Ili wasiacces contacts zako mamaake uende kwenye settings ukaswitch off permission ya kuaccess contact na app zingine km sms n.k Hapo watakua na contacts mbili tu ulizozijaza km wadhamini. Naurudia tena kiubinadam ukipata walipe
Nia ya kuwalipa mkuu ninayo na Sasa hivi nshafuta App Yao pamoja na kua remove access zote za pesa.x kwenye simu yangu
Lengo ni kutosumbuliwa pamoja na kudhalilishwa wakati huo ntapambana niwataftie pesa Yao taratibu Ili niwalipe Sina Nia ya kuwadhurumu
 
Basi hapo utaishia tu kupata usumbufu wa call na text zao Ila mambo ya group au contacts zako hakuna.
 
Naskia ukifanya chochote wanakutumia meseji hata ukinywa maji wanakwambia "unakunywa tu maji madeni ya watu hulipi" ukicheka unashangaa meseji "unacheka kwa raha gani ulizonazo?" Ukilala meseji inakuja " Unalala kama una raha kumbe masikini".
 
Ulitakiwa uwajulishe mapema kabla ya siku ya rejesho ili kuonyesha uaminifu.
Hawakubali wale.
Tena wanakujibu kwa maneno machafu wakikwambia hizo shida zako sisi tunataka hela yetu.
Hakika loan niliwajulisha siku tatu kabla ya siku ya malipo,ila walinichenjia na wakanitukana juu.
Na sasa siku ya tatu kutoka deadline nilipata hela ila kwa ule udhalilishaji wa mdomo sikuwalipa.
 
Kama hauna mshipa wa Aibu haitakuwa na maana. Ila kama unao lazima uwe na aibu na utaumia nafsi.. Wanakutengenezea group ambalo member ni ndugu zako(ulo save namba namba zote) wanaweka na maneno makali sana (kama Tapeli, muogopeni ni mwizi)
Kuna mwanangu mtoto wa bro alifanyiwa hiyo kitu sijui namba zetu alitoa wapi. Tena hapo anakuwa ameattach kitambulisho chake cha NIDA kisha anaandika hayo maneno ya utapeli.

Halafu alivyo yule muanzisha group ye mwenyewe ndo anakuwa na uwezo wa kuandika.
 
Hawakubali wale.
Tena wanakujibu kwa maneno machafu wakikwambia hizo shida zako sisi tunataka hela yetu.
Hakika loan niliwajulisha siku tatu kabla ya siku ya malipo,ila walinichenjia na wakanitukana juu.
Na sasa siku ya tatu kutoka deadline nilipata hela ila kwa ule udhalilishaji wa mdomo sikuwalipa.
Kuna binti anafanya kazi kwenye hizo taasisi sasa nikamsikia vile anapiga simu kwa wateja kuwakumbusha malipo😂😂ile kazi ni ukichaa maana ni matusi mazito mazito vitisho vingi kumbe hawana lolote, nasikia na Mwamposa nae kajiweka kwenye hizo taasisi na hana riba kubwa na anatoa mpaka laki 2, itakuwa na wiki kadhaa hivi nadhani, sikumbuki jina
 
Hawana kauli za kistaarabu.
Mwanzo walinitisha wakisema ooooh tutapost picha zako nikasema hawanijui.
Nikafuta taarifa zangu muhimu zote.
Kesho yake wananitafuta kiupole,aisee sikuwasikiliza na laini nikavunja.
Walinitusi sana wale mbwaa.
 
Alokopa hadi nikaungwa kwenye group lake akiitwa tapeli huwezi amini anakunja 2.5M kwa mwezi kama mshahara tena take home hiyo na bando kuna vimaokoto vya hapa na pale ila jamaa ana utumiaji mbovu wa hela akajikuta kanasa kwenye vi mkopo vyakijinya kama hivi..
Ilikuwa aibu hadi walokuja kulipa ni Mkuu wa tasisi yao maana nae aliungwa pia kwa hilo group ili kuficha aibu..
😂😂😂 Kulipa Deni la mtu ambae hamuonani ni kazi..
 
Imagine, wachukue no. za wafanyakazi wenzangu wote wawaweke kwenye group plus mademu zangu na ma x 🤣 Alooo, ntahisi kufa mimi
Mimi nimewaza nina namba nyingi za wateja wanaoniamini kwenye biashara yangu,tena wengi tumekutana Online,na wengine hatujawahi hata kuonana ila huwa wananiamnini wanatuma pesa....just imagine wamewaweka kwenye group moja alafu wakasema huyu ni TAPELI nadhani itakua mwanzo wa kufilisika,Mungu niepushe na mikopo ya Online
 
Hahahaaaa waleeee kausha damu fanya jamaa alivyoelekeza hapo juu unblock akafu fyatuka na mwingine walipe ukishalipa watakupa zingine fanyia kazi ikikaribia kulipa fyayua mwingine
 
Kuna mshakaji wng alikopa halafu akakataa kulipa walitumiwa sms mpka wakwe zake ilikua aibu sio poa 🤣
alikua anapigiwa cm za jamaa zake kila dakik mbona tunambiwa umekopa hela hutak kulipa akawa anawambia acheneni nao hao ni matapeli tu.
Hakulipa ata tsh 10 mwish wakachana nae
Huyo ni kauzu zaidi ya dagaa....Hadi wakwe.😂😂😂
Ila sio Kama wameachana naye, wanatabia ya kupumzika kwa muda halafu wanaanza kukuwashia Moto Tena.
 
Naskia ukifanya chochote wanakutumia meseji hata ukinywa maji wanakwambia "unakunywa tu maji madeni ya watu hulipi" ukicheka unashangaa meseji "unacheka kwa raha gani ulizonazo?" Ukilala meseji inakuja " Unalala kama una raha kumbe masikini".
Dooh nimecheka kama mazuri mkuu
 
Back
Top Bottom