Kipindi nnanunua eneo la kujenga mzee aliandika jina lake baada ya langu
Siku naenda kufata ile hati ya mauziano nakuta jina lake...nkasema tu ah mzee aje au alisahau ...anyway nkapotezea zangu
Ila sasahiv naelewa Na pengine service zote nkatumia majina yake...
Unapotaka kuowa mkuu make sure una kitu mkononi na unajiweza kidogo kiuchumi
Kitu pekee nnachoweza kukuambia mkuu ni hiki
Asikudanganye mtu eti kuna mwanamke atakupenda wewe et umekaa tu ndani
Fedha ndio hasa heshima ya mwanaume
Tafuta fedha jijenge mwenyewe
Wale wanawake wakusema tuowane tutajenga pamoja
Wa mwisho kufanya hivyo alikua ni mama yako pekee
Hawa wengine wanataka uwe na kitu