siku ya Idd nilimpigia simu rafiki yangu nikitaka kujua kwanini hakunialika/kunikaribisha kwenye IDD wala hakunitumia ujumbe hata zile za kufowadiana tu ( Yeye alikua mwislam) na tulikua na mazoea haya ya kukaribishana au hata kujuliana hali tu kila mara, basi nikapiga, haikupokelewa, nikazidi kupatwa mashaka maana haikua kawaida yake, nikajua akiona missed call yangu atanipigia, ila hadi asubuhi ya siku iliyofuata hakupiga, nikazidi kukosa amani. Nakumbuka ilikua mida ya saa tatu asubuhi nilikua nimetoka home nikapiga tena simu ila nikaanza kukosa tu amani bila sababu ya msingi, mara simu ikapokelewa na sauti ya kike, sikustuka maana ni kawaida simu yake siku nyingine kupokelwa na mke wake. Nilivyosikia sauti ya kike nikaanza kumtania "Shemeji imekuaje mmekula iddi peke yenu bila kunikaribisha?:" nikaona kama vile yule mtu hanifahamu, ikabidi nitulie nimuulize, wewe si ni mama fulani? Akajibu akasema "Mimi ni Shemeji yake, jana nilikua kwako Baba fulani ni mgonjwa, hivyo wakati naondoka nikasahau nikabeba simu yao nikaacha yangu, wapigie kwenye namba ya airtel"
Nikaipiga namba ya mshkaji akapokea mke wake akaniambia jamaa yako ni mgonjwa, nikamwambia mpe simu niongee nae, akasema hawezi hata kuongea, aagh kidogo sikuamini maana tangu nimefahamiana na jamaa zaidi ya 15 years ago sijawahi kusikia anaumwa kiasi hiki, shida nini akaniambia. nikawashauri wampeleke hospital........ila hawakuweza.
Jioni ya siku ile nikapiga simu tena, nikaambiwa jmaaa bado hali yake sio nzuri, nikaongea na ndugu zake na bado nikasisitiza wampeleke hospital, Kaka yake akanijibu kuwa ni vyema niende kwanza nikamuone then mambo ya hospital yatafuata, Siku ya Mechi ya Kazier Chiefs na Simba SA bikajisemea moyoni wacha hii mechi ikiisha niende kwake hata kama ni usiku nikamchukue nimpeleke hospital.
Mechi iliish akwa Simba kufungwa, nikasema wacha tu nikalale muda huu nitaenda asubuhi nikamchukue nimpeleke hospital maana ndugu zake walikua wanasema amerogwa hivyo sikutaka sana kuingilia mambo ya ndugu japo mkewe alinielewa.
Asubuhi saa kumi na moja moja kuna namba ngeni ilinipigia mara mbili ila sikusikia simu, saa 12 asubuhi nikaamka nisikilize DW nikaona missed calls, nikawa najiiliza huyu anayepiga simu mida hii nani? Kupiga ile namba nikapokelewa na KILIO cha Mwanamke, dah nilikufa ganzi aiseeee....
Pengine ningeacha kwenda mpirani jana yake ningeweza kumuokoa Jamaa......Hii scenerio bado mbichi kabisa, nimeshiriki kila kitu kwenye msiba wake but naona nina hatia kubwa sana. Pumzika kwa amani Kaka.