Najutia kuoa kwa kukurupuka na kutumia hisia sehemu ya kutumia akili

Najutia kuoa kwa kukurupuka na kutumia hisia sehemu ya kutumia akili

KUKULU- KAKALA

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2019
Posts
312
Reaction score
1,299
Wakuu habari! Poleni na majukumu na hongereni pia.... Nimepewa ruhusa na mhusika wa tukio hili niweze kushare humu ndani kisa kilichomtokea kutoka Kwa Binti aliyemuoa yapata miezi mitano Sasa.

Nina Jamaa angu ni mwenyeji wa Mara Lakini kwasasa anaishi Mbeya na tunaishi Naye Kwenye apartment za eneo moja. Jamaa ni mpambanaji sana na ni mlevi sana pia wa pombe.

Mwaka Jana mwezi wa Kumi alikutana na Binti Fulani tumuite ( Flora) akiwa Kwenye shughuli Zake za upambanaji Binti ni mwenyeji wa Kagera ila alikuja Mbeya kutafta Maisha. Jamaa akampenda Binti na akaanza mahusiano Naye Rasmi na MWEZI WA 12 wakafanikiwa kufunga ndoa.

Binti wakati anakuwa approached alimwambia Mwamba kuwa yeye ana mahusiano ( MULTIPLE RELATION) kama Mbili moja ni Mwanaume ambaye wazazi wake walimtaftia Huko Kwao Kagera na mwingine ni Mwalimu yupo Mbeya ila akakubali kuwa kama utanioa Kweli Niko Tayari kuachana Nao.

Jamaa kwavile alimpenda Binti akakubali na wakafunga ndoa Binti akidai kuwa ameamua aachane na hao watu wake WA zamani. Yule aliyesema fimbo ya Mbali haiui nyoka Kumbe alikosea aisee inategemeana na urefu wa fimbo. Baada ya ndoa Mwanzo walikuwa POA sana na Maisha yalikuwa mazuri full upendo..kupeana unyumba Hadi kero Kwa majirani..kutoka wote na Mwamba akampa mtaji jamaa kama million 2 Kwajili ya biashara ndogo ndogo.

Tatizo lilianza pale Ambapo mwamba alianza kushika Simu ya Bebi wake. Hakuamini alichokiona.... Akagundua kuwa Binti Bado ana endelea na mahusiano na Watu wake WA kale Hasa yule WA Kagera na anamponda Mwamba Kwa washikaji Zake kuwa nilimkubalia anioe tu kisa sikuwa na pakwenda na Maisha yalikuwa magumu ila Mimi Nakupenda wewe na nipo Tayari kuachana Naye we tafta biashara nzuri Huko Kagera Kisha nitakuja tuanze Maisha mtaji ntakupa Mimi na ntakua nakutumia Laki 3 Kila MWEZI Kwajili ya kujikimu.

Mnasemaga hakuna mkurya mjinga Basi huyu Jamaa angu Alikuwa mjinga Sana pamoja na Kuona sms hizo Binti akasema Hamna baby hizo sms SIO zangu ni za Rafiki Angu anaazimaga simu kwangu achat na wakwao. Jamaa akaamini na kuendelea na Maisha. Kali kuliko Kuanzia mwezi wa Tatu Jamaa kanyimwa Show Kumbe ni maelekezo KUTOKA Juu kuwa usimpe Mwambie unaumwa. Juzi Tarehe 6 Jamaa kakuta Chatting za Baby wake akiambiwa mwezi wa tano Njoo Kagera tuendelee na Maisha na wife kaanza kumsumbua Mwamba kuwa anataka akasalimie Kwao.

Katika story za HAPA na pale nikagundua makosa kadhaa Mwamba alifanya kabla hata ya kuoa na ndiyo yanayomgharimu Mpaka Sasa.

1) Jamaa aliamua kutumia Hisia badala ya Akili Kwenye kuoa.

Alijua kabisa mwanamke ana Watu wengi Lakini Bado alimwamini akijua atabadilika.

2) Jamaa alivutiwa na Shepu kuliko Akili ya mwanamke na Tabia.

Mwanamke alionyesha Toka Mwanzo Yuko kimaslahi Zaidi na ndo kwanza ndoa Ina miezi mitatu alishamletea Jamaa Hadi wadogo zake awalee huku Jamaa ndo anaanza Maisha na kuwahamisha Shule kabisa Toka Kagera Kuja Mbeya.

3) Jamaa alipuuza viashiria vidogo vidogo Toka Mwanzo vyenye Dalili ya kukosa uaminifu baina Yao

Small small details matters a lot.
- Binti Kila simu ikipigwa Alikuwa ANATOKA kuongelea NJE.

4) Jamaa alikurupuka kuoa MTU ambaye hajamjua vyema.


5) Jamaa alikosa CODES za kiume.

Kushika simu ya MWANAMKE ni Kosa kubwa sana alilolifanya. Kuna mtu alisema wenzetu WA jinsia Ke ni kama hawajui wanataka nini. Unaweza mnunulia gari ya million 25 akampenda Mwanaume aliyempa ofa ya mafuta ya efu 15 na kukuona uliyemnunulia gari si kitu


5) Jamaa alioa Kisa umri unakimbia na SIO KISA kapata mtu SAHIHI.

Peer pressure na mob psychology zinawapoteza Vijana wengi sana na kuangukia Kwa wanawake waovyooo.

Mwisho: NIWATAKIE SIMBA SC USHINDI WA KISHINDO NA KUVUKA SALAMA.
 
Tako jamani tako huyo atakuwa alikuwa anapewa tope 🤣🤣🤣🤣 ukionja tope huwezi waelewa washauri maama ile raha unayopata wakati wakula tope acha kabisa.

Anyways vijana tuwe makini na haya matakoz. Tutumie akili na sio hisia. U will never go wrong.
 
Inakuaje ndoa ililyofungwa kwa sala , dua na mizimu ivunjike kisa simu ya 2M kushuka chini.

We need to know detachment is something hardest.

Ukioa mwanamke au mwanaume akioa nyote mnabidi kujipa miaka kumi ya kusahau x wako is not easy to forget the one ambaye mmeshare good moment it takes time
 
Back
Top Bottom