Akili ya biashara wanaiweza Wachaga. Sasa Mhaya atauza nn na mbwembwe zile?
Binafsi Hizi hesabu za Kiwanja kinapanda thamani huwa sizielewi kabisa.
Nakumbuka mwaka juz Kuna Eneo Eka 1 lilikua linauzwa 25mil uko Kibaha-machinijioni.
Jamaa kashaur sana tununue ili tunapakane Jamaa anauza bei Rahisi Mno.
Nkasema, Nkinunua likakaa afu cha kuwekeza sina Itakua HASARA.
Mwenzangu kanunua, Mi nkaendelea na Na Kuimarisha biashara zangu ile 25mil nkaiingiza kwny mzunguko.
Mwezi Ulopita, Baada ya Biashara kuchanganya vizur.
Nmenunua Kiwanja kizur zaidi Ukubwa ule ule pale pale maili 1 kwa 85mil kikiwa na tofali 219 za block
Ila Sijutii, maana kimenunuliwa mda muafaka kabisa kwa ajili ya kukitumia.
Jamaa angu, Biashara zake zimeyumba.
Hana bajeti tena ya kupaendeleza.
Na manispaa wanamzingua kua kama hatopaendeleza ananyang'anywa hati ya umiliki ifikapo DEC mwaka huu.
Kiwanja chake nakiona bado kipo tu kinaendelea tu kusubiri mteja mwezi wa 3 sasa maana katangaza Anauza 75mil.