Najutia kufuata ushauri mlionipa kumuonea huruma muuza duka auze bidhaa zake, wachache mlionishauri niweke huruma pembeni mnajua biashara

Najutia kufuata ushauri mlionipa kumuonea huruma muuza duka auze bidhaa zake, wachache mlionishauri niweke huruma pembeni mnajua biashara

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Kuna uzi niliweka humu jamiiforums Nilimruhusu msaidizi auze bidhaa zake ndogo ila zinamlipa kuzidi mshahara wake. Je, nifanye maamuzi gani?

Summary / Muhtasari:

Msaidizi aliniomba aanze kuuza bidhaa zake, Sina uzoefu sana kwenye biashara niliona nitakuwa kauzu nikimkatalia, nilitaka kuonekana nipo "fair", NIKAMRUHUSU !

Niliweza kupata mbinu ya kujua hesabu zake, kuna kidaftari huwa anakificha sehem flani, nikiona hayupo nakipiga picha fasta
  • Mwezi wa 10 kapata faida 183,500
  • Mwezi wa 11 kaingiza faida 413,000
  • Mwezi wa 12 alianza kutunza mzigo mpaka stoo, Mwezi haujaisha ila faida inakaribia 700,000
  • Mwezi wa 11 katikati nilipata taarifa kauza simu yake laki 2 na kitu, kwa hesabu za fasta aliingiza kwenye mtaji.

Mshahara naomlipa ni 150,000 + allowance ya matumizi elf 70, jumla 220,000 kila mwezi

Kwa upande mwengine biashara yangu imeshuka sana, Mwezi wa 10 faida ilikuwa laki 3, Mwezi wa 11 faida laki 2 na 15, mwezi huu laki 2 na 40

Gharama za biashara jumla ni 870,000 kila mwezi
  • frame - 500,000 ( ni kwetu wachache tulioziwahi, wengine ni laki 8)
  • mshahara na allowance - 220,000
  • Tra, Jiji, umeme, maji, usafi, n.k. - 50,000

Nikafungua uzi humu jamiiforums niombe ushauri nichukue hatua zipi, nilishambuliwa sana kwamba nina ROHO MBAYA nimuache niwe na HURUMA. Ndicho nilichofanya !!

Matokeo yake
  • Anajali zaidi biashara yake kuzidi yangu, Hapo zamani alikuwa ananipa mwendendo wa biashara , hesabu, n.k. sikuhizi kaacha kabisa, ni mpaka nimkumbushe.
  • mara kadhaa nimefika dukani hayupo, nilifuatilia na kugundua anaenda kujumua mzigo wake.
  • Namlipia frem, kodi, jiji, usafi, chakula, n.k. lakini bado anaendelea kuchukua allowance ma mshahara licha ya kwamba biashara yangu inachechemea huku yake inanawiri bila gharama zozote.
Siku ya jana nimemuambia haya
  • Mwaka huu naongeza bidhaa hizo anazouza, Kwa location nilipo kuna wateja wengi
  • Biashara zote zinazofanyika dukani zitakuwa mali ya duka, Ikiwa muuza duka kanipa idea nitamkadiria comission.
Najua fika kabisa mtu alieanza kuzoea faida za laki 7 ukijumlisha na allowance ya laki 2 ni ngumu kukubali kushuka upya, Kwa saikolojia ya binadamu najua atatafuta mbinu, Nilichofanya ni kuweka cctv Camera tarehe 17 mwezi huu na kumuacha aendelee na biashara yake, Lengo likiwa ni kuanza kuitumia cameranikianza kuweka mzigo wangu.

Kwa upande mwengine wala simkatazi awe na biashara yake, Itapendeza zaidi apate ukomavu na uzoefu zaidi kwa kuanza kujilipia gharama za biashara, mfano frem laki 8 (minimum miezi 6), umeme, tra, jiji, n.k.

Kuna wadau mmenishauri nitafute muuza duka mwengine, ikiwa kuna dalili za kuto kuelewana au usumbufu nitafanya hivyo.
 
Huo upuuzi mimi siuwezi ni sawa unamifugo halafu anatokea mpuuzi anasema naomba kamfugo kangu nichanganye na mifugo yako ili namimi nijisogeze kidogo...jicho nitakalo mpiga kabla ya kumjibu atajua huyu mtu amekataa...Tenganishen biashara japo ulishakosea muamishe haraka sana.
Huku wewe unaendelea kugharamika ulinzi, chakula, matibabu, kodi, n.k.
 
Ndugu zangu mjini kuna mambo mengi. Kuna jamaa alikuwa mpishi hotelini alikuwa anauza kuku wake mwenyewe. Yaani anatumia viungo na mafuta ya boss. Walikuwa wanapeana zamu ya Wiki na anaekusanya fedha. Wiki hii yeye Wiki ijayo anaekusanya fedha. Boss anashangaa mbona kuku hawalipi mpaka wanaoza kwenye Friji. Wakikaribia kuoza wafanyakazi wanakula bure kabisa. Katika biashara ukiwa na wafanyakazi wengi hakikisha unakuwa karibu karibia na kila mfanyakazi. Ukiwafanya wafanyakazi wa chini wakuogope kama mmiliki au Boss na ukawa karibu na viongozi uliowaajiri utakufa vibaya sana kibiashara .
 
Huo ni ubepari kwenye biashara bila ubepari na huruma hutoboi
Ubepari sio kitu cha kushabikia mana hauna huruma. Kwa muktadha huo jamaa aweke conditions ambazo zitamuamsha tena jamaa kuwa yukona biashara ya mtu anatakiwa auze. Mana nina hakika hiyo karatas aliyoiona hapo ndani ndo anaona dogo anafaidi. Akimtoa hapo bila kuona muelekeo mzuri atamuharibia maisha kabisa
 
Ndugu zangu mjini kuna mambo mengi. Kuna jamaa alikuwa mpishi hotelini alikuwa anauza kuku wake mwenyewe. Yaani anatumia viungo na mafuta ya boss. Walikuwa wanapeana zamu ya Wiki na anaekusanya fedha. Wiki hii yeye Wiki ijayo anaekusanya fedha. Boss anashangaa mbona kuku hawalipi mpaka wanaoza kwenye Friji. Wakikaribia kuoza wafanyakazi wanakula bure kabisa. Katika biashara ukiwa na wafanyakazi wengi hakikisha unakuwa karibu karibia na kila mfanyakazi. Ukiwafanya wafanyakazi wa chini wakuogope kama mmiliki au Boss na ukawa karibu na viongozi uliowaajiri utakufa vibaya sana kibiashara .

Mbona wahindi hawafi vibaya kibiashara na ndio wanaoongoza kwa kuwatisha na kuwanyoosha wafanyakazi wao?
 
Back
Top Bottom