hili uwe na uhakika na report yako lazima ufanye uchunguzi WA kina na ndio maana jamaa akaiangalia zaid ya episode 2,uwez toa. maoni kwa kuona episode 1,je ikibadilika mbele,kwaiyo jamaa yuko sahii kuona zaid ya hizo episode hili ajilidhishe
Kama ndivyo, how come tena anadai miaka mingi imepita bila kujichosha akili yake kwa kuangalia UJINGA wa kile kinachoitwa series?! Alijuaje kwamba series za takribani miaka 10 iliyopita zilikuwa ujinga mtupu wakati alikuwa haziangalii?!
That's one but again, unatoa wapi appetite ya kuangalia episodes 31 ambazo ni upumbavu mtupu?! Huna kazi zingine za kufanya?! Au unaamua kupoteza muda ili ufanye kile alichoamini ni analysis?!
Tunaposoma uandishi wa script tunafundiswa kwamba, the first 10 pages of your scripts are of essence coz' ndizo zita-determine kama Reviewer aendelee kuisoma script yako au aitupe kapuni!!
Kwanini tunaambiwa hivyo?! Kwa sababu there's no way mtu anaweza kusoma 45-120 pages script wakati ni boring script! Kwa maana nyingine, no one will watch the whole episode or the whole feature film wakati ni upumbavu mtupu!
Lakini wakati anataka kuonesha kwamba ni "series za siku hizi" kwa upande mwingine anaonesha sio mtu wa series at all unless kama maelezo yake siyo ya kweli!
Ninachokiona toka kwake ni ile hali ya Wabongo wengi series zao za kwanza kuwa ni Prison Break na 24, na matokeo yake inakuwa ni kama ile simulizi ya Kipofu Kaona Mwezi! Kwao hakuna best series kama PB na 24 !!
Kingine ninachokiona kwa jamaa kuanza kuangalia wakati tayari alishakuwa na perception yake kichwani kwamba PB, 24 na Traveler ndo kila kitu, na series za siku hizi ni upumbavu mtupu!!!
Ni kutokana na hilo, ndo maana mapema tu akatarajia watu wafanye tukio na kusepa zao bila kufahamu jamaa hawakuingia benki ambako tayari kuna noti bali waliingia sehemu ambayo walitakiwa kuchapisha noti!!!
Ameshindwa kuona ni namna gani Stockholm syndrome si kitu cha ajabu kwenye situation kama zile! Fanya homework upate mkasa wa Norrmalmstorg Robbery, jijini Stockholm, mkasa ambao ndio ulizaa the so-called Stockholm syndrome!
Binafsi Money Heist sio my top series,na haipo hata kwenye my Top Ten; na nimeshawahi kuandika humu ni namna gani huwezi kumlinganisha Michael Scofield na Professor coz' Michael is far smarter compared to Professor!
But seriously mtu aliyeangalia Money Heist critically anaweza kusema badala ya kufanya mishe za kuondoka ndo kwanza kunatokea "...
mishe za kitoto za professor za kumtongoza inspector." Like serious?! Hivi aliangalia na kuelewa mazingira yaliyomkutanisha Professor na Inspector Raquel?!
Kukosoa kwamba eti movie haioneshi walitoka vp Spain hadi Caribbean inaonesha wazi hana ufahamu wa mambo ya filamu! Ni filamu za wapi hizo zinaonesha kila kitu?!
Kanuni moja wapo ya uandishi wa script ni kwamba, "write a scene that will push a story forward"!
Kuandika scene ikionesha wanaondoka Spain to Caribbean ingekuwa ni wastage of resources coz scene kama hiyo could never push the story forward unless ndani yake waingize additional twisting!
Kinyume chake, angalia scene iliyowakutanisha Professor na Raquel ilivyoweza ku-push story forward lakini yeye ndo kwanza anaponda!!
Unachambua halafu unashangaa mambo ya mapenzi... are you guys serious?! Hivi mmeona ni namna gani mambo ya mapenzi yalivyoweza ku-push story forward?! Kwanza aliyeangalia vizuri atagundua unlike PB ambayo characters walikutana gerezani, Money Heist walikutana uraiani na wakatumia siku kadhaa kupanga mipango!
Ingawaje Prof alikuwa against mahusiano among the Team Members lakini jambo hilo halikuwezekana kwa sababu there's no way unaweza kuweka watu wazima pamoja halafu wasianzishe mahusiano!!
Lakini kile kile ambacho Professor kilimfanye apinge mahusiano, ndivyo ambavyo mahusiano ya Tokyo na Rio yalivyoleta tafurani zilizoweza kufanya story iende mbele! Ni baada ya Tokyo kumwacha Rio kule batani, siku zilizofuata Rio recklessly akampigia simu Tokyo na hivyo kusababisha kuwa tracked!
Akawa tracked na kukamatwa, jambo ambalo lilizaa a new heist ambayo ililenga kwenda kumwokoa Rio!
Ni mapenzi ndiyo yalileta yote hayo!
Ni mapenzi ya Professor kwa Raquel ndiyo yalimfanya Professor apoteze dira baada ya kuhisi Raquel ameuawa!!! Ni mapenzi ya mama kwa mwana ndiyo pia yalisababisha Nairobi kupigwa risasi na kuleta tafurani kundini! Bogota's strong feelings kwa Nairobi ndizo zilimfanya hatimae aondoke kwenye reli na kutumia muda mwingi kumuhudumia Nairobi!
Mleta mada anaisifia PB... anasahau ni mapenzi ya Sarah kwa Michael ndiyo yaliwezesha Michael kutoroka! Ni mapenzi ya Warden Pope kwa mke wake ndiyo yalimpa access Michael ofisi ya Warden!! Ni mapenzi ya Sucre kwa Maricruz ndiyo yalimfanya Sucre ajiunge na mpango wa prison breaking!! Ni mapenzi ya T-Bag kwa Suzan Hollander ndiyo yalithibitisha hakuna mkate mgumu kwenye chai manake na ujanja wake wote ule, kwa mara ya kwanza tukamshuhudia T-Bag analia!!!
Mifano kama hiyo pia ipo mingi hata kwenye 24!
Hapa itoshe tu kusema kwamba, kwenye uandishi kuna kitu kinaitwa kutengeneza conflicts! Mapenzi ni moja ya vyanzo vikuu vya conflicts kwenye literature coz yanafanya watu wawe stupid and reckless! Haya yalimkuta hadi Mmatumbi mwenzetu, Ngoswe!
Hali ya watu kuwa idiot ndiyo inazaa mikasa na twisting nyingi kwenye uandishi! Lau kama Money Heist isingekuwa na zile vurugu za mapenzi basi kuna hatari story ingekuwa flat, na hatimae kuwa totally boring!!