Najutia kuoa kwa kukurupuka na kutumia hisia sehemu ya kutumia akili

Najutia kuoa kwa kukurupuka na kutumia hisia sehemu ya kutumia akili

Wakuu habari! Poleni na majukumu na hongereni pia.... Nimepewa ruhusa na mhusika wa tukio hili niweze kushare humu ndani kisa kilichomtokea kutoka Kwa Binti aliyemuoa yapata miezi mitano Sasa.

Nina Jamaa angu ni mwenyeji wa Mara Lakini kwasasa anaishi Mbeya na tunaishi Naye Kwenye apartment za eneo moja. Jamaa ni mpambanaji sana na ni mlevi sana pia wa pombe.

Mwaka Jana mwezi wa Kumi alikutana na Binti Fulani tumuite ( Flora) akiwa Kwenye shughuli Zake za upambanaji Binti ni mwenyeji wa Kagera ila alikuja Mbeya kutafta Maisha. Jamaa akampenda Binti na akaanza mahusiano Naye Rasmi na MWEZI WA 12 wakafanikiwa kufunga ndoa.

Binti wakati anakuwa approached alimwambia Mwamba kuwa yeye ana mahusiano ( MULTIPLE RELATION) kama Mbili moja ni Mwanaume ambaye wazazi wake walimtaftia Huko Kwao Kagera na mwingine ni Mwalimu yupo Mbeya ila akakubali kuwa kama utanioa Kweli Niko Tayari kuachana Nao.

Jamaa kwavile alimpenda Binti akakubali na wakafunga ndoa Binti akidai kuwa ameamua aachane na hao watu wake WA zamani. Yule aliyesema fimbo ya Mbali haiui nyoka Kumbe alikosea aisee inategemeana na urefu wa fimbo. Baada ya ndoa Mwanzo walikuwa POA sana na Maisha yalikuwa mazuri full upendo..kupeana unyumba Hadi kero Kwa majirani..kutoka wote na Mwamba akampa mtaji jamaa kama million 2 Kwajili ya biashara ndogo ndogo.

Tatizo lilianza pale Ambapo mwamba alianza kushika Simu ya Bebi wake. Hakuamini alichokiona.... Akagundua kuwa Binti Bado ana endelea na mahusiano na Watu wake WA kale Hasa yule WA Kagera na anamponda Mwamba Kwa washikaji Zake kuwa nilimkubalia anioe tu kisa sikuwa na pakwenda na Maisha yalikuwa magumu ila Mimi Nakupenda wewe na nipo Tayari kuachana Naye we tafta biashara nzuri Huko Kagera Kisha nitakuja tuanze Maisha mtaji ntakupa Mimi na ntakua nakutumia Laki 3 Kila MWEZI Kwajili ya kujikimu.

Mnasemaga hakuna mkurya mjinga Basi huyu Jamaa angu Alikuwa mjinga Sana pamoja na Kuona sms hizo Binti akasema Hamna baby hizo sms SIO zangu ni za Rafiki Angu anaazimaga simu kwangu achat na wakwao. Jamaa akaamini na kuendelea na Maisha. Kali kuliko Kuanzia mwezi wa Tatu Jamaa kanyimwa Show Kumbe ni maelekezo KUTOKA Juu kuwa usimpe Mwambie unaumwa. Juzi Tarehe 6 Jamaa kakuta Chatting za Baby wake akiambiwa mwezi wa tano Njoo Kagera tuendelee na Maisha na wife kaanza kumsumbua Mwamba kuwa anataka akasalimie Kwao.

Katika story za HAPA na pale nikagundua makosa kadhaa Mwamba alifanya kabla hata ya kuoa na ndiyo yanayomgharimu Mpaka Sasa.

1) Jamaa aliamua kutumia Hisia badala ya Akili Kwenye kuoa.

Alijua kabisa mwanamke ana Watu wengi Lakini Bado alimwamini akijua atabadilika.

2) Jamaa alivutiwa na Shepu kuliko Akili ya mwanamke na Tabia.

Mwanamke alionyesha Toka Mwanzo Yuko kimaslahi Zaidi na ndo kwanza ndoa Ina miezi mitatu alishamletea Jamaa Hadi wadogo zake awalee huku Jamaa ndo anaanza Maisha na kuwahamisha Shule kabisa Toka Kagera Kuja Mbeya.

3) Jamaa alipuuza viashiria vidogo vidogo Toka Mwanzo vyenye Dalili ya kukosa uaminifu baina Yao

Small small details matters a lot.
- Binti Kila simu ikipigwa Alikuwa ANATOKA kuongelea NJE.

4) Jamaa alikurupuka kuoa MTU ambaye hajamjua vyema.


5) Jamaa alikosa CODES za kiume.

Kushika simu ya MWANAMKE ni Kosa kubwa sana alilolifanya. Kuna mtu alisema wenzetu WA jinsia Ke ni kama hawajui wanataka nini. Unaweza mnunulia gari ya million 25 akampenda Mwanaume aliyempa ofa ya mafuta ya efu 15 na kukuona uliyemnunulia gari si kitu


5) Jamaa alioa Kisa umri unakimbia na SIO KISA kapata mtu SAHIHI.

Peer pressure na mob psychology zinawapoteza Vijana wengi sana na kuangukia Kwa wanawake waovyooo.

Mwisho: NIWATAKIE SIMBA SC USHINDI WA KISHINDO NA KUVUKA SALAMA.
kwani ungesema ni wewe ndie uliyeoa kuna ubaya?
 
Ukioa rasmi halafu ukafanyiwa vituko inauma sana!

Wakati mwingine ikiwa sio rasmi ukafanyiwa vituko unasema "Ntaoa Tena" ogopa Sasa uwe mfia Dini Tena mkristo madem wanawapenda sana hao coz Kuna hakikisho la umilele!

Huyo dem ni "Mshangazi mdogo mdogo"kama huyu ninaemuona hapa site!!!
 
HAKUFANYA KOSA KUSHIKA SIMU YA MKEWE ila alikosea kutomchunguza vizuri tangu mwanzo alitakiwa Alie timing simu hasa baada ya kuambiwa kuwa alikuwa na mahusaiano happy nyuma
 
"Kushika simu ya MWANAMKE ni Kosa kubwa sana alilolifanya. Kuna mtu alisema wenzetu WA jinsia Ke ni kama hawajui wanataka nini. Unaweza mnunulia gari ya million 25 akampenda Mwanaume aliyempa ofa ya mafuta ya efu 15 na kukuona uliyemnunulia gari si kitu"

Unampondea mwenzako kumbe wewe mwenyewe FAMBA TU!!.

Yaani unaogopa vipi kushika simu ya huyo malaya wako.Nyie vijana hivi kama hamuwezi uanaume si mleft group kuliko hizi fedheha za rejareja.

Nakuelekeza kesho ufike makao makuu ya chama KATAA NDOA.Uchukue barua yako.Na kwanzia J3 uwe u ahudhuria vikao vya jioni kwaajili ya kujifunza mbinu na code za kiume.

📌📌KATAA NDOA,NDOA NI UTAPELI!!!
 
Inawezekana kabisa mkuu.

I have a friend of search kind, alimpenda sana Mpare mmoja kwa muonekano na alikuwa mzuri kweli kweli,
Mwamba alipigwa matukio kidogo afariki.

Tena tukio la kwanza lilianza siku tu ya kupeleka mahari, huko milimani.
Jamaa aliletewa mtoto wa binti wa kijijini, daah nikawa mstari wa mbele kumnyima asitoe tena mahari.

Aliniwekea sana bifu akifikiri sitakia aoe demu mkali.
Tulishuka mlimani anani mind sana, kwanini nilitaka kumwaibisha Yvone wake mbele ya wazazi wake.
Anyway he is my friend ila nilijua hakuna anakokwenda, jamaa akaoa.
Mtoto wa kwanza, akakutwa na kadi mbili za cliniki. Bado hakuelewa kitu.

Mwisho wa siku yalikuja kumshinda jamaa tena kwa gharama kubwa sana.
Kudadekii zake Yule jamaa🤔
 
Back
Top Bottom