Najuta kutokununua Bitcoin/Binance 2017/2018, uwezo nilikuwa nao ama kweli bahati haiji mara mbili

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
9,205
Reaction score
22,219
GT
HIi ndo ilkuwa nafasi yangu pekee yakuwa billionea hapa mjini. Nakumbuka nikiwa na rafiki.yangu tulikuwa kila siku tunsoma na kufuatilia graph za crypto na uwezo wa kununua tulikuwa nao.

Nakumbuka pamoja na price fluctuations lakini BTC ilikuwa ina range between $3200 mpaka $3800 kipindi hicho. Miaka hiyo hiyo Binance ilkuwa $10 leo inasoma $600 imepanda zaidi ya mara 60

Jamaa.yangu yeye alinunua kadhaa Bitcoin, ethu..xrp na stellar lakini baadae akamuuzia jamaa wa Ghana mwaka huohuo Daaaa anajuta sana saivi. Kama kuna promising coin mpya tujuzane wadau niwahi nisichelewe tena.

Huwezi amini leo hii Bitcoin inasoma $95000 zaidi ya mara 25 kutoka price ya mwaka 2017/2018 Hata kama ningenunua Btc au Binace za $ 500 leo hii ningekuwa naitwa freemason..

Jamani fursa zinapotokea tusilaze ubongo kwa Simba na Yanga kwa sasa bitcoin haikamatiki japo unaweza nunua you never know may be itakuja kuuzwa $5M in next 10/20 years bado hatujachelewa..

IMG-20250430-WA0076.jpg

IMG-20250430-WA0075.jpg

IMG-20250430-WA0074.jpg
 
Shida ni Je unaweza kusubir kwamuda huo wote
 
Bongo zozo anapigia kelele sana hili jambo.
Wengi tumechelewa ila bado nafsi ipo
 
GT
HIi ndo ilkuwa nafasi yangu pekee yakuwa billionea hapa mjini. Nakumbuka nikiwa na rafiki.yangu tulikuwa kila siku tunsoma na kufuatilia graph za crypto na uwezo wa kununua tulikuwa nao.

Nakumbuka pamoja na price fluctuations lakini BTC ilikuwa ina range between $3200 mpaka $3800 kipindi hicho. Miaka hiyo hiyo Binance ilkuwa $10 leo inasoma $600 imepanda zaidi ya mara 60

Jamaa.yangu yeye alinunua kadhaa Bitcoin, ethu..xrp na stellar lakini baadae akamuuzia jamaa wa Ghana mwaka huohuo Daaaa anajuta sana saivi. Kama kuna promising coin mpya tujuzane wadau niwahi nisichelewe tena.

Huwezi amini leo hii Bitcoin inasoma $95000 zaidi ya mara 25 kutoka price ya mwaka 2017/2018 Hata kama ningenunua Btc au Binace za $ 500 leo hii ningekuwa naitwa freemason..

Jamani fursa zinapotokea tusilaze ubongo kwa Simba na Yanga kwa sasa bitcoin haikamatiki japo unaweza nunua you never know may be itakuja kuuzwa $5M in next 10/20 years bado hatujachelewa..

View attachment 3321050

View attachment 3321051

View attachment 3321052
Nunua XRP na XLM kwa kadiri uwezavyo hata kukopa ikibidi kakope then hold utamshukuru Mungu baadae.
Kwa kifupi sana XRP na XLM zinaenda kuwa uti wa mgongo wa global digital curreny na wala usizani itachukua miaka mingi ni ndani ya muda mfupi sana leo XRP ni USD 2.22 na XLM ni USD 0.27 yaani bado kabisaaaaaaa zinauzwa kwa bei sawa na bureeeee na hivyo unaweza nunua kadiri utakavyo.
Ila jambo moja nikukumbushe unapowekeza uwe tayari pia kukubali Mungu atumie sehemu ya utajiri utakaoupata.
 
Kwa nini XRP XLM?
 
Nunua sasa usubiri miaka 10 itakuwa 1 milioni.

Hakuna tofauti ni Bitcoin ile ile na pesa kama unayo ni vile vile hujachelewa.
 
Angalia usife kwa depression mkuu, kuna sababu ni kwanini hukununua, na wala usidharau hizo sababu maana ni za msingi sana sema unazipuuza eti kwa kuwa 1btc sasa ni usd 100k
 
Majuto hayatakusaidia chochote, kila mwanadamu ana kipindi ambacho kama angerudi kurekebisha leo hii angekuwa tajiri. Wewe ni 2017 kwenye BTC, mwengine kwenye ardhi, mwengine kilimo mwengine mgodini yote kwa yote ndo maisha ya binadamu. Cha msingi tukio hilo litumie kama funzo - jifunze Kisha rekebisha ili ipatapokuja fursa nyengine usifanye makosa kama uliyofanya wakati huo. Dunia haimtambui mtu mwenye majuto.
 
We unaonekana ulitaka kufanikiwa kipindi kile kile yani ulale maskini uamke tajiri
 
Back
Top Bottom