Najuta nimezaa nje ya ndoa, ushauri wako muhimu sana

Najuta nimezaa nje ya ndoa, ushauri wako muhimu sana

'Mtoto wa nje' ndo kitu gani? I hate this neno,kwangu mtoto ni mtoto na ninao kibao na nawapenda wanangu wote na kuwatunza.
Mtoa mada sikiliza bana,huyo mkeo asikutishe na wala huna sababu y a kuogopa kihivyo. Ulichokifanya ni jambo la kawaida sana na asilimia kubwa ya wanaume tumepitia huko.La kufanya:
A) Face the girls parents. Mchukue nduguyo unayemwamini mwende kwa wazazi wake, weza kwenda na baba,mama,kaka,mjomba does'nt matter,nyie nendeni,mtalipishwa faini itakuwa imetoka hiyo.
B) Tafuta ndugu upande wa mke ambaye mkeo anamweshimu sana,mpasulie ukweli kuwa umezaa na huyo mdada,mwombe akuite wewe na mkeo na kwenye kikao yeye ndo atamke yeye na sio wewe kisha mama watoto akikuhoji jibu 'ndiyo' halafu usiongee sana,be cool,akipandisha just stay quite ila akijitia kurusha ngumi mtandike maana si ruksa akunyanyulie mkono hata kama una kosa.
Katika hili aki pack na kuondoka kamwe usimfuate,its up to her kuamua kurudi au kuacha,nakuhakikishia atarudi,hujaua mtu aslan.
Always remember waume wa kwelituko wachache sana hapa mjini na hakuna mwanamme anaachwa siku hizi.
Najua it sounds arrogant ila ukweli i am advising by drawing on my deep experience ya ku deal na mama zetu hawa.

Umeshawahi kuimagine mkeo amebeba mimba ya mtu mwingine?umeshawahi kuimagine uko hospitali mkeo anajifungua ukijua mtoto sio wako?umeshawahi kuimagine mtoto anakuita baba ilihali ukijua sio mtoto wako.hii ni ndoa kaka kwa ubabe haujengi na hapa sio swal la mwanamke kumtisha huyu mtoa mada ,he messed up na anataka ku undo his mistakes,sidhani kama kumjaza kicwha na kiburi kutasaidia kuiokoa ndoa yake na pengine hujui tu wanawake tuna kawaida ya kusema its okey while its not na kusema its not ok while its ok sasa kuwa mwangalifu sana na mkeo kama unae anaweza akawa anakupa go ahead ya kuleta watoto kila uchao lakini believe me hujui ana heal out maumivu yake vipi,nakwambia haya kwa uhakika kabisa!IT TAKES A WOMAN TO UNDERSTAND A WOMAN!
 
mmmh? Pole mkuu, jipange mwambie wife wako.
Mimi kuanzia leo nikienda bush nitafungasha condoms.
Hii inaleta msongo wa mawazo aisee!
 
i like how most of the comments kwenye hii thread are +ve as compared to ile ya aliyezaa na mke wa mtu na mtoto wa rafiki yake. wanaJF mkiamka vizuri mnakuwa +ve sana, thumbs up.
paulss umeona kosa, umekiri na unajaribu ku-correct it hongera 4 that. mwambie mkeo na hao wazazi, mwanzoni utakuwa mgumu kidogo but in the long run u'll make na mtaendelea kwa amani
paulss lazima apate +ve comments sababu kajua kosa lake na kakiri, yule mwingine ni kama alikuja kujisifia jinsi alivyokuwa kidume.
hapa ushauri wangu kwake ni kufanya kama alivyofanya hapa kwa mkewe. kama kweli anampenda huyo mke ni bora amwambie mwenyewe kuliko aje kusikia toka nje. maana hali inakoenda ni lazima yatafika tu nyumbani, itakuwa mbaya sana mkeo akisikia toka kwa mwingine.
Ongea taratibu tu na mkeo, atakuelewa, atakusamehe na atakupa solution kuhusu malezi ya hao watoto, believe me.
 
Last edited by a moderator:
Wadau wakati mwingine katika maisha tunafanya mambo ambayo ukikaa utulie unajiona mpumbavu na kutoamini kama kweli ni wewe umefanya au ulirukwa na akili.

Mkasa ulio nikuta ni matokeo ya uzembe wangu ambao naujutia hakuna mfano, so naomba ushauri wako badala ya kuendelea kunihukumu kwani tayari nimejifunza

Mwaka juzi tulienda kwenye shughuli fulani mkoani kwetu kwa wiki mbili, na katika katiza katiza za hapa na pale nikapata kabinti kamoja nikaanza nako uhusiano huku nikiwa na mke wangu na watoto wawili ambao niliwaacha Dar,
Kibaya zaidi mazingira tuliyokuwepo kondom zikawa hakuna na nikafanya kosa la mwaka kwa kujamiiana naye bila kinga.

Baada ya shughuli kwisha nikarudi Dar na kuendelea na maisha na nikawa sina tena mawasiliano na yule binti kwani alikuwa hana simu,hata hivyo ilikuwa ni kama hit and run

Sasa mwezi machi nikaenda likizo mkoa na familia, tukiwa katika wiki ya mwisho kama bahati nikakutana na yule binti akiwa na rafiki yake wote wamebeba watoto, basi yule binti kuniona tu alishtuka na kupiga kelele almanusura anguke na kuzirai, akaja akanikumbatia na kunishikilia kwanguvu huku akilia na kuongea maneno yaliyonichangaya kabisa.

Ikabidi tutafute sehemu tukae atulie kisha akamtoa mtoto mgongoni na yule wa rafiki yake akasema wanao hawa wako mapacha.
Kiukweli nilipo waona tu roho ilipasuka maana kitu fotokopi,huitaji hata mtaalamu kubaini kama wale watoto ni wangu kwani tumefanana nao mno.

Baada ya maongezi marefu nikajiridhisha kuwa watoto kweli ni wangu kwa mujibu wa maelezo yake na mfanano wa watoto.
Na akanieleza jinsi alivyohangaika kunitafuta kwani hakuwa hata anajua ninapokaa nikiwa mkoa na jina nilimpa la uongo hivyo na watoto kawapa jina hilo kama ubini wao.

Ilibidi nimpatie pesa ya matumizi kwanza palepale na nikachukua tax na kuwapeleka kwao kwa ahadi kuwa nikapajue kwao kisha kesho yake ntakwenda na wazee kujitambulisha kama mimi ni baba wa watoto wale,akanipa namba zake za simu alikuwa nayo nikazuga nita mbeep nkiweka vocha kisha nikaondoka bila kushuka na kusalimia kwao na nikamwambia asiseme kitu kwanza nijipange kwani anaishi na wazazi wake.

Niliporudi home nikajiuliza usiku kucha sikupata majibu,
Nampenda mke wangu na ananiamini sana kila nikifikiaria akijua akili haikubali, nahisi nitaharibu familia yangu
Baada ya tafakuri ya muda mrefu nikafanya maamuzi ambayo nayo naona yanaanza kunishinda ndio maana nipo hapa kwa ushauri wenu.

Nilichoamua ni kuhakikisha natunza siri hii peke yangu, nikaamua kesho yake nikanunua line mpya ya simu na kuisajili jina lile feki nikampigia simu kuwa nimepata dharura nimeondoka alfajiri na nikamtumia pesa laki3 kwaajili ya matumizi na kuahidi nitarudi soon.
Baada ya hapo nikamaliza wiki yangu mkoa nikiwa nashinda home tu hadi nilipoondoka na familia kurudi Dar.

Huu ni mwezi wa 6 sasa ninachofanya ni kila mwezi natuma laki moja ya matumizi kwa ile line na kama anataka kunitaarifu kitu labda watoto wanaumwa basi atatuma meseji na mimi kila siku jioni huwa naweka line ile kwa muda mchache na kuangalia kama kuna ujumbe au nataka kujua jambo then naitoa.

Nafanya haya yote kujaribu kuprotect familia yangu lakini pia kuhakikisha watoto wale wanapata huduma kama watoto wengine.

Siku za karibuni presure toka kwa wazazi wa yule binti imekuwa kubwa, wanataka kunijua na kubeba jukumu kama baba kweli na si kutuma tu pesa wakati hawamjui mzazi mwenza wa binti yao, wamejaribu sana kuni trace bila mafanikio maana kila nikiwasha ile line jioni nakutana na sms kali kali kuto kwa wazazi wake, wanaongea maneno makali hadi kufikia kunitisha.

Hakuna ndugu yangu anajua maana niliogopa angeweza kusababisha mimi kujulikana kitu ambacho sipo tayari kitokee kwani mke wangu akijua nahofu ya kupoteza furaha ya familia yangu

Lakini pia wakati mwingine nawafikiria wale watoto wanahitaji baba anayeoneka hata kama sita ishi nao .
Pia najiuliza ni kwa muda gani nitaweza kukaa na jambo hili peke yangu huku likinipa hofu na kuniondolea furaha ambayo ndio naogopa kuipoteza kwenye familia yangu

Wakuu naombeni mawazo yenu tafadhali, kama ni kosa limeisha fanyika lakini I feel like I can't hold it anymore, but when I think about my family I got stuck
Duh...! Najaribu kujiuliza kama ile familia ya kijijini kwenu sasa ni familia ya nani..., ambayo nayo sasa haina amani wala furaha unayojaribu kuitunza kwa familia ya mjini....! Kwa mtazamo wangu fupi, naona njia zifuatazo zinawezekana....!
  1. Kuuweka familia ya kijijini huru kwa kuanika ukweli wote....!
  2. Kuamua kubeba laana kwa kuitelekeza familia hiyo mazima....!
  3. Kujinyonga ili mjadala uishe....!
  4. Kwenda mwenyewe gerazani tayari kwa kifungo....!
 
Unacheza karate nini? Nikikuona nitimue mbio

Ndahani mbona wanitenda hivyo mwana wa mwenzio..........

Let me fafanua basi wanawake siku hizi wanakazi nzuri, wanamikwanja kwa sana, so kumtisha eti atakosa pa kwenda au atashindwa maisha ni kujidanganya hapo cha muhimu ni huyo mwanamke kukubali matokeo tu MWANAUME WA PEKE YAKO UTAMTOA WAPI SIKU HIZI???
 
  • Thanks
Reactions: ram
I love u Kongosho, mpe Paulss, mwisho wa siku watoto wanakuwa wa mataani na baba yao yupo kabisa tena ana uwezo, jamani Paulss hebu funguka kwa mkeo na uwatunze watoto wako, mweeh!

Paulss, unajali hisia za mke wako, ni kweli ni vizuri kujali hisia za mke.

Je hisia za watoto? Achia mbali haki yao ya kumwona baba??

Je huyo mwanamke mwingine, ana jiwe kifuani?? Unadhani hana hisia kabisa sababu tu si mke?? Zingatia kuwa watoto wanafanya mahusiano yasipotee.

Hapa suala la hisia sioni kama ni priority tena maana mambo yashaharibika.

Hapa ni kufanya 'the right thing kwa kutumia right ways'

kumwambia mkeo haiepukiki, ya nini watoto wakutane siku ya msiba wa mzazi wawe rivals kwenye mali??

Siombei hili, imagine linatokea balaa kwa watoto wako utalia kimya kimya? Utaenda waliko kuonesha msibani??
Na ukienda msibani what for?? Unamkubali akiwa si hai wakati ulimkataa akiwa hai??

Sema mapema, tena sana na ikibidi baada ya muda mrefu watoto hao wawe wanakuja kwako ili wasionane kama maadui bali watu wa familia moja.
 
Wapi Bishanga bhana, nilikumisi kimouma

'Mtoto wa nje' ndo kitu gani? I hate this neno,kwangu mtoto ni mtoto na ninao kibao na nawapenda wanangu wote na kuwatunza.
Mtoa mada sikiliza bana,huyo mkeo asikutishe na wala huna sababu y a kuogopa kihivyo. Ulichokifanya ni jambo la kawaida sana na asilimia kubwa ya wanaume tumepitia huko.La kufanya:
A) Face the girls parents. Mchukue nduguyo unayemwamini mwende kwa wazazi wake, weza kwenda na baba,mama,kaka,mjomba does'nt matter,nyie nendeni,mtalipishwa faini itakuwa imetoka hiyo.
B) Tafuta ndugu upande wa mke ambaye mkeo anamweshimu sana,mpasulie ukweli kuwa umezaa na huyo mdada,mwombe akuite wewe na mkeo na kwenye kikao yeye ndo atamke yeye na sio wewe kisha mama watoto akikuhoji jibu 'ndiyo' halafu usiongee sana,be cool,akipandisha just stay quite ila akijitia kurusha ngumi mtandike maana si ruksa akunyanyulie mkono hata kama una kosa.
Katika hili aki pack na kuondoka kamwe usimfuate,its up to her kuamua kurudi au kuacha,nakuhakikishia atarudi,hujaua mtu aslan.
Always remember waume wa kwelituko wachache sana hapa mjini na hakuna mwanamme anaachwa siku hizi.
Najua it sounds arrogant ila ukweli i am advising by drawing on my deep experience ya ku deal na mama zetu hawa.
 
DUH!!!
Pole sana but ni vizuri wife ajue,,,,,,,,sasa jinsi ya kumwambia na effects zake ndo mh!!!!

may be,,, nunua namba nyingine utume sms kwako(ujidai ndo huyo binti) ambayo unajua mkeo ataiona kama hamyimani cm. mfano (nimekutana na rafiki yako ndo kanipa namba yako, nina mtoto au watoto wako kutokana na tendo tulilofanyaga ulipokua huku, naomba unipigie tafadhali tuongee),,,,alaf cku hiyo unakua na huzuni kwa mkeo mpaka bas na kukuna kichwa, huli chakula vitu ka hivyo,,,,,,hata akiiona anajua kuwa unajutia na atakufariji ingawa atakulalamikia
 
Lete watoto nyumbani kwa wazazi wako. Ulidhamiria uharibifu sioni kwa nini uogope. Hao mapacha wanaweza wakawa na maisha mazuri, ukiwatelekeza watakufanya kama Kanumba na Diamond.

Huwezi jenga moja kwa kubomoa nyingine, hiari yako kujenga zote au kubomoa zote.
 
Word!!!!

Mtoto wa kumkuta na mtoto wa kuletewa ni vitu viwili tofauti kabisaaaa!

Na mawazo ya humu achanganye na akili zake....maana asijechukua ushauri kumbe wanaomshauri kwa sasa wanaishi na mke wa saba; wao kuoa na ku divorce si issue (naongelea wale ambao dini hairuhusu na wanafanya).



Mamii ilikuwa rahisi kwa kuwa huyo mtoto ulimkuta to be frank nizungumze nikiwa ni mwanamke ni ngumu sana kukubali kulea mtoto aliyekukuta.maana kupitia kwake unauona uovu wa mumeo,kupitia kwake unjiona labda pengine kuna sehemu hukukamilika,kupitia kwake unazidi kujihisi una mapungufu si unajua siye wanawake tunavokimbilia kujilaumu katika kila makosa ya waume zetu,so please tusilinganishe mtoto wa nje ya ndoa na mtoto wa kabla ya ndoa hawa ni watoto tofaut KABISA,na justification zake pia ni tofauti,mimi mume wangu aniletee hata watoto kumi ambao aliwapata kabla ya kunijua mimi nitawalea maana inawezekana mimi ndiye sababu ya mama yao kuachwa,lakini walio chini ya umri wa ndoa yangu please!mwanaume anapaswa kuwa na busara sana tena sana PLUS MAOMBI!vinginevyo akiendekeza zile za kidume dume za "HAYAISHI,YANI BADO UMEKASIRIKA TU,MKE WANGU SI UNISAMEHE,MBONA HATA KAKA NAE ANA MTTOT MWINGINE NA HAJAMWAMBIA MKEWE SI BORA MI NIMESEMA,!''mambo yanaweza kuwa mabaya sana.nimejaribu kuvaa viatu vya huyo mke though najua siwezi kuimagine atareact vipi!
 
Nayo kweli itakuweka huru, nawe utakuwa huru kweli kweli. Funguka kwa mkeo, mwambie ukweli ya kilichotokea, atakasirika, itamuuma lakini ndo ukweli wenyewe na kama ni muelewa basi atakuelewa. Akishakuelewa chukua watoto wako uwalee kwa mapenzi yote, kama unayowapa hao watoto wa mkeo.

Kuna mchangiaji mmoja amekuuliza ikitokea yule mdada akafa, unadhani hao watoto utawatunzaje tena, manake hiyo laki unamtumia huyo mdada, akifa? Usifanye watoto wakakua katika mazingira magumu wakati uwezo wa kuwatunza na kuwalea unao, plz, ongea na mkeo, tunakuwaga wakali but naamini atakuelewa. All da best
 
Yaaani, roho inaniuma utafikiri mie ndio huyo dada niliyezalishwa..nway, Nakupongeza kwa kuonesha moyo wa kuwajali hao viumbe na nakupa pole kwa kuitia dosari ndoa yako. Nakushauri uonane na familia ya huyo dada, waweke wazi kuwa tayari una mke na watoto. Jipe muda kuisoma familia yao ni watu wa namna gani huku ukiendelea kuhudumia hao malaika. Kama ni watu wakorofi inabidi uendelee nao kisiri siri na umjengee huyo mama mazingira mazuri ya kujitegemea. Mkeo anapaswa kufahamu hili ila zingatia mambo mawili kabla ya kumfahamisha. Kwanza, maamuzi atakayochukua (akusamehe aendelee na ndoa au adai talaka), pili zingatia familia ya yule binti. Iwapo familia ya yule binti sio watata na ikatokea umemwambia mkeo ila akadai talaka inamaana hapo uwe tayari kuendelea na huyo binti kama mke na mume. Kama familia yao ni watata na unaona huwezi kucope na huyo binti nakushauri usimwambie mkeo hadi hapo watoto watakapokuwa wakubwa. Ila unahitaji kuwa smart katika huu mchezo.
 
duu,huu uzi kweli nimechelewa.mfikirie na huyo aliebeba uja uzito.unampotezea muda wake,na wafikirie hao watoto,baba ni yule muwajibikaji wa vitendo juu,sio kutuma hela tuu.be honest kwa mke wako,muanzie kwa mbali,kuliko kuiendeleza kuwa siri.no one is perfect,ila tunapokesea ni vizuri kujaribu kuparekebisha
 
1. Ulimdanganya binti kwamba hujaoa ukampa jina la uongo
2. mlipoona ukaendelea kumdanga na wakati huo unajua kabisa una familia
3. ili kuficha uongo wako ukaanza kumwaga mijihela, maana kijijini kumkabidhi binti laki 3 ni hela nyingi kidogo
4. ukaenda kusajili line kwa jina lile la uongo ili uendelee kumdanganya na hele ua matumizi unatuma kila mwezi!!!

kama huko kijijini maisha yao ni choka mbaya huoni wazazi wanakuwa wakali ili umchukue huyo binti kwasababu hawajui kama una mke? na huyo binti ni wakijiji chenu au cha jirani? maana ninavyojua watu vijijini wanafahamiana sana, kweli binti akuelezee jinsi ulivyo washindwe kutambua ni mtoto wa fulani kweli na ivi unasema watoto wanafana!?

fanya hima uweke mambo hadhari mwenyewe maana huyo mkeo akisia ndo umeharibu kabisa

afu kama wewe ni ngosha kweli unanifanya niconclude reseach yangu ninayowafanyia kina ngosha, "when it comes to inf ni waongo sana aisee"
 
Wakati unafanya uzinzi ulituomba ushauri nenda kamuombe mke wako atakusaidia kwa hili

Kuwa muungwana tia zipo domo lako. Si lazima uchangie kama huna ushauri wa maana. Mwenzio ana matatizo ndio maana kaamua kuanika ukweli wake ili asaidiwe. Makosa tunayafanya sote. Si vema kuhukumiana.
 
Wakati unafanya uzinzi ulituomba ushauri nenda kamuombe mke wako atakusaidia kwa hili

Kuwa muungwana, tia zipu domo lako. Si lazima uchangie kama huna ushauri wa maana. Mwenzio ana matatizo ndio maana kaamua kuanika ukweli wake ili asaidiwe. Makosa tunayafanya sote. Si vema kuhukumiana.
 
kiongozi mi sina ushauri!nikupongeze tu kwa kutoa mapacha!hivi kutoa mapacha ni kipaji,karama,maarifa au bahati?
 
Ndahani mbona wanitenda hivyo mwana wa mwenzio..........

Let me fafanua basi wanawake siku hizi wanakazi nzuri, wanamikwanja kwa sana, so kumtisha eti atakosa pa kwenda au atashindwa maisha ni kujidanganya hapo cha muhimu ni huyo mwanamke kukubali matokeo tu MWANAUME WA PEKE YAKO UTAMTOA WAPI SIKU HIZI???
Teh teh teh...mimi najipigia debe ntakuwa wa mwanamke mmoja tu. Unajua ulitema cheche mpaka nikasema kuna mtu anapigwa karate hapa akileta za kuleta...anyway ni kweli wanawake wako empowered kama wanaume kwahiyo hakuna wa kumtishia mwenzake. Ila inakuwa poa kama hata cost sharing inapewa umuhimu.
 
Mkuu mimi sitakupa pole ila nikupongeze na ninakulaumu kwa kutokuwajibika ipasavyo!

Binafsi ninaamini kwamba hakuna aliye mkamilifu na kama ni kukosa wengi tumejikuta tunafanya kinyume na maadili zetu hivyo huna sababu ya kujutia kitendo hicho. Kimsingi uliongozwa na tamaa Mungu akabariki coz watoto siku zote ni baraka otherwise wengi wanahangaika kuwatafuta hata kwa waganga na bado ngoma haionekani.

This is what you have to do from my own opinion, be honest to yourself first. Be honest to the person you respect most after your wife, then be open to your wife infront of as many respectable people as possible.

Huwezi kuishi kwa kujificha ni hatari mno, jitokeze home kwenu wape ukweli, kama wazazi wapo mwagize shemeji aende home huko akutane nao wamuandae kisaikologia then utambulishe mada.

Ninaamini hao watoto watakuwa chanzo cha baraka kwako na familia na ninakuombea Mungu amuonyeshe njia shemeji akuelewe.

Once a man, always a man!
 
sema ukweli japokuwa unauma. Jambo hilo huwezi kulificha maisha yako yote. Kumbuka mahitaji yao yanakua kama wanavyokua wao hivyo huwezi kufanya siri muda wote wa maisha yako. Mwisho wao hawana hatia ww ndiye mwenye hatia na kadri unavyochelewa ndivyo unavyozidisha hatia yako. Chukua hatua haraka kaka.
 
Back
Top Bottom