Wakuu Salaam,
Kama kichwa cha habari kinavyosema.
Niliwahi kuwa na rafiki yangu wa karibu sana,alikuwa sio mgonjwa au sikujua anaumwa. Tulikuwa tukikutana ana tabasamu zaidi ya mimi na muda wote alikuwa anafuraha mpaka mimi alikuwa ananishauri akiniona sina furaha.
Siku moja aliniambia anafikiria kujiua sikushtuka nikamshauri kidogo kama vile ushauri wa vijana, wiki mbili baadaye akajinyonga. Nimekaa na hili jambo muda mrefu sana lakini limegomakutoka kwenye nafsi yangu, sina furaha, najilaumu, ninahisi sikutimiza wajibu wangu sehemu fulani ambayo ukiniuliza ni sehemu ipi siijui lakini ninahisi kama rafiki yake nilifeli kumsaidia.
Huu ni mwaka wa 12 sasa naishi kwa maumivu makali sana na sijui nitajitoaje. Je, kuna mtu alishawahi kuwa katika mazingira kama yangu na alisahau vipi akawa na furaha na amani kama zamani?,Mimi nimeshindwa kutojilaumu! popote ulipo Suleiman Nisamehe!
Kama uliwahi kujutia kitu ambacho unahisi ungekifanya na hukukifanya hebu tirirka hapa tuone msaada unaoweza kupatikana.
Bas bhana wakati nasoma sekondari ilitokea nikapata dada ambaye alinipenda sana kiufupi tuliivana vizuri na kila mtu akawa anajua sisi ni ndugu wakat huo yeye anasomea ualimu mimi niko form2. Boyfrend wake alikua akinichukulia mie shemeji yake kabisa kwa kipindi hicho mie mdogo wao dada p yupo ualimu na mpenzi wake yeye kwasabu kwao kulikua na uwezo alipelekwa form5&6.
Kumbuka hawa wapenzi walianza mapenzi yao tangu wakiwa shule ya msingi ila sekondar walitenganishwa japo hawakuacha mawasiliano ila ukubwan ndiyo kama hivo walikuja wakakutana tena na mapenz yakaanza upyaaaa.
Japo kulikua na tofaut wakat wanasomea masomo ya juu kwasabu msichana tayar alianza kuwa na mabuz ili ajiendeshe kimaisha kutokana na maisha ya kwao kuwa dun hivyo hata aliyekua akimsomesha kazi yake hiyo ni buz lake na alikua na mabuz wengine pia ambao sasa mie kama mdogo mtu nilikua nawajua kwasabu ndo nilikua natumika kimawasiliano hasa ukizingatia miaka hiyo simu hazikua sana.
Baadae tulikua! na wale wapenz japo walizaa lakin walitengana kutokana na mwanaume alijua tabia za dem wake akachoka.
Ila sasa wakati wanaachana wote walikua washapata kazi mwanaume anafanyia dar mwanamke anafanyia mkoani vijijni huko mie nami nikawa nimekua nikapata boyfrend ambaye ni rafiki yake na shemeji yangu kwahiyo mara nyingi nilikua nikionana na shemeji na dada pia kwa wakat tofaut .
Sasa gafla dada akaumwa mi sikujua kumbe chanzo cha kuachana kwao ni pamoja na huyu dada alipata ukimwi kwahiy kama mnavyojua tena ukiumwi unaua mie mda mrefu kidogo sijawasiliana na dada kutokana na majukumu nilienda kusoma nje ya nchi kurudi nikawa nimejishkiza kwenye ofis ya serikal ambayo boyfrend wangu alikua anaijua siku hiyo nikapokea simu kuwa dada yako p amefariki dah! Niliumia sana kwakua pia sikupata nafas ya kwenda kuzika siku zikapita.
Siku hiyo nikaamua nimpigie dadaake na p simu kumjulia hali uwii nilikutana na shutma nzito sana kuwa mimi nilianza kutembea na shemeji yangu na nilikua najifanya nampelekea zawadi dada p na kumueleza mambo ya shem kumbe mnafiki tu yaan nilipata shutuma nyingi mnooo na kwamba dada p kafa akinitaja kuwa mimi ni mnafiki saana na amenichukia hata akifa nisiende kuzika asee niliumia kwa kipindi kirefu mnoo kutokans na hizo shutma saana!
Nikawa nataman dada p afufuke au mimi nife nikutane naye huko kwa mungu nimwambie siyo kweli maneno aliyoambiwa!
Hadi siku moja nikaota dada p amekuja akanikuta uwanjan akawa ananiambia twwnde mdogo wangu twende kule niliko huku ulipo siyo pazuri et ananivuta mkono mi nikawa nakataa ila nikamwambia dada p huko uliko naimani ni pakujua ukwel sasa je umejua ukweli kuhusu mimi na shemeji? Akaniambia ndiyo mdogo wangu siyo kweli kumbe ni watu tu walituchonganisha ndiyo maana nakwambia nifuate huku ulipo siyo pazuri utataseka tu. Nikamwambia hapana we bora umejua ukweli mie huko siend wewe nenda tu!
Baada ya ile ndoto nadhan sasa ndiyo roho yangu ikapumua japo hadi leo sitakagi kumuona ndugu yake yoyote kwasabu wameshanihukumu tayar na siwez kuwabadilisha tena.