Najuta kutembea na binti wa kirangi

Najuta kutembea na binti wa kirangi

Wakuu siandiki thread hii Kwa lengo la kukashifu au kutweza mtu au kabila la mtu.

Iko hivi
Miaka 10 au zaidi kidogo iliyopita nilijikuta kwenye huba zito na binti mmoja pale Arusha mjini.
Bint huyu alikuwa mzaliwa wa Arusha lakin wazazi wote wawili ni warangi.
Kwa sababu za hapa na pale mahusiano yetu yaliisha rasmi mwaka 2015 .

Ajabu ni kuwa bint huyu aliolewa miaka hiyo hiyo ya 2015 ila kila mara akipata changamoto basi mama yake anamwambia mwanaye kwamba ameenda Kwa mganga kaambiwa mwanae karogwa na Mimi.

Hii imekuwa kero kubwa Sana kwanga na suala hili linanifedhehesha Sana.

Je naweza kuchukua hatua gani kukomesha tabia hii?
Acha Kumloga binti wa watu
 
Badala ya kujua namna ya kutatua changamoto zao wao wana kimbilia kwa mganga. Kazi ipo.
 
wazee wa juju shrine.. haya sasa X kishakukamata kwenye Tv asilia.. hebu rudi kilingeni mshirika tujue tunafanyaje!!
 
Kifuatacho aitivii ni hao warangi kuanza kukurushia makombora kupitia waganga wao...
 
Nilikua nasikiliza mahubiri jana,yanasema "kila dhambi unayoifanya lazima iache alama kwenye maisha yako"sasa hapa nawaza tu sijui kuna ukweli...
 
Waganga wa ovyo,,,tena kwa sasa wamejaa hawa wa majini,,bora kidogo wa mizimu sema kwa sasa ni wachache sana,,,,waganga wa majini wepesi sana,,hao kazi ikiwa ngumu atapindisha mambo ila hawez akasema hawezi,,,akute aliekuroga kamzidi nguvu atapindisha, akute aliekuroga ni mwanachama mwenzie kwenye mambo yao atapindisha,,...shida inakuja tena kama kazidiwa utaalam na mwenzie( kuna wachawi wanatumia vivuli vya watu wengine kuroga ili wasionekane, sasa kama huyo mganga sio mtaalam atakua anaona tu watu wasio husika ila mhusika hamuoni na hio ishu yako inaweza ikawa imedondokea hapa, inawezekana mchawi anatokea humohumo kwenye familia yao ila kwakua anakufaham basi anatumia kivuli chako kufanyia mambo yake, sasa hao wakienda kwa wataalam wao wanakuona wewe)
 
Wakuu siandiki thread hii Kwa lengo la kukashifu au kutweza mtu au kabila la mtu.

Iko hivi
Miaka 10 au zaidi kidogo iliyopita nilijikuta kwenye huba zito na binti mmoja pale Arusha mjini.
Bint huyu alikuwa mzaliwa wa Arusha lakin wazazi wote wawili ni warangi.
Kwa sababu za hapa na pale mahusiano yetu yaliisha rasmi mwaka 2015 .

Ajabu ni kuwa bint huyu aliolewa miaka hiyo hiyo ya 2015 ila kila mara akipata changamoto basi mama yake anamwambia mwanaye kwamba ameenda Kwa mganga kaambiwa mwanae karogwa na Mimi.

Hii imekuwa kero kubwa Sana kwanga na suala hili linanifedhehesha Sana.

Je naweza kuchukua hatua gani kukomesha tabia hii?
Wacha uwoga mkuu wee endelea na mambo yako ya Maisha.

Wanataka kukutoa kwenye mstari na ukiingia kingi tu asee Mzee wangu umepotea.
 
Sipo Arusha Kwa zaidi ya miaka 8 sasa.

Mimi ni wale wasio amin ushirikina na Imani yangu hainiruhusu kupiga ramli
Hupo Arusha, mwanamke ulishaachana naye, umejuaje kuwa mama yake huwa anasema hivyo? Umejuaje kuwa wanakwenda kwa waganga? napeta kero gani wakati uko mbali na tena ni muda mrefu?
 
Back
Top Bottom