Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

hivi nakaaya 'alilazimika' kurudi ccm? :confused2:

May be alilazimishwa. Na nani, hilo ndo swali ambalo yeye pekee anaweza kujibu.

Hata hivyo nafsi pekee ndiyo inayoweza kumfanya mtu mwenye akili timamu alazimike au alazimishwe. Mbona watu kibao walifia kile wanachokiamini na leo tunawakumbuka kama heros? Nadhani amefanya kitu kizuri kuitumikia nafsi yake ambayo imemsuta kwamba she is not worth the status of joining real fighters.
 
Ikumbukwe Dr. Walid Amani Kabourou aliporudi CCM toka CHADEMA watu walihuzunika sana. Acheni Nakaaya aende, hivyo ndivyo anavyoandika historia yake. Tukumbuke mtu huzaliwa, akaishi mwisho hufa, ni historia inaundwa hiyo. Mwacheni aende, mwacheni Mbowe aende CCM kama atataka. Acheni mimi niende CCM kama ntataka. Mwisho wa siku Mapinduzi yaja kwa kuwa hata CCM yenyewe ilikuwa Chama Cha Mapinduzi na sasa ni CCM tu (CCM haina elements za Mapinduzi chanya yoyote). Kuna siku tutaamka, Watanzania wamekataa kunyanyaswa na kudanganywa.

Nawauliza ndugu zangu, ikiwa Slaa atashindwa hamdhani kuna watu watalia? Hakuna watu watakaorudi CCM na kumwacha Slaa na Mbowe? haitatokea?? Basi ukiona mambo kama ya Nakaaya yanatokea basi ujue ukombozi ndo waja huo. Ni wakati wa mafuta kujitenga na maji. Watakaokebehi nilichosema wafanye hivyo sasa, watakaonikosoa basi wanikosoe kwa hoja. Msinung'unike mioyoni mwenu kwa kuwa muda wa mapambano umekaribia sana.

Naomba kuwasilisha.
 
Ni tukio la kusikitisha lakini ni muhimu sana. Huwezi kutegemea mavuno mazuri kama shamba limejaa magugu. Huyo hakuwa mwanamapinduzi na kuondoka kwake kunatakiwa kuwa faraja kwa wapinganaji. Ni heri kuwa na jeshi dogo lenye wapiganaji ambao wanapigana kutoka ndani ya mioyo yao kuliko kuwa na watu wakibao wanasubiri kugombania mali za mateka wa vita. Nakaaya amejigundua kuwa hana ujasiri wa kiana mapinduzi. Ngoja aende mapema ili shamba liendelee kustawi.

Mkuu kama ulivyosema. Unaweza kukuta alikuwa anawabania vijana wa ukweli wenye hoja za kimapinduzi kuonekana. Kumbuka ameingia kwenye siasa akiwa na jina kama mwanamuziki. Inaweza kuwa alipoingia aliwazibia sana vijana wengine
 
Brainless chicken!


wakuuu ze nyetiz ni kuwa ningeshangaa sana kama nakaaya angebaki CHADEMA....kwani hata alipohamia CHADEMA alifanya hivyo kwa hasira tu..baada ya kuwa sugar daddy wake EDWARD LOWASSA alipoachishwa uwaziri mkuu......sio siri na kila mtu anajuwa mahusiano ya nakaaya na lowassa [haitakuwa ajabu pia kuwa wamepasiana na JK]...kwahiyo tukio la leo ni la wapenzi waliomaliza tofauti zao...Amerudi kwenye chama cha bwana yake............tuendelee kukata issues!!!
 
Unaangalia vingi, lakini akili ya mtu ni zaidi. Kwa mfano mtu kwenye avatar yako huwezi kusema ana busara hata kidogo!

Siwezi kusema mengi juu yako kwa kuwa baadhi ya wanajamvi wamenisaidia. Hata hivyo maoni yako yaonesha ukuuu wa uumbaji. Kwamba dunia na hata JF ni kama kokoro. Lazima litakomba na vitu vingine zaidi ya samaki.
 
Who the hell is she anyways? Hana faida nasi aende tu kila heri wasalimie wale waliobado wamelala usingizi pono pamoja na wewe. Lakini sisi tunasema ukombozi umetufikia kwani tunaota ndoto na kuona maono mungu atupe nini kama si raha ya milele
 
Wanasiasa wananiacha hoi sana! Kule JKT ana vyuoni unapomaliza mkataba wako huwa kuna clearance form! unajaza na kurejesha mali zao unajitaka. Sasa wanasiasa wanarudisha kadi za CCM ama CUF wanapohamia CHADEMA, kwa viongozi wa CHADEMA! ama kinyume chake, kwanini NA-KAYA asingerudisha kadi yake ya CHADEMA kwa wale waliompa na akaenda CCM kupewa mpya! Mchungaji nakosa jibu!!

Its too illogical to make sense!

Kadi ya CHADEMA unawapa CCM lol!

Nakaaya kura yako kwa Dr Slaa!
 
Siwezi kusema mengi juu yako kwa kuwa baadhi ya wanajamvi wamenisaidia. Hata hivyo maoni yako yaonesha ukuuu wa uumbaji. Kwamba dunia na hata JF ni kama kokoro. Lazima litakomba na vitu vingine zaidi ya samaki.


Ni kweli. Umeona wapi nyani akimsaidia chui kutoka mtegoni? Mnafanana kwa vyote.
The fact remain; the lady is intelligent and wise.
 
Hongera Nakaaya , ni uamuzi wako binafsi iwe kwa manufaa yako or kwa kufuata sera za chama . nilikuona Jasiri sana kwa kijana kama wewe ambaye ni msanii mwenye kuhitaji msaada wote toka kwa walio shika mpini wa sanaa za burudani na kuamua kuhamia chama cha upinzani. nikajiuliza je , huwezi baniwa , haswa ukizingatia baba yao Ruge ndio mpambe mkubwa?
Wote tukielewa huwezi fanikia kama hujaenda CCM (Kama Mh Makamba alivyo sema) , natumai ni uamuzi wako wa kuona mbali ukahmua kurudi ,nakutakia kila la kheri , huku nikiwa bado na mfuatilai mrembo mwingine ambaye yuko kwnye sanaa ya utangazaji akionyesha hisia zake na chaguo lake kubwa kwa chama cha upinzani nayeni Joyce Kyria.
 
Ni kweli. Umeona wapi nyani akimsaidia chui kutoka mtegoni? Mnafanana kwa vyote.
The fact remain; the lady is intelligent and wise.

Na wewe ni intelligent kama yeye. Na labda ndo yeye au umefichwa kwenye bra yake.

Kwa hiyo?
 
Yes, CHADEMA si mtu ni watu, CHADEMA hakuna pesa kuna sera - Wababaishaji hawana maisha CHADEMA - hongera bi mkubwa kugundua hayo mapemaa - Once again i congraturate you MISS POLITICIAN for going back to where you belong.
 
Na wewe ni intelligent kama yeye. Na labda ndo yeye au umefichwa kwenye bra yake.

Kwa hiyo?

Haki ya nani aisee! Hutambui umuhimu wa huyu binti kwa jamii?! Naamini ndiyo maana mnapiga piga kelele tu kutwa nzima hapa bila points. Huyu binti anaweza infuence watu zaidi ya 1000 kubadili mwelekeo. Unaelewa lakini maana yangu? Uliza nikupe maelezo? Mwambie na mwenzako mlionaye dark city. Kama hamtaki, endeleeni na jamvi la style yenu
 
Yes, CHADEMA si mtu ni watu, CHADEMA hakuna pesa kuna sera - Wababaishaji hawana maisha CHADEMA - hongera bi mkubwa kugundua hayo mapemaa - Once again i congraturate you MISS POLITICIAN for going back to where you belong.

Wakuu sometimes we are overstating hizi habari, Nakaaya ni nani? Is she a politician too? Zaidi ya huo wimbo wa Mr. Politician can someone remind me ni upi mwingine amewahi kuutengeneza ukawa maarufu. I would be shocked if say Mr. Nice (Yes Mr. Nice) alikuwa CHADEMA akahamia CCM.

By the way bado hamjaigundua tu janja ya CCM, why only CHADEMA ndiyo inakuwa nuwz? kama ni suala lakuongeza wanachama wako wapi kutoka CUF, NRA, UDP?
 
Back
Top Bottom