Nakaaya Sumari amerudisha kadi ya Chadema jioni ya leo na kumkabidhi JK kwenye mkutano wake ulio fanyika leo mkoani Arusha, JK amempongeza sana kwa kitendo hicho na kumwambia karibu mama CCM ndicho chama pekee Tanzania.
Wahenga walisema, ndege wafananao huruka pamoja. Msishangae sana kuhusu Nakaaya na JK, hawa wanafanana, ingawa si kwa "daraja" moja.
Nyepesi/nyeti nilizozinyaka - katika safari yangu ndefu ya UCHOKONOZI - nimenyetishwa kwamba miaka kadhaa, Nakaaya, wakati akiwa mwajiriwa (cashier/teller) wa benki ya Standard Chartered, jijini Dar es Salaam, aliwahi kukumbwa na kashfa ya wizi wa pesa kadhaa wakati akiwa kazini. Habari za kuaminika (source withheld) zinadai kwamba wakati huo Nakaaya alikuwa anatumia jina lake la Glory/Gloria, lakini baada ya kukumbwa na kasha hiyo iliyomfikisha lupango (na kesi kuzimwa kiaina), aliacha kutumia jina hilo na kuanza kutumia hilo la nyumbani, Nakaaya.
Wenye data zaidi mnaombwa kufuatilia. Tunataka kujua ukweli wa madai haya.
Asanteni.
<(MCHOKONOZI)>
haki yanani JF kwa data mnanimaliza.
mimi leo niko na raha zangu tele, namtakia kila la heri Nakaaya kokote kule aendako
Wanaojiunga na CCM kipindi hiki, poleni sana, CCM iko mwishoni sana kuanguka hata kama hamna vyama vya upinzani, ni lazima CCM kuanguka, muda unaruhusu CCM kuanguka. CCM haina muda mrefu wa kuanguka.
Dalili ya CCM kuanguka ni pamoja kubeba watu kwenye magari tayari kupelekwa kwenye kampeni kama magunia, kukakataa kushiriki kwenye midahalo, kukataa kuumlizwa maswali wakati wa kampeni, rushwa kuongezeka sana.
Narudia kusema CCM imebakiza muda mfupi sana. Tusubiri, mimi ninaipigania nchi yangu.
Wakuu zangu ebu niulize kitu kimoja, Hawa watu wakitoka CCM kuingia Chadema wanaitwa ni watu wenye tamaa waliokosa Uongozi, lakini nachoshangaa CCM hiyo hiyo inapokea watu kutoka vyama vingine sijui hawa wako vipi?!. Hivi huyu binti hafikirii huko CCM anachukuliwa vipi ndani ya CCM?
Nashangaa sana kuona hii nayo imekuwa ni issue humu, mpaka watu wazima tunachukua muda wetu na kuijadili. This chick is an opportunist na sidhani kama alikuwa amefanya kitu chochote cha manufaa kwa Chadema kama chama na wanancho wa Arusha in general. Kwa hiyo mwache aende kwa MAFISADI.
I say GOOD RIDDANCE!!
Nakaaya Sumari amerudisha kadi ya Chadema jioni ya leo na kumkabidhi JK kwenye mkutano wake ulio fanyika leo mkoani Arusha, JK amempongeza sana kwa kitendo hicho na kumwambia karibu mama CCM ndicho chama pekee Tanzania.