Najuta nimezaa nje ya ndoa, ushauri wako muhimu sana


Umeshawahi kuimagine mkeo amebeba mimba ya mtu mwingine?umeshawahi kuimagine uko hospitali mkeo anajifungua ukijua mtoto sio wako?umeshawahi kuimagine mtoto anakuita baba ilihali ukijua sio mtoto wako.hii ni ndoa kaka kwa ubabe haujengi na hapa sio swal la mwanamke kumtisha huyu mtoa mada ,he messed up na anataka ku undo his mistakes,sidhani kama kumjaza kicwha na kiburi kutasaidia kuiokoa ndoa yake na pengine hujui tu wanawake tuna kawaida ya kusema its okey while its not na kusema its not ok while its ok sasa kuwa mwangalifu sana na mkeo kama unae anaweza akawa anakupa go ahead ya kuleta watoto kila uchao lakini believe me hujui ana heal out maumivu yake vipi,nakwambia haya kwa uhakika kabisa!IT TAKES A WOMAN TO UNDERSTAND A WOMAN!
 
mmmh? Pole mkuu, jipange mwambie wife wako.
Mimi kuanzia leo nikienda bush nitafungasha condoms.
Hii inaleta msongo wa mawazo aisee!
 
paulss lazima apate +ve comments sababu kajua kosa lake na kakiri, yule mwingine ni kama alikuja kujisifia jinsi alivyokuwa kidume.
hapa ushauri wangu kwake ni kufanya kama alivyofanya hapa kwa mkewe. kama kweli anampenda huyo mke ni bora amwambie mwenyewe kuliko aje kusikia toka nje. maana hali inakoenda ni lazima yatafika tu nyumbani, itakuwa mbaya sana mkeo akisikia toka kwa mwingine.
Ongea taratibu tu na mkeo, atakuelewa, atakusamehe na atakupa solution kuhusu malezi ya hao watoto, believe me.
 
Last edited by a moderator:
Duh...! Najaribu kujiuliza kama ile familia ya kijijini kwenu sasa ni familia ya nani..., ambayo nayo sasa haina amani wala furaha unayojaribu kuitunza kwa familia ya mjini....! Kwa mtazamo wangu fupi, naona njia zifuatazo zinawezekana....!
  1. Kuuweka familia ya kijijini huru kwa kuanika ukweli wote....!
  2. Kuamua kubeba laana kwa kuitelekeza familia hiyo mazima....!
  3. Kujinyonga ili mjadala uishe....!
  4. Kwenda mwenyewe gerazani tayari kwa kifungo....!
 
Unacheza karate nini? Nikikuona nitimue mbio

Ndahani mbona wanitenda hivyo mwana wa mwenzio..........

Let me fafanua basi wanawake siku hizi wanakazi nzuri, wanamikwanja kwa sana, so kumtisha eti atakosa pa kwenda au atashindwa maisha ni kujidanganya hapo cha muhimu ni huyo mwanamke kukubali matokeo tu MWANAUME WA PEKE YAKO UTAMTOA WAPI SIKU HIZI???
 
Reactions: ram
I love u Kongosho, mpe Paulss, mwisho wa siku watoto wanakuwa wa mataani na baba yao yupo kabisa tena ana uwezo, jamani Paulss hebu funguka kwa mkeo na uwatunze watoto wako, mweeh!

 
Wapi Bishanga bhana, nilikumisi kimouma

 
DUH!!!
Pole sana but ni vizuri wife ajue,,,,,,,,sasa jinsi ya kumwambia na effects zake ndo mh!!!!

may be,,, nunua namba nyingine utume sms kwako(ujidai ndo huyo binti) ambayo unajua mkeo ataiona kama hamyimani cm. mfano (nimekutana na rafiki yako ndo kanipa namba yako, nina mtoto au watoto wako kutokana na tendo tulilofanyaga ulipokua huku, naomba unipigie tafadhali tuongee),,,,alaf cku hiyo unakua na huzuni kwa mkeo mpaka bas na kukuna kichwa, huli chakula vitu ka hivyo,,,,,,hata akiiona anajua kuwa unajutia na atakufariji ingawa atakulalamikia
 
Lete watoto nyumbani kwa wazazi wako. Ulidhamiria uharibifu sioni kwa nini uogope. Hao mapacha wanaweza wakawa na maisha mazuri, ukiwatelekeza watakufanya kama Kanumba na Diamond.

Huwezi jenga moja kwa kubomoa nyingine, hiari yako kujenga zote au kubomoa zote.
 
Word!!!!

Mtoto wa kumkuta na mtoto wa kuletewa ni vitu viwili tofauti kabisaaaa!

Na mawazo ya humu achanganye na akili zake....maana asijechukua ushauri kumbe wanaomshauri kwa sasa wanaishi na mke wa saba; wao kuoa na ku divorce si issue (naongelea wale ambao dini hairuhusu na wanafanya).



 
Nayo kweli itakuweka huru, nawe utakuwa huru kweli kweli. Funguka kwa mkeo, mwambie ukweli ya kilichotokea, atakasirika, itamuuma lakini ndo ukweli wenyewe na kama ni muelewa basi atakuelewa. Akishakuelewa chukua watoto wako uwalee kwa mapenzi yote, kama unayowapa hao watoto wa mkeo.

Kuna mchangiaji mmoja amekuuliza ikitokea yule mdada akafa, unadhani hao watoto utawatunzaje tena, manake hiyo laki unamtumia huyo mdada, akifa? Usifanye watoto wakakua katika mazingira magumu wakati uwezo wa kuwatunza na kuwalea unao, plz, ongea na mkeo, tunakuwaga wakali but naamini atakuelewa. All da best
 
Yaaani, roho inaniuma utafikiri mie ndio huyo dada niliyezalishwa..nway, Nakupongeza kwa kuonesha moyo wa kuwajali hao viumbe na nakupa pole kwa kuitia dosari ndoa yako. Nakushauri uonane na familia ya huyo dada, waweke wazi kuwa tayari una mke na watoto. Jipe muda kuisoma familia yao ni watu wa namna gani huku ukiendelea kuhudumia hao malaika. Kama ni watu wakorofi inabidi uendelee nao kisiri siri na umjengee huyo mama mazingira mazuri ya kujitegemea. Mkeo anapaswa kufahamu hili ila zingatia mambo mawili kabla ya kumfahamisha. Kwanza, maamuzi atakayochukua (akusamehe aendelee na ndoa au adai talaka), pili zingatia familia ya yule binti. Iwapo familia ya yule binti sio watata na ikatokea umemwambia mkeo ila akadai talaka inamaana hapo uwe tayari kuendelea na huyo binti kama mke na mume. Kama familia yao ni watata na unaona huwezi kucope na huyo binti nakushauri usimwambie mkeo hadi hapo watoto watakapokuwa wakubwa. Ila unahitaji kuwa smart katika huu mchezo.
 
duu,huu uzi kweli nimechelewa.mfikirie na huyo aliebeba uja uzito.unampotezea muda wake,na wafikirie hao watoto,baba ni yule muwajibikaji wa vitendo juu,sio kutuma hela tuu.be honest kwa mke wako,muanzie kwa mbali,kuliko kuiendeleza kuwa siri.no one is perfect,ila tunapokesea ni vizuri kujaribu kuparekebisha
 
1. Ulimdanganya binti kwamba hujaoa ukampa jina la uongo
2. mlipoona ukaendelea kumdanga na wakati huo unajua kabisa una familia
3. ili kuficha uongo wako ukaanza kumwaga mijihela, maana kijijini kumkabidhi binti laki 3 ni hela nyingi kidogo
4. ukaenda kusajili line kwa jina lile la uongo ili uendelee kumdanganya na hele ua matumizi unatuma kila mwezi!!!

kama huko kijijini maisha yao ni choka mbaya huoni wazazi wanakuwa wakali ili umchukue huyo binti kwasababu hawajui kama una mke? na huyo binti ni wakijiji chenu au cha jirani? maana ninavyojua watu vijijini wanafahamiana sana, kweli binti akuelezee jinsi ulivyo washindwe kutambua ni mtoto wa fulani kweli na ivi unasema watoto wanafana!?

fanya hima uweke mambo hadhari mwenyewe maana huyo mkeo akisia ndo umeharibu kabisa

afu kama wewe ni ngosha kweli unanifanya niconclude reseach yangu ninayowafanyia kina ngosha, "when it comes to inf ni waongo sana aisee"
 
Wakati unafanya uzinzi ulituomba ushauri nenda kamuombe mke wako atakusaidia kwa hili

Kuwa muungwana tia zipo domo lako. Si lazima uchangie kama huna ushauri wa maana. Mwenzio ana matatizo ndio maana kaamua kuanika ukweli wake ili asaidiwe. Makosa tunayafanya sote. Si vema kuhukumiana.
 
Wakati unafanya uzinzi ulituomba ushauri nenda kamuombe mke wako atakusaidia kwa hili

Kuwa muungwana, tia zipu domo lako. Si lazima uchangie kama huna ushauri wa maana. Mwenzio ana matatizo ndio maana kaamua kuanika ukweli wake ili asaidiwe. Makosa tunayafanya sote. Si vema kuhukumiana.
 
kiongozi mi sina ushauri!nikupongeze tu kwa kutoa mapacha!hivi kutoa mapacha ni kipaji,karama,maarifa au bahati?
 
Teh teh teh...mimi najipigia debe ntakuwa wa mwanamke mmoja tu. Unajua ulitema cheche mpaka nikasema kuna mtu anapigwa karate hapa akileta za kuleta...anyway ni kweli wanawake wako empowered kama wanaume kwahiyo hakuna wa kumtishia mwenzake. Ila inakuwa poa kama hata cost sharing inapewa umuhimu.
 
Mkuu mimi sitakupa pole ila nikupongeze na ninakulaumu kwa kutokuwajibika ipasavyo!

Binafsi ninaamini kwamba hakuna aliye mkamilifu na kama ni kukosa wengi tumejikuta tunafanya kinyume na maadili zetu hivyo huna sababu ya kujutia kitendo hicho. Kimsingi uliongozwa na tamaa Mungu akabariki coz watoto siku zote ni baraka otherwise wengi wanahangaika kuwatafuta hata kwa waganga na bado ngoma haionekani.

This is what you have to do from my own opinion, be honest to yourself first. Be honest to the person you respect most after your wife, then be open to your wife infront of as many respectable people as possible.

Huwezi kuishi kwa kujificha ni hatari mno, jitokeze home kwenu wape ukweli, kama wazazi wapo mwagize shemeji aende home huko akutane nao wamuandae kisaikologia then utambulishe mada.

Ninaamini hao watoto watakuwa chanzo cha baraka kwako na familia na ninakuombea Mungu amuonyeshe njia shemeji akuelewe.

Once a man, always a man!
 
sema ukweli japokuwa unauma. Jambo hilo huwezi kulificha maisha yako yote. Kumbuka mahitaji yao yanakua kama wanavyokua wao hivyo huwezi kufanya siri muda wote wa maisha yako. Mwisho wao hawana hatia ww ndiye mwenye hatia na kadri unavyochelewa ndivyo unavyozidisha hatia yako. Chukua hatua haraka kaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…