Kuna uzi niliweka humu
Nilimruhusu msaidizi auze bidhaa zake ndogo ila zinamlipa kuzidi mshahara wake. Je, nifanye maamuzi gani?
Summary:
Msaidizi aliniomba aanze kuuza bidhaa zake, nilimruhusu !
Niliweza kupata mbinu ya kujua hesabu zake, kuna kidaftari huwa anakificha sehem flani, nikiona hayupo nakipiga picha fasta au naweza kumtuma aninunulie vocha nakipiga picha fasta.
- Mwezi wa 10 alikuwa na faida ya 183,500
- Mwezi wa 11 kaingiza faida ya 413,000
- Mwezi wa 12 alianza kutunza mzigo mpaka stoo, Mwezi haujaisha ila faida inakaribia 700,000
Mshahara naomlipa ni 150,000 kwa mwezi, allowance ya matumizi yake elf 70, jumla 220,000
Meanwhile biashara yangu imeshuka sana Mwezi wa 10 faida ilikuwa laki 3, Mwezi wa 11 faida laki 2 na 15, mwezi huu laki 2 na 40
Gharama za biashara
- frame - 500,000 (Gharama hii ni kwetu wachache tulioziwahi, wengine ni laki 8)
- mshahara na allowance - 220,000
- Tra, Jiji, umeme, maji, usafi, n.k. - 50,000
Ni mwezi wa 11 nilifungua uzi humu kipindi hicho hesabu zake hadi tarehe 13 faida inasoma 186,500 niombe ushauri nichukue hatua zipi, nilishambuliwa sana kwamba nina
ROHO MBAYA nimuache niwe na
HURUMA.
Ndicho nilichofanya, Matokeo yake
- Anajali zaidi biashara yake kuzidi yangu, Hapo zamani alikuwa ananipa mwendendo wa biashra , hesabu, n.k. sijgizi kaacha kabisa.
- Biashara yake kwanza yangu baadae, mara kadhaa nafika dukani hayupo, nilifuatilia na kugundua anaenda kujumua mzigo wake.
- Namlipia frem, kodi, jiji, usafi, chakula, n.k. lakini bado anaendelea kuchukua allowance licha ya kwamba anaingiza pesa nyingi.
Siku ya jana nimemuambia haya
- Mwaka huu naongeza bidhaa hizo anazouza, Kwa location nilipo kuna wateja wengi mno.
- Biashara zote zinazofanyika dukani zitakuwa mali ya duka, Ikiwa muuza duka kanipa idea nitamkadiria cha juu ama tutakuwa tunaenda kwa percent.
Najua fika kabisa mtu alieanza kuzoea faida za laki 7 ukijumlisha na allowance ya laki 2 ni ngumu kukubali kushuka upya, Kwa saikolojia ya binadamu najua atatafuta mbinu, Nilichofanya ni kuweka cctv Camera tarehe 17 mwezi huu na kumuacha aendelee na biashara yake, Lengo la hiocamera ni kumchunguza nikianza kuweka mzigo wangu.
Kwa upande mwengine wala simkatazi awe na biashara yake, atapata ukomavu zaidi kwa kuanza kujilipia gharama za biashara, mfano frem laki 8 (minimum miezi 6), umeme, tra, jiji, n.k. (Faida = mapato - gharama)