Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Hii nchi ukiwa na pesa utaendelea kuwa tajiri kwasababu maskini hana mtetezi
 
Ni kweli mamlaka za udhibiti siyo zimelala bali zinanufaika Kwa namna Moja au nyingine....
 
Kama app kwenye simu wanaona kila kitu. Hata wanauwezo wa kujua location uliyopo pamoja na kutumia camera ya simu yako kupiga picha pale unapoitumia simu. Jamaa wana mitambo ya hatari . Hao wachina na wahindi wanaozagaa mjini ndio kazi. zao
Wana uwezo mdogo sio kama huo, binafsi nimewapiga 350k as a trial. Wana teknolojia ndogo na ndio maana wanarely sana kwenye vitisho.

Wanangu wa Ethical Hacking mtanielewa ukishainstall app unamonitor traffick kati ya app yao na server zao utajionea vituko.
 
Hawa mm nmeshapanga siku nitawatafutia simu mpya na namba za nida za mtu mwingne
 
,
,
,
Habari, bado hatujaona ukikamilisha malipo ya deni lako, kama kampuni tunaendelea kukusisitiza ulipe deni lako siku zinazidi kwenda licha ya kukupatia ofa ya kufutiwa penalty ila umekuwa kikwazo kwenye biashara yetu sasa tunakuomba kwa mara nyingine lipa deni lako mapema asubuhi hii kumbuka tupo hatua za mwisho za kukudai hiyo pesa kwakuwa upo nje ya mkataba na makubaliano yetu unatukwamisha pakubwa sana.
 
,
,
,
Kampuni inaendeshwa kwa misingi ya kibiashara na makubaliano na wateja wake tulikuamini sana kwa kujua kuwa kulingana na taarifa ulizojaza kwetu ni sahihi na za kuaminika sasa umetugeuka umechukua mkopo na mpaka sasa tunaona dhumuni lako ni dhuluma umeamua kukaa kimya maafisa wetu wanahangaika kukutafuta ulipe kwa hiyari lakini bila mafanikio sasa tusilaumiane taarifa zako ulizojaza pamoja na wadhamini wako zitapelekwa makao makuu kisha itafunguliwa kesi ya udanganyifu na utapeli mitandaoni hii bila shaka itakuwa ni hitimisho ya safari yetu nawewe kibiashara na usije kulaumu umeonewa muda wa kurejesha hiyo pesa ulishapita na tumekupa ofa ya kuondolewa penalty bado umenyamaza kimya sasa jiandae muda wowote kutoka sasa kwa hatua hii akaunti yako itafungwa muda wowote kuanzia sasa ili kuruhusu mchakato mwingine kuendelea.
 
Pesa x wanasema watanifungulia kesi makao makuu
 
Namba ulizokuwa nazo kwenye simu wao tayari wanazo ... Watakukutengenezea hadi Group la Whatsapp na wataweka hadi picha zako na kiasi ulichokopa .. Yaaan Hadi unakopa tayari ulisha ruhusu wawe na namba zako zote na baadhi ya picha
Nikisajili line mpya kwa ma free lancers bila kutumia namba yangu ya NIDA na contact ni zangu kwa majina tofauti na mke wangu kisha nikawutumia picha ya Usher Raymond watafanyaje!
 
Bado hawaja kukera mkuu hao watatuma meseji kwa contact zoteee za kwenye phone book yako! Kuna jamaa aliwakopa cha moto alikiona hadi boss wake nami nilipata meseji kuwa nime mdhamini. Ilihali sijadhamini
 
Ni nusu Kwa nusu,. Mbona ni kama matapeli tuu. Ila Kwa kulinda heshima yake alipe tuu. Maana nasikia wanatuma meseji Kwa contact zako zote kuwafamisha kuwa mkopaji ni tapeli. Na wenye wasap watatumiwa picha pia
Tatizo watanzania hatuna uelewa wa mambo. Sidhani kwamba kuna sheria ya kutuma message kwa watu kwamba mtu unaye mdai ni tapeli.
Kama mtu kashindwa kurejeshe mkopo , kuna njia za kufuata ku recover mkopo sio hii ya kujumuisha wasio husika. Naona mawakili hawajaona fursa huku.
 
Acha wapigwe tu. Wakati mwalimu wa hesabu anafundisha kuhusu riba wao walikuwa wanakula makamasi. Yaani hapo anarudisha zaidi ya 80% ya hela aliyopokea. Hata kama hiyo hela anaizungusha hawezi pata 80% yake. Watu wengi hutanguliza hisia badala ya kukaa chini na kupiga hesabu kama mkopo unalipika. Kimsingi riba ikishazidi 20% kwa mwezi basi huo mkopo ni ngumu kuulipa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…