Umesema yote Mkuu.
Wengi wa sisi watanzania hawapendi kutumia akili zao kuchambua mambo. Wanaendeshwa na hisia au mihemko.
Kuna uwezekano huyu ndugu yetu alikuwa kizuizi kwao hivuo ni lazima wangemuondoa tu. Sasa tujiulize amewazui nini hao jamaa?, na kwanini?.
Nikimuangalia ni Mmaasai na kuna hii kasumba ya watanzania baadhi hasa wa ukanda wa kaskazini kujiita wayahudi weusi au wayahudi waliopotea na kujinasabaisha na israeli, sio ajabu na huyu alikuwa huko. (Sijasema nimewaza)
Bado kuna hawa watanzania watu wa dini wao ni kuvaa nguo zenye bendera ya israeli, mara waweke kwenye magari kama sticker au vitambaa hadi makanisani inapeperushwa bendera ya taifa lingine bila utaratibu. Hawa nao wakija kupigwa bomu wataanza kulalamika hovyo. Huwenda na huyu alikuwa na vazi au sticker ya hivyo kwa misingi ya kiimani (Sijasema nimewaza)
Mambo ni mengi sana hasa ukizingatia aliyetangazwa kuuawa kipindi chake hichi alikuwa askari wa Israeli, kazi maalumu. Labda na yeye pia who knows! kwani si tumeona watanzania wa huko Urusi kilichotokea.
Tukitumia akili hili jambo sio dogo hata kidogo.
Ukiangalia hizo video ni dhahiri ipo namna aliwakwaza hao jamaa, huyo anayemuuliza swali sijui ni kumfokea, huyo sio chizi kwamba amfokee au kumuuliza maswali mwanafunzi asiyejua kitu, mtu mweusi kutoka Afrika, tena Tanzania. Sio rahisi
Watu wakiwa kwenye kazi zao usijihusishe nao. Utajiponza.