Ikumbukwe Dr. Walid Amani Kabourou aliporudi CCM toka CHADEMA watu walihuzunika sana. Acheni Nakaaya aende, hivyo ndivyo anavyoandika historia yake. Tukumbuke mtu huzaliwa, akaishi mwisho hufa, ni historia inaundwa hiyo. Mwacheni aende, mwacheni Mbowe aende CCM kama atataka. Acheni mimi niende CCM kama ntataka. Mwisho wa siku Mapinduzi yaja kwa kuwa hata CCM yenyewe ilikuwa Chama Cha Mapinduzi na sasa ni CCM tu (CCM haina elements za Mapinduzi chanya yoyote). Kuna siku tutaamka, Watanzania wamekataa kunyanyaswa na kudanganywa.
Nawauliza ndugu zangu, ikiwa Slaa atashindwa hamdhani kuna watu watalia? Hakuna watu watakaorudi CCM na kumwacha Slaa na Mbowe? haitatokea?? Basi ukiona mambo kama ya Nakaaya yanatokea basi ujue ukombozi ndo waja huo. Ni wakati wa mafuta kujitenga na maji. Watakaokebehi nilichosema wafanye hivyo sasa, watakaonikosoa basi wanikosoe kwa hoja. Msinung'unike mioyoni mwenu kwa kuwa muda wa mapambano umekaribia sana.
Naomba kuwasilisha.