Najuta kuhamia kwangu Kerege

Kwani kusubiri maana yake ni kumngoja mtu?
 
Nimegundua wengi waliomshaul ni wanafunzi wa chuo wanaopenda maisha ya kwenye video, dume zima ukaona kerege mbali na watu wanakaa moro wanafanya kazi dar nimewazalau kwelikweli
manengelo si mwanafunzi lakini! Nadhani ongeza aggrandizer maana mtu anayepata 200,000 ya uhakika kwa siku ni Prof au waziri etc
 
Unapumzika lini sasa, ikiwa hata siku za mapunziko unafanya kazi ya kubeba abiria?!
 

Me pia nlijifanya nahamia pagale langu kilichonipata mbona nilirudi kupanga
 
Muhindi huwa hapangi nyumba hao unaowaona wapo mjini nyumba za NHC hizo ni nyumba zao walijenga kwa pesa zao nyerere akawataifisha na mababu zao wengine wamefariki kwa presha ya kuzulumiwa soma juu ya nyumba zote za NHC zimeandikwa majina ya wenyenyumba na mwaka waliojenga mfano Patel 1897 zingine Ramesh 1902.wamebaki kushukuru mungu. Ila nyinyi vibanda vyenu vikivunjwa kwa ajili ya utanuzi wa barabara mnaona mmeonewa sana lakini kwa muhindi gorofa kumi kutaifishwa umefurahia sana
 
Mkuu unataka Mungu akupe nin? Acha kufuru.

Uko kwako huwazi kodi lakini bado unalialia. Saivi unauwezo wa kula hela zote bila shida kabisa.

Fanya mpango uongeze kipato.
 
Dada mwenyewe anayesema anapata zaidi ya 200k kwa siku anaishi Kahama, sasa huko kuna biashara gani ya 200k na muda wa kushinda jf

Mkuu usichulie poa, huko mikoani na vijijini ndio hela ilipo.. Dar watu wamekaba kila fursa, unahitaji mtaji wa kutosha kuingia kwenye mbilingembilinge za Dar..

Kahama,Geita, Katoro,Nzega hiyo miji mzunguko wa hela ni mkubwa na kama unacheza karata zako vizuri uwezo wa kuingiza 200K kwa siku upo... Hiyo 200K mbona hata Dar au Mwanza ukicheza draft yako vizuri unaipata??
 
Unajua kuna wakati mtu unaweza kudhani unaokoa gharama kumbe hamna lolote

Sinza kodi unasema unalipia 400,000

kerege usafiri mafuta inazidi 400 tufanye mafuta unatumia ya 500k

ina maana ukitoa 500k mafuta - 400k kodi sinza unapata 100k ambayo hii 100k kwako ndio unaiona kama hasara

Ok tuseme umerudi sinza Kodi utalipa 400k then kazini bado utatumia gari ambapo kwa mwezi utatumia mafuta ya 50k

Jumla ukirudi sinza kwa mwezi utatumia 450k ila kerege ulikua unatumia 500k (umeokoa 50k)

sasa hii 50k kweli ikutoe kwako uone kama adhabu? mimi nadhani hamna unachokikimbia

Baki kerege kwako Pambana nyumba yako uweke ukuta maisha yako yaendeleeee

Siku ukikosa hela ya mafuta una uwezo wa kupanda dala dala ukaenda kazini

ukiwa sinza siku ukikosa KODI huna lugha utayomuelezea mwenye nyumba akakuelewa

Tulie zako Kerege unapaona kama Pagumu ni kwa sababu ni mwanzo tu mkuu ila amini usiamini Kerege ndio OPTION

Huko kwenye majumba ya kupanga trust me utakonda mkuuu,kapumzike zako kerege

Hao vibaka wanakutisha tu siku moja we tengeneza hata baruti ukiwaona Piga chini usku Watajua una CHUMA

hawatorudia hata kupita hapo nnje kwako mchana nakwambia,wanakuja kuja sababu wanakuona mgeni nakwambia

ila usiwaogope pambana nao.

SIKUSHAURI URUDI SINZA maana hamna unachokikimbia.
 
Kwa gharama unaweza kuwa sahihi. Ila socially akiwa Sinza atapata muda wa kuona hata familia. Huko Kerege ndio unaamka SAA 10 watoto wamelala, unarudi SAA 4 watoto wamelala
 
Service ya gari si unaijua mzee..hiyo 14 haitaweza kuservice gari..otherwise labda kama umeamua tu kuwasaidia watu
Service siyo issue mkuu, tena huwa na bajeti yake pembeni! Kinachotafutwa ni ile ahueni ya gharama za mafuta za kila siku za kwenda na kurudi kwenye mihangaiko!

Si umeona hata jamaa analalamikia mafuta yanavyomuumiza, kuna mahali kagusia service?

Service hata usipobeba mtu, utaifanya tuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…