Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Bagamoyo port

187207357_824439615118172_3216648188948662793_n.jpg
 
Tatizo la kujenga nje ya mji hata ukisema upangishe hiyo nyumba huwezi pata mpangaji,we unafikiri nani akapange kilomita zaidi ya 35 kutoka town ni ngumu.

Bei tunazonunulia viwanja dsm ni bora ukaenda mkoani utapata kiwanja karibu kabisa na mjini unajenga nyumba yako safi na ukiipangisha hukosi kodi ya 200k au 150k kwa mwezi.

Mfano mkoa kama Tanga ukiwa na million 6 au 7 unaweza kupata kiwanja within 15 kilomita kutoka mjini, ukijenga nyumba nzuri kupata mpangaji ni uhakika. Kodi utakayopata mkoani unaitumia kupanga sinza au magomeni
Watu wengi hawana maarifa yakutosha na mikoani, ukiwa na hela yako nzuri Kwenye real estate ni vizuri kuwekeza huko. Mimi binafsi naona kuwa dar imejaa huwezi pata eneo la maana kwa bei nafuu
 
Daah ulinunua Bei Che Sana Sasa hivi mil 9 hupati kiwanja pale...[emoji26][emoji26][emoji26]
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Kutokana na sasa hela kuwa ngumu nimeweka ukuta mfupi, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba kupitia kwa madalali na Zoom haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.

Enzi za mkwere aka vasco da gama ilikuwa nzuri kwa mafisadi. Hivyo, sioni cha kujutia zaidi ya kupoteza fursa za kupiga walalahoi.
 
Kama mtu ni educated anaweza hata kutembea kwa mguu, ila kama ameenda shule lakini hakuelimika itakuwa ngumu. Maisha wengi yanawashinda kwa kutokuwa na ujasiri wa kujishusha wakati hali inakushusha. Wewe unan'ang'ania juu mpaka tawi linakatika unadondoka ndii. Kama ni kijana let say 30s au 40s anaweza kununua kapikipiki kadogo kakamtoa huko kerege hadi Tegeta nyuki, anakawekesha anapanda daladala yake hadi town. Ila kuamka ni saa 11 kama ameajiriwa

Kongole sana Mkuu. Umetoa bonge moja la pointi. Mungu akubariki sana.
 
Na ataongeza speed ya safari ya kumrudia muumba wake!

Awe makini tu barabarani kwani uhai na umauti upo mikononi ndiye anayeamua nani afe na nani aishi. Kwahiyo kutumia pikipiki siyo paspoti ya kifo.
 
Back
Top Bottom