Najuta kuoa Single mother, kila nikimtazama huyu mtoto wake Moyo wangu Unaumia kwa machungu makali. Nahitaji msaada

Single mother wanateseka sana, me nna rafiki yangu wa kike nlikutana naye chuo, Yeye alipewa mimba akiwa form four na mwanafunzi mwenzake, mpaka leo ana miaka 30 bado hajapata mtu serious, amepita kwenye r/ship kadhaa wahuni wanakula Mzigo wanakimbia, Sahv amekata tamaa analea mtoto wake ambaye yuko form one
Ukimuangalia kwa muonekano wa nje ni mkarimu sana, beautiful ila mpaka sasa yuko kitaa
 
Angekuwa ni mwanamke ameolewa mwanaume mwenye mtoto akawa anapitia changamoto kama hizi ungetoa ushauri mwingine au ndo huu huu both sides?
Kitu cha kwanza wanawake kinachowaangamiza ni kujilinganisha na mwanaume,Mwanaume na mwanamke ni viumbe 2 tofauti kuanzia tabia mpaka akili.Mwanaume ana uwezo wa ku control mambo-mwanamke hana uwezo huo.Mtoto yoyote kwa sheria za kidunia na kidini ni wa Mwanaume na sio wa Mama hii ni duniani kote.so,mfano wako hauna mlinganisho sawia.
Vilevile,wenzetu wazungu mtu anaweza oa mwanamke mwenye mtoto na isitokee hata siku moja akawa na mafungamano na mzazi mwenzake hii ni tofauti na wanawake wa kiafrika-hivyo,ni risk kuoa mwanamke mwenye mtoto kwa Afrika.
 
Nashukuru sana. Vipi wewe kama Mzazi utakubali mwanao akuletee mwanamke mwenye mtoto ikiwa yeye Hana?
 
Kila siku anatusanua Kuna neno huwa analitumia ana sema tusiwe masimp

Angalia sasa ndugu yetu ana Lia Lia wakati angemsikiliza Natafuta Ajira haya yote yasinge mkuta

Mimi kuanzia nianze kumsoma huyu jamaa nimekuwa makini sana na hawa single maza
A simp is a shame to his friends, parents and ancestors
 
Kichwa Cha habari kimejieleza kabsa Mkuu labda kama hujasoma, umekimbilia kutoa comment.

Kuhusu upande wazazi. Niwe Mkweli wazazi wangu hawakuridhia nioe huyu mwanamke ni ukaidi wangu tu ndiyo umepelekea yote haya.
 
Mkuu najilazimisha sana kumpenda huyu mtoto lakini nafsi yangu imegoma kabsa. Na sijui nifanyeje.
 
Utoto unakusumbua,miaka ya 60 kuna mzee alioa mama wa watoto wawili kwa mwanaume mwingine,yule baba wa watoto alienda pwani kutafuta maisha,baba wa kambo alilea kwa miaka kumi hawa watoto mpaka walipochukuliwa na baba yao,huko pwani walisoma,wakawa na maisha, watoto wa baba wa kambo hawakusoma,wale watoto hawakumsahau baba wa kambo,alipougua waligharamia matibabu kwa kuwa watoto wa baba wa kambo hawakuwa na uwezo,alifariki,waligharamia mpaka mazishi,kabla walikua wakimkumbuka kwa mavazi na sukari
 
Hakika mwanzo shida haikuwepo, na nilimpenda sana huyu mwanadada shida imekujaa baada ya kuingia kwenye ndoa. Ninafanya kila mbinu ya kumpenda huyu mwanae nimeshindwa kabsa. Nafsi yangu nailazimisha but ndiyo hivyo imegoma.
It's to be free niutue huu mzigo Sasa.
 
Siyo wote wanakua hivyo
 
Njemba inainjoi kuwa Baba wawili.
Haijali lolote ipo tu yani inainjoi life.
 
Kanuni ya single mother ni kumtundika mimba na kumuongezea mtoto.

Halafu unakula nduki, akikuuliza unamwambia mbona yule wa kwanza hakukuoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…