Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Hakuna kitu muhimu kama kutafuta right and perfect site, yaani usikurupuke kabisa... Ni sawa na kutafuta mke coz huko ndiyo utamalizia maisha yako, hasa kwa sisi walio wengi wasio na uwezo wa kujenga majumba mengi.
Dada yangu kajenga huko huko mitaa ya baobab sec school, ndani ndani ni anajutraa balaa, nae kapakimbia!
 
Let's assume hypothetically wafanyakazi woote wa Dar wawe wanaishi jirani na makazini kwao, in this case Posta... Nini kitatokea??
Kwa Dar kwa mfanyakazi wa kawaida kutaka ujenge nyumba kiwanja utapata kilomita 40 au zaidi nje ya mji ujenge.

Mbaya zaidi ofisi nyingi ziko posta hivyo itakulazimu uwe unaamka sa 9 ili kufika ofisini sa 2, na kurudi nyumbani ukitoka sa 11 unafika sa 3. Hii sababu ni moja tu ya miundombinu mibovu kwa hapa Dar es salaam, barabara ya kuja na kutoka mjini ni zile zile hakuna njia mbadala na kama zipo ni za hovyo sana.

Mimi Dar siwezi kujenga, ni hasara tupu, ggharama za usafiri kutoka kwako hadi kazini ni zaidi ya 200,000 kwa mwezi, hujaja chakula, uusumbufu mwingine alafu niwe najisifu tu eti kisa nakaa kwangu.

Nenda kinyerezi, mbezi makabe, goba, mabwepande na kwenda huko Mapinga, mbweni, kitopeni, nk watu wametelekeza nyumba nzuri kule kwa sababu ya adha ya usafiri.

Bora upange jirani na mjini uishi kwa raha kuliko kua na kwako huku unaishi kwa shida kisa unaishi kwako. Kuna mshikaji wangu kajenga huko kimara porini imebidi akimbie nyumba, akapange apartment kariakoo.

Mimi nimepanga jirani tu na kazini kwangu, kilomita 8, hata sa 1:30 natoka kwangu na nafika kazini kabla ya ya 2:00 na maisha ni matamu sana.

Maisha ni hesabu, ukifanya miscalculation maisha yako yatakua magumu sana.
 
Maamuzi magumu kama haya unayoshauri yanataka ujasiri na roho ngumu, hasa kwa vijana wa kizazi kipya....
Mkuu uza hiyo gari tafuta Toyota hiace ya 15milion, Asubuhi unapokuja mjini beba abiria, unaporudi kerege pia beba abiria. weekend aamka asubuhi piga trip kazaa tegeta bagamoyo.. Hapo utakuwa umejiongezea kipato lakini pia utakuwa umepata hela ya mfuta kila siku ya kuendea kazini..
 
Hakuna kitu muhimu kama kutafuta right and perfect site, yaani usikurupuke kabisa... Ni sawa na kutafuta mke coz huko ndiyo utamalizia maisha yako, hasa kwa sisi walio wengi wasio na uwezo wa kujenga majumba mengi.
Kerege kesho kutwa tu panakuwa town, hajakosea sana
 
Kuna biashara mtu mzima ukizifanya hutoboi kama hiyo ya turnout 200k kwa mwezi siwezi kuigusa
Huku JF kila MTU ni tajiri sana...yaani 200k kwa mwezi ni umaskini?yaani ukweli ulivyo hiyo ni hela ndefu sana na kwa taarifa yako ni wachache mno hapa JF wanayoifikia hiyo pesa kwa mweziii ....
 
Huku JF kila MTU ni tajiri sana...yaani 200k kwa mwezi ni umaskini?yaani ukweli ulivyo hiyo ni hela ndefu sana na kwa taarifa yako ni wachache mno hapa JF wanayoifikia hiyo pesa kwa mweziii ....

Kabisa mkuu!
 
Huku JF kila MTU ni tajiri sana...yaani 200k kwa mwezi ni umaskini?yaani ukweli ulivyo hiyo ni hela ndefu sana na kwa taarifa yako ni wachache mno hapa JF wanayoifikia hiyo pesa kwa mweziii ....
Wachache mno?! Umefanya sensa ukajua vipato vya wana JF hadi ukafikia hitimisho hilo?
 
Mkuu vumilia zamani hata Kimara palikuwa shamba na mbali na mji.Tulikuwa tunapishana na viboko na nguruwe.
Usiuze hiyo nyumba utajuta baadae cha kufanya tafuta chumba panga karibu na kazini kwako.Hiyo nyumba ya Kerege tafuta mwenyeji mswahili wa huko muache akae hata bure akulindie mji.
Mimi sijuti kununua viwanja Kimara mwaka 1969 sasa hivi mimi ni kamfalme kadogo
Maendeleo ya majengo na miundo mbinu yanamfuata mtu sio kinyume chake
Duh hongera Mkuu, sahiv una miaka Mingap kiongozi? Asante
 
Back
Top Bottom