Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Ungesajili laini mpya isiyo na majina ili ukopee, au inyime app ruhusa ya kuaccess contacts zako
Line au simu kama hazina majina hawakupi mkopo na usiporuhusu wa access contact zako kabla haujachukua mkopo hupewi
Ila kwa Sasa nimeshafuta hiyo App Yao ...ntatafuta pesa nkipata niwalipe taratibu taratibu
 
Sio lazima waanze na 5,000. Inategemea na sms za miamala watakazoona kupitia line unayokopea. Wakiona cashflow ni nzuri basi wanaanzia pakubwa. Kama Line ni mpya haina historia ya miamala ndio wanaanza na hiyo 5,000
 
Wiki iliyopita si ni li kopa pesa x ikawa natakiwa nirejeshe pesa nusu mara mbili ndani ya siku 14 yani kila baada ya siku Saba nirejeshe.

Sasa rejesho la kwanza lilikuwa jana ila cha moto nakipata! Aloo najuta, sio kwa meseji hizo ninazotumiwa!

Kwani nisipolipa watanifanya nini tofauti na kuwapigia wadhamini wangu?

Pia soma: Nape: Tumewaagiza TCRA wachunguze wale wanaodhalilisha watu waliowakopesha Mtandaoni
Pole sana, Kuna jamaangu Moja kadharirika sana na awo jamaa wa pesa mtandaoni.
Ni kweli shida aina adabu lkn Bora ukawa na shida zako kuliko kuwakopa hawo Jamaa.
 
Pole sana, Kuna jamaangu Moja kadharirika sana na awo jamaa wa pesa mtandaoni.
Ni kweli shida aina adabu lkn Bora ukawa na shida zako kuliko kuwakopa hawo Jamaa.
ASante mkuu, ila Kuna shida nyingine huwez Kaa nazo lazima uzitatue,, niliwakopa Ili niweze ku print research yangu pamoja na.ku bind nisingeweza ku submit research nisingeweza ku graduate huu mwaka,, maana deadline ilikuwa imepita takribani mwezi mzima, ndo nkapewa mwezi mzima Wa kukamilisha research yangu nilikuwa Sina budi kukopa Ela .
 
Mamlaka zimelala,hizi applications zimekua nyingi sana,ni watakatishaji fedha wa wazi..BOT wamechelewa sana kuchukua hatua,hawa jamaa wana ukwasi wa hatari! Wanatumia umasikini na ujinga wa watanzania kuwaibia..
Mtanzania akiwa na shida we mpe form ya vigezo na masharti wala hatasoma,ataishia kusaini tu,na hapo ndio mnapopigwa! Huwezi kuamini wanasema Tanzania kuna pesa za bure..angalia pia kwenye makampuni ya kamari! Na msitegemee hali kubadilika kwa sababu kuna wakubwa wananufaika na pia wapo kwenye payroll ya hawa mabwana.
 
Back
Top Bottom