Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Utaishije nje ya mji kwa kigezo cha kukimbia gharama wakati usafiri wa daladala tu unakucost 150000 kwa mwezi na ukiforce kuendesha gari unatumia laki 4 kwa mwezi?.
Bora upange apartment city centre,nyumba weka mradi wa mifugo na nyumba yako akae msimamizi kama hakuna wapangaji
HhhaahahahahahahahahaahahahahahahahMKUU,
TUPE MWONGOZO KIDOGO KUHUSU HIYO NYUMBA YA NHIF (National Health Insurance Fund) ALIYOKULIA NDUGU_MO.
Pole sana kwa haya maswahibu. Sio jambo jema kujenga nyumba zaidi ya km 20 kutoka sehemu yako ya biashara au kazi.
Nilipoona hii post imenishtua kidogo, maana nimetoka kununua kiwanja juzi tu hapo Kerege CCM. Ila nachoshukuru ni kwamba Dar es Salaam sio sehemu yangu ya Biashara au ajira. Mara nyingi nikiwa Dar ni sehemu tu ya kupumzika.
Badilisha mbinu na mitindo ya maisha. Siafikiani sana na bajaji au bodaboda maana usalama ni mdogo sana kwa umbali huo mrefu.
Kama utaweza chagua siku za kutumia gari yako binafsi kwenda Kazini itafaa. Fikiria labda kwa week utumie gari yako mara tatu au mbili kwenda kazini na siku zilizobakia utumie usafiri wa Umma. Gharama utakazo okoa hapo, wekeza kwenye kuimarisha ulinzi wa nyumba yako na ipendezeshe uipende zaidi.
Au pesa hizo wekeza kwenye biashara ambayo itakuwa mahususi kwa gharama zingine.
Viwanja vya bei rahisi[emoji38]
Viwanja vya bei rahisi[emoji38]
Kuna viwanja vinauzwa 1.3milion huko kisemvule na vikindu, huwa najiuliza kiwanja cha 1.3milion si kitakuwa mbali sana na mjini..yaani kila siku una drive 70km kwenda na kurud kazini..lakin hongera kwa kuwa na Nyumba
Inawezekana wewe umekomaa vigimbi lakini siyo akili,
Nyumba ya million 50 ni Dar na kwa taarifa yako Mimi real estate ndio fani yangu.
Kutoka harusini saa 8 usiku kudrive km 50 huu nao ni zaidi ya uwendawazimu.
Kama umezaliwa kijijini Nyalugusu ni lazimà ushangae swala LA outing, kila MTU na hobby take mwingine disco mwingine live band mwingine matamasha.
Mbona Arusha hamna changamoto za usafiri au haupo Arusha tenaMe pia nlijifanya nahamia pagale langu kilichonipata mbona nilirudi kupanga
acha kuchukulia serious sana jf utaugua vidonda vya tumbo.[emoji1][emoji1][emoji1]
Tahadhari::: fanya kama unayajua magari na unaweza kusimamia kwa karibu, vinginevyo achana na hiyo kitu - najua nimeshawahi na nafanya biashara hiyo..
Hiyo route ya Khm - Ushirombo inalipa lakini gari ipo kwenye risk kubwa hasa hivyo vihiace wanakimbia sana na competion kubwa..
Kama uko vizuri tafuta Tata bus la hata 40mil lipeleke Geita - Kakola - Nzega, litafutie gepu la asubuhi na jioni ligeuke..Kahama to Tabora nako sihaba ..
Narudia tena:: biashara ya magari inahitaji roho ngumu, uvumilivu, ukaribu wa biashara, roho mbaya kwa madereva na makonda, uyajue magari na tabia zake..
Vibaka washabeba smart TV na laptop imebid nisinunue vingine mpaka ntakapoweka ukuta na electric fence
Dadaangu kajenga huko huko mitaa ya baobab sec school, ndani ndani ni anajutraa balaa, nae kapakimbia!
Dar moro masaa mawili hadi matatu kwa private ..lakini Posta Chanika inaweza chukua hadi saa tano kutegemeana na barabara ilivyo hiyo siku. So sijaelewa point yako unaongelea umbali au matumizi ya muda barabarani.
Kwanini nyumba za kupangisha zimeshuka bei tofautu na kipindi cha kikwete? Leo maeneo ya sinza, kijitonyama, kinondoni, nyumba zimeshuka bei alaf madalali wamekuwa wachache
Tatizo la kujenga nje ya mji hata ukisema upangishe hiyo nyumba huwezi pata mpangaji,we unafikiri nani akapange kilomita zaidi ya 35 kutoka town ni ngumu.
Bei tunazonunulia viwanja dsm ni bora ukaenda mkoani utapata kiwanja karibu kabisa na mjini unajenga nyumba yako safi na ukiipangisha hukosi kodi ya 200k au 150k kwa mwezi.
Mfano mkoa kama Tanga ukiwa na million 6 au 7 unaweza kupata kiwanja within 15 kilomita kutoka mjini, ukijenga nyumba nzuri kupata mpangaji ni uhakika. Kodi utakayopata mkoani unaitumia kupanga sinza au magomeni