Najuta kupoteza muda wangu kuangalia Ujinga uliopo Kwenye series ya money heist

Mkuu Chige ,tuko pamoja kwenye taste ya series.
 

wewe wazo lako kama langu, traveller walishindwana kwenye mikataba, ila me nasema PRISON BREAK NOMA SANA
 
Mimi nilimwelewa sana Berlin alivyokuwa smart kwenye kazi yake kuanzia episode ya kwanza.
"First thing, good evening! I start by offering apologize, this is not a good way to end the weekend, but you are here as the hostages. Follow the instruction, then you wil be safe" Sasa anavyoongea hadi unasema kama ujambazi ni taaluma basi huyu kasomea kweli. Mimi binafsi Berlin alivyokufa na mimi nikaacha kuangalia kwa umakini, nikarusha rusha tu.
 
Nilichogundua hapa tatizo lako ni moja tu, mkurugenzi...hujui kingereza,[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hivyo ukikutana na series ambayo scene nyingi ni drama kuliko action lazima upagawe utaona sio tamu kabisa.
 
Mbona hata PB mna i overrate sana ile kitu ya kawaida mno
 
Vikings
Billions
Nimeongezea hapo
 
Nilichogundua hapa tatizo lako ni moja tu, mkurugenzi...hujui kingereza,[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hivyo ukikutana na series ambayo scene nyingi ni drama kuliko action lazima upagawe utaona sio tamu kabisa.
Traveller, prison break na 24 wametumia lugha gani?
Au walikuwa wanaongea kisukuma?
 
Asante mkuu Kwa kunijuza nitajitahid kuzitafuta hizo movie ni muda mrefu Sana huwa nachek single movie tu.
 
Mkuu Laskaboza, kwamba Money Heist ina scenes nyingi za hovyo nakubaliana na wewe!!

Ukijiuliza lile swali la msingi katika utengenezaji filamu kwamba "hivi hii scene ingekuwa ni kwenye real world, ningefanya kama alivyoona Mwandishi?" Ukijiuliza hilo swali, utakuta Money Heist ina scenes nyingi ambazo hazi-make sense in a real world.

Kinyume chake, hiyo scene uliyoitolea mfano, kajaribu kuiangalia tena na utaona ina-make sense! Unfortunately sikumbuki ilikuwa episode ipi lakini naikumbuka ile scene!

Mosi, Tokyo hakutokea eneo la tukio kama Tokyo basi alikuwa ameji-impersonate as a Police Officer in a police uniform huku kichwa chote kikiwa kimefunikwa na bike protective gear.

Na wakati anaingia eneo la tukio, team mzima ya mapolisi ilikuwa ndani ya hema lakini polisi mmoja aliyekuwa nje, akawa amem-suspect Tokyo lakini hakuwa na uhakika kwa sababu alikuwa kichwa chote kipo kwenye protective gear!

Afande alipoanza kum-suspect Tokyo, akajaribu kutaka kumsimamisha... Tokyo akaona isiwe taabu, akakanyaga mafuta! Baada ya kukanyaga mafuta, ndipo yule afande akapata uhakika kwamba "huyu ni intruder" lakini nae wala hakufahamu kwamba ni Tokyo kwa sababu wakati anapiga radio call, alisema "...another unauthorized vehicle is entering the perimiter" wakati ile ilikuwa ni "no-pass zone" for unathorized vehicles.

Na kama ujuavyo mambo ya kijeshi... you can't just shoot kwa kitu usichokifahamu bila order ya kufanya hivyo! Lucky for Tokyo, hadi Snipers wanapata "a shoot order" ilishakuwa kind of too late (though it's within seconds) coz' tayari Tokyo alikuwa close to gate!

Na mbali ya Sniper Team, pale chini kulikuwa na team nyingine wakisubiri order! A moment wanapewa order kwamba " a target is in your range" hapo hapo wakaanza ku-shoot toward a high speeding bike!

Lakini sekunde chache baadae, wakajikuta wanashambuliwa kutoka nyuma na Tokyo's Team ambao walikuwa wameshafungua gate na kuwafyatulia risasi jamaa kama namna ya ku-divert attention yao, na walifanikiwa kwa sababu wakalazimika kugeuka kutupiana risasi na wale waliokuwa ndani wakiwashambulia wao!!

Na ukiangalia hata yule Team Leader wakati anatoa order to shoot, nae wala hakuwa na uhakika kwamba ni Tokyo... it's just a military intuition kwamba atakuwa " a daughter's mother"!

So, kwangu ile scene naona kama ina hitilafu, basi itilafu zake ni za kifilamu zaidi kuliko illogical errors!
 

Mkuu naheshimu maoni yako lakini nataka nipingane na wewe kidogo
Hizo scene umetolea mfano hembu ziangalie tena kwa utulivu utaona zina make sense
Hadi Tokyo anaingia ndani hakuna mtu alikua anahakika yule ni nani, na kumbuka polisi wote pale attention yao ilikua ndani na sio nje
Kumbuka pia Tokyo aliingia pale akiwa na uniform za polisi na helmet so hakuna mtu alimtambua zaidi ya yule askari aliye suspect kuna polisi kaingia bila utaratibu......so order ya kushoot ilikuja too late wakati lango linafunguliwa

Kuhusu kutoroshwa kwa Requel bado sijaona makosa makubwa kulinganisha na stori za kisinema sinema

Kitu pekee nakubaliana na wewe ni kwamba kuna kitu kina miss ukilinganisha na series za hollywood
Series za Hollywood zimetuharibu mind set zetu
Inakua ni vigumu sana kuanza kuangalia movie au series za kutoka nje ya Hollywood na ukazielewa bila kutoa kasoro

But all in all series ipo poa sana inaangalika
 
"Banshee" hii series sijui watu hawaijui au ila ni series tamu balaa......ni among ya my favourite series.Ingawa sikupenda jinsi ilivyoisha.
 
Bora niendelee kuiangalia The walking died wanapambana hasa but not money heisty ovyo poor poor poor poor
 
"Banshee" hii series sijui watu hawaijui au ila ni series tamu balaa......ni among ya my favourite series.Ingawa sikupenda jinsi ilivyoisha.
Hata me naona banshee Ni moja Kati ya series yangu Bora kabisa sijui kwanini watu hawaizungumzii?au watu wengi hawajaiona? Pia Kuna into the Badlands nayo Ni nzuri ebu naomba unitajie series inafanana na banshee
 
Chukua pepsi big hapo ntakuja kulipia
 
Duh, kazi ipo.

Umeeleza vizuri. Nisingependa tuhadithiane Movie humu ndani lakini anyway, acha nijikumbushie enzi zangu pale Kijenge Juu wakati nimewakusanya watoto wa majirani na story zangu za Tai Chi..Lol

Here we go ...

Kwanza Suala la Tokyo kuwaza kurudi Bank anayojua imezungukwa na mapolisi wenye silaha kali ni kitu cha ajabu sana. Sijui waliwaza nini kuipenyeza hii scene. Kama walitaka Tokyo abaki kule ndani bora wangeipotezea tu ile idea ya Berlin kumsukuma Tokyo nje. Japo najua walifanya hivyo ili kuivuta episode iwe ndefu, lakini idea yao ya kumrudisha tokyo ndani imekosa uhalisia fulani.

Mbili, Tokyo alivyofika maeneo ya ile Bank na ile pikipiki aliongea na Rio kwenye simu lakini hakumwambia kuwa anampango wa kurudi kule Bank. Alifanya kama anamuaga tu Rio. Lakini Rio akajiongeza kuwa Tokyo anampango wa kurudi Bank, kitu ambacho kina utata kidgo maana mazungumzo hayakuendana kabisa na suala la yeye kurudi kule Bank. Actually sio rahisi kuwaza kitu kama hicho kama huja.trace hata location ya simu uliyopigiwa. Kumbuka Rio alitoa taarifa kwa wenzake kuwa tokyo anarudi Bank bila hata kumuona Tokyo anashambuliwa na ma polisi kule Nje.

Tatu, mnasema order ya shoot ilichelewa kutolewa. Sio kweli. Tokyo alivyoanza tu kukimbia na pikipiki taarifa ikatolewa saa hiyo hiyo na shooting zikaanza. Snipers walikua kama wa 4 hivi na wakashindwa kumlenga muendesha pikipiki mmoja anayenyooka na barabara kuelekea kwenye lango la bank, achilia mbali shooting za mapolisi wengine. Kitu kingine cha kushangaza tokyo aliwapita mpka baadhi ya policia waliokua kwenye ground pembezoni mwa zile njia za kwenda bank and yet, they failed to do anything na order ilishatolewa. Keep in mind all this happening kabla kina Rio hawajafungua mlango wa Bank na kuanza kum.cover tokyo.

So to cut the story short. Mambo mawili niliona hayana uhalisia.

Moja, wazo la Jambazi wa Bank (Tokyo) aliyeponea chupuchupu kuwekwa jela, kuamua kurudi kwenye bank iliyozungukwa na mapolisi. Hakuna mhalifu anaweza kufanya jambo la kipuuzi kama hili.

Mbili, eneo lililozungukwa na polisi wengi wenye silaha za moto mpaka na snipers zaidi ya mmoja, na kushindwa kumlenga Jambazi (Tokyo) anayekimbia na pikipiki eneo la wazi kabisa. Halafu cha ajabu walifanikiwa kumshoot moscow aliyekua kule juu mbali karibu na mlango wa bank tena akiwa amezungukwa na zile nguzo za bank. This is a Joke!


Nime share link (youtube) ya tukio zima lilivyokua. So watch it ni tukio la dk 2:45 so it won't cost much of your Data.

 
Kwangu Hom land bado ipo
Poa
 
Huu mjadala hatuwezi fikia muafaka as long as haya ni maoni na mitatzamo yetu tofauti
ITOSHE TU KUSE NAHESHIMU MAWAZO NA MAONI YAKO MKUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…