Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Ndio maana nasema, kumiliki kiwanja ni biashara ya kimasikini. Kama una idea ya biashara bora uizungushe hiyo hela ule matunda yake ukiwa kijana.

Ukikimbilia kumiliki kiwanja utakufa masikini na ndugu yako waje kuuana kisa mirathi.

Wanasema kiwanja kinapanda bei ila wanasahau kuwa inflation nayo inagonga vilevile.

Utakuta mtu anakwambia alinunua kiwanja 1M miaka 10 badae anauza kwa 10M. Hapo anasahau kuweka time value of money.
Umefumania milioni kumi na tano,umeajiriwa,muda wa kufanya mambo yako binafsi ni mchache sana hivyo huwezi kusimamia biashara. Swali,anayeamua kujenga hata kama siyo kwa kumaliza na atakayefanya biashara katika hali kama hiyo nani anazika pesa mkuu
 
Pole sana kwa haya maswahibu. Sio jambo jema kujenga nyumba zaidi ya km 20 kutoka sehemu yako ya biashara au kazi.

Nilipoona hii post imenishtua kidogo, maana nimetoka kununua kiwanja juzi tu hapo Kerege CCM. Ila nachoshukuru ni kwamba Dar es Salaam sio sehemu yangu ya Biashara au ajira. Mara nyingi nikiwa Dar ni sehemu tu ya kupumzika.

Badilisha mbinu na mitindo ya maisha. Siafikiani sana na bajaji au bodaboda maana usalama ni mdogo sana kwa umbali huo mrefu.

Kama utaweza chagua siku za kutumia gari yako binafsi kwenda Kazini itafaa. Fikiria labda kwa week utumie gari yako mara tatu au mbili kwenda kazini na siku zilizobakia utumie usafiri wa Umma. Gharama utakazo okoa hapo, wekeza kwenye kuimarisha ulinzi wa nyumba yako na ipendezeshe uipende zaidi.

Au pesa hizo wekeza kwenye biashara ambayo itakuwa mahususi kwa gharama zingine.
Usafiri wenye afadhali ni piki piki japo usalama wake siyo mzuri sana. Angeuza hiyo gari anunue piki piki
 
Sema Moro to Ubungo, au kimara na kibamba. Kama utafanya reference hiyo, utatoka moro saa kumi..utafika ubungo saa moja asubuhi.. utafika posta saa tatu.
Kuna mtu anatoka kiluvya hadi kurasini anatumia masaa 3 kwenda na 3 kurudi.

Foleni hiyo tena anatumia public transport.

Hapo anajitapa anakaa kwake.
 
Umefumania milioni kumi na tano,umeajiriwa,muda wa kufanya mambo yako binafsi ni mchache sana hivyo huwezi kusimamia biashara. Swali,anayeamua kujenga hata kama siyo kwa kumaliza na atakayefanya biashara katika hali kama hiyo nani anazika pesa mkuu
Ningekuwa nimeajiriwa, hata ningepata 10M, ningeacha kazi right away na kufocus kwenye biashara 24/7.

Watu wanaacha kazi kisa tu amepata 5M mtaji wa biashara sasa wewe wa 15M inakuwaje hapo?

Ishu ni suala la determination, focus na hard working. 15M ni mtaji mkubwa sana wa kutengeneza cashflow ya 10-15M na faida ya 2-3M kwa mwezi.
 
Kama mtu ni educated anaweza hata kutembea kwa mguu, ila kama ameenda shule lakini hakuelimika itakuwa ngumu. Maisha wengi yanawashinda kwa kutokuwa na ujasiri wa kujishusha wakati hali inakushusha. Wewe unan'ang'ania juu mpaka tawi linakatika unadondoka ndii. Kama ni kijana let say 30s au 40s anaweza kununua kapikipiki kadogo kakamtoa huko kerege hadi Tegeta nyuki, anakawekesha anapanda daladala yake hadi town. Ila kuamka ni saa 11 kama ameajiriwa
Mkuu ni ujinga tu, umesema kweli, ma poyoyo wengi wanadhani kuwa na gari inakubeba kila siku ni akili,kumbe ujinga, tembeza mwili kwa miguu ni afya, unang'ang'ania gari inayokusababishia maradhi kibao

Tuelimike jamani, Kama umejenga amua ukae huko au ukae kwengine nyumba yako ipo tu haiyendi popote Kerege kutachangamka japo sio leo.

Aliyetoa ushauri wa kutumia daladala amekusaidia, chukua ushauri. Gari sio fahari ni maradhi
 
Ningekuwa nimeajiriwa, hata ningepata 10M, ningeacha kazi right away na kufocus kwenye biashara 24/7.

Watu wanaacha kazi kisa tu amepata 5M mtaji wa biashara sasa wewe wa 15M inakuwaje hapo?

Ishu ni suala la determination, focus na hard working. 15M ni mtaji mkubwa sana wa kutengeneza cashflow ya 10-15M na faida ya 2-3M kwa mwezi.
Sikukatalii mkuu ila hiyo mentality ni wachache sana wanayo. Kuna watu kibao humu wanakuja kuomba wazo la biashara ya 50mil,ni mweupe kichwani utadhani katokea sayari nyingine muda si mrefu.
 
Ndugu katika maisha ukisema uige mtu husogei....nmchukua mkopo nkatoa kitu mwandege navutia kasi tu mwendokasi uje wakati now nakula daladala zangu mwandege posta...i..wakati kuna jamaa zangu walibeba mkopo wakanunua harrier tako la nyani now linawala tu mafuta.....watu wanapiga kelele za kupanga nyumba sinza sijui tabata hawajui hizo ni investmwnt za wajanja miaka 20 nyuma na miji inakua kwa kasi.....nakumbuka maza alinambia mbezi beach pale makonde tu walikua wanalazimishwa kununua kiwanja...mwisho wa siku akili ya kuazima changanya na yako
Mkuu mwandege town kabisa pale
 
Mkuu ni ujinga tu, umesema kweli, ma poyoyo wengi wanadhani kuwa na gari inakubeba kila siku ni akili,kumbe ujinga, tembeza mwili kwa miguu ni afya, unang'ang'ania gari inayokusababishia maradhi kibao

Tuelimike jamani, Kama umejenga amua ukae huko au ukae kwengine nyumba yako ipo tu haiyendi popote Kerege kutachangamka japo sio leo.

Aliyetoa ushauri wa kutumia daladala amekusaidia, chukua ushauri. Gari sio fahari ni maradhi
Kwa hiyo kwa kutokua na gari hautaugua kamwe. Akili za wabongo kama Kamongo. Tunaishi kama digidigi huko maporini
 
Sikukatalii mkuu ila hiyo mentality ni wachache sana wanayo. Kuna watu kibao humu wanakuja kuomba wazo la biashara ya 50mil,ni mweupe kichwani utadhani katokea sayari nyingine muda si mrefu.
Kama ukitaka kuishi mbali kama huko Kerege, unatakiwa uwe na cash flow ya uhakika na utengeneze modality ya kutopoteza muda wako kwenye mafoleni.
 
Masaa mawili- matatu kufika kazini/nyumbani
 
Back
Top Bottom