Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Ningekuwa nimeajiriwa, hata ningepata 10M, ningeacha kazi right away na kufocus kwenye biashara 24/7.

Watu wanaacha kazi kisa tu amepata 5M mtaji wa biashara sasa wewe wa 15M inakuwaje hapo?

Ishu ni suala la determination, focus na hard working. 15M ni mtaji mkubwa sana wa kutengeneza cashflow ya 10-15M na faida ya 2-3M kwa mwezi.
Unawaambia watu ambao mmoja kasema anapata 200k Kwa siku wamemshambulia hadi kabadili gear angani? Hawawezi kukuelewa
 
Posta Mpya. Dar
mkuu jipange tu magari ya kwenda town (makumbusho) yapo mengi sana ukidamka..pia wakati wa kurudi yapo ingawa ukichelewa fika makumbusho (kumi na moja na kuendelea) yanakuwa yakugombania kaa ya mbagala, kutoka kwako kwenda kituoni chukua bajaji gharama zake kidogo sana ukilinganisha na unavyongurumisha gari hadi town (km 80 approx kwenda na kurudi)
 
Mimi nakushauri kama una mchumba muoe maana kuoa ni ulinzi wa nyumba, ni rahisi hata kufuga maana dada wa kazi atakuwepo na kaka wakutunza mifugo so mchana kutakuwa na usalama na mchumba kama hafanyi kazi atasimamia mifugo, mfungulie na biashara maeneo ya huko huko utaona faida ya kuoa kama ukipata mwanamke mwenye akili na mpambanaji
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
 
1. Kwasababu hujui thamani ya muda, ndio maana unaona sawa kukaa masaa 3 kila siku.

2. Hujui thamani ya pesa, hiyo hela unayoiweka kwenye kiwanja usubiri ukiuze miaka 30 mbeleni ungeizungusha kutengeneza cashflow ambayo utajenga nyumba mjini hapahapa.

Binafsi nina nyumba mbele ya tegeta sijahamia bado kwasababu ni mbali na shughuli zangu. Nafikiria kuiuza.
Ndugu, tegemea kuitwa kila aina ya majina kwa wajuaji ila kwa tunaojua thamani ya kuizungusha pesa ilete mrejesho wa maana zaidi tunakuelewa.
 
jamani tenganisheni UKWELI na UONGO
enzi za Mkwere mwenzako kajenga sasa hali ni ngumu hata mpangaji hapati
Eti wewe una sema leo biashara imechanganya, ni ipi hiyo? maana hata ya kutakatisha pesa, ngada na mashuzi zote HAZITOKI Chinga wote wanalia, wewe ukanunue kiwanja 85m bila taarifa TRA
Tafuta waraka wa fedha kuhusu zaidi ya 10M popote ni lazima uitolee maelezo (huwezi nikubandikie sasa hivi uisome)
wewe unasema mwezi uliopita, hata aliyekuuzia angeshajieleza kwanini KODI hamjalipa
Mleta Mada kasema ukweli tuliobaki ni matajiri nyuma ya keybody
Usikariri, kama kwako hayaendi usifikiri hayaendi kwa wote. Binafsi kipindi cha Mkwere nilikula maisha kwa pesa ya mzee, pesa hasaa ikaja ikakata tukala msoto haswaaaa! Ila sasa hivi ninajimudu vilivyo kipindi hiki, ninatengeneza pesa.

Usikaririshwe, mfano mdogo tu, angalia sasa hivi namba za gari zimefikia herufi ipi.
 
Usikariri, kama kwako hayaendi usifikiri hayaendi kwa wote. Binafsi kipindi cha Mkwere nilikula maisha kwa pesa ya mzee, pesa hasaa ikaja ikakata tukala msoto haswaaaa! Ila sasa hivi ninajimudu vilivyo kipindi hiki, ninatengeneza pesa.

Usikaririshwe, mfano mdogo tu, angalia sasa hivi namba za gari zimefikia herufi ipi.


Nikiwa sema zamani...hiki ni kipindi cha kutengeneza matajiri wapya km mtu unajiweza!unajua sie wabongo nimekuja jua kitu kimoja..runapenda shortcut...ss km era hzi hazitak short cut kwann uendelee kufanua hvyo??lols!ukiwa na documentation zainazohitajika kila kitu kinakaa sawa!
 
jamani tenganisheni UKWELI na UONGO
enzi za Mkwere mwenzako kajenga sasa hali ni ngumu hata mpangaji hapati
Eti wewe una sema leo biashara imechanganya, ni ipi hiyo? maana hata ya kutakatisha pesa, ngada na mashuzi zote HAZITOKI Chinga wote wanalia, wewe ukanunue kiwanja 85m bila taarifa TRA
Tafuta waraka wa fedha kuhusu zaidi ya 10M popote ni lazima uitolee maelezo (huwezi nikubandikie sasa hivi uisome)
wewe unasema mwezi uliopita, hata aliyekuuzia angeshajieleza kwanini KODI hamjalipa
Mleta Mada kasema ukweli tuliobaki ni matajiri nyuma ya keybody



Mkuu kwa taarifa yako sasa hv huko nje hela zinapatikana vzr tu!usikariri
 
Japo sipajui huko kerege lakin naona huna tofauti sana na mm nae ishi mkuranga Pwani halaf unapiga mishe mikocheni Dar.
Though binafsi napenda sana kuishi nje ya mji and am comfortable that way.
Natumia usafir wa umma na nafika kwa kibatuani saa 7:30am natoka home saa 5:00am.
Ila inachosha sana kiasi kwamba weekend unapumzika mpaka sio vizur yan
 
Ukijenga maeneo ya ndanindani mbali na barabara kuu kwa maeneo hayo,
Yabidi shughuli zako ziwe maeneo ya jirani, kama vile Bunju au Tegeta Nyuki.
Kweli km8 kutoka barabarani ni nyingi sana ukiamua kwenda kukaa mbali basi bora katibu na barabara kubwa
 
Kweli km8 kutoka barabarani ni nyingi sana ukiamua kwenda kukaa mbali basi bora katibu na barabara kubwa
Karibu na barabara kubwa ili upanuzi wa barabara ukitokea wakuondoe?
 
Kwa Dar kwa mfanyakazi wa kawaida kutaka ujenge nyumba kiwanja utapata kilomita 40 au zaidi nje ya mji ujenge.

Mbaya zaidi ofisi nyingi ziko posta hivyo itakulazimu uwe unaamka sa 9 ili kufika ofisini sa 2, na kurudi nyumbani ukitoka sa 11 unafika sa 3. Hii sababu ni moja tu ya miundombinu mibovu kwa hapa Dar es salaam, barabara ya kuja na kutoka mjini ni zile zile hakuna njia mbadala na kama zipo ni za hovyo sana.

Mimi Dar siwezi kujenga, ni hasara tupu, ggharama za usafiri kutoka kwako hadi kazini ni zaidi ya 200,000 kwa mwezi, hujaja chakula, uusumbufu mwingine alafu niwe najisifu tu eti kisa nakaa kwangu.

Nenda kinyerezi, mbezi makabe, goba, mabwepande na kwenda huko Mapinga, mbweni, kitopeni, nk watu wametelekeza nyumba nzuri kule kwa sababu ya adha ya usafiri.

Bora upange jirani na mjini uishi kwa raha kuliko kua na kwako huku unaishi kwa shida kisa unaishi kwako. Kuna mshikaji wangu kajenga huko kimara porini imebidi akimbie nyumba, akapange apartment kariakoo.

Mimi nimepanga jirani tu na kazini kwangu, kilomita 8, hata sa 1:30 natoka kwangu na nafika kazini kabla ya ya 2:00 na maisha ni matamu sana.

Maisha ni hesabu, ukifanya miscalculation maisha yako yatakua magumu sana.
Point of correction Kimara sio porini na pia kutoka kimara Mwisho stendi ya mwendokasi mpaka posta ni Km 16 hivyo sio mbali kama maeneo ya Mbweni au Madale. Aliyejenga Kimara mie simlaumu hata kidogo
 
Hapa umenisema kabisa. Nimeacha nyumba kubwa nzuri Msumi nimerudi NHC Ubungo kodi laki mbili . Kule mafuta kwa mwezi laki nne bado foleni, kuchelewa kulala na kuwahi kuamka. Watoto huwaoni hadi weekend. Juu ya yote gharama za maisha bidhaa bei juu sana . Tufikirie sasa vertical building extension.
Ahahahah.Hapo kwenye kuwaona watoto ndio haswaa.Binafsi toka tumalize jumapil pamoja sijaonana nao leo inaenda siki ya pil.Angalau firs5 born yy huwa anawah kuamka kujiandaa shule atleast mnaweza gongana alfajir au usiku akichelewa homework zake.Wengine ni mpaka Mungu apende kama sio weekend.
So sad

NB:
Niliamua kujenga na kuhamia huku cz wife yy ni mtumishi wa serikal na so tulikua temeke but nikaona kwake ingekua mateso sana kwennda na kurud kazin plus kazi za nyumbani na ku take care watoto ingekua ishu.so nikaona acha mm ndio nipambane na hali ili wife awe jiran na ofis.
 
acha usiwafuate waswahili wanaopenda Mjini.
Hapo Kerege patajakuwa Mjini kati kabisa, mwaka 1979 Sinza Makaburini ndio palikuwa mwisho wa Mji wa DSM linafuata pori hadi UDSM
Leo Kibaha ni Mjini kabisa ngoja hiyo njia 6 ya Highway km hukona mwendo kasi halishii Kimara
Ardhi ni mali huwezi linganisha Ardhi yenye ukubwa sawa kwa Miji ya Tanga, Dodoma au Mwanza
Tafuta wenyeji, Mkiti au Mjumbe wakutafutie wapangaji hiyo ni Rasilimali kubwa kuliko kupanga km Mhindi Mjini, Shika ardhi popote km Elimu kwani ni utajiri kuliko hao wezi wa leo tu
Halafu watu manakaa MAPINGA na wanapiga kazi mjini. Ni mipango tu na wala sio mbali kihivyo. Na soon mwendo kasi nayo itakuwa road ya tegeta hakutakuwa mbali kihivyo kama watu wanavyofikiri.
 
Back
Top Bottom