Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Nakaaya amefanya kile ambacho yeye anakiona ni sahihi kwake kukifanya. Anajua sababu ya kufikia uamuzi huo.
Ila ni wazi kuwa heshima yake aliyokuwa nayo mbele ya vijana wenzake na hasa wapenzi wa muziki wake ya kuonekana ni moja kati ya wanaharakati itashuka kwani kwa hili wengi watamwona msaliti na mtu anayesema kile ambacho yeye mwenyewe hawezi kufanya. Uchaguzi ukiisha huenda ndo ukwa mwisho wa Nakaaya kwenye muziki kwani itamchukua muda sana kujenga "trust" tena kwa mashabiki wake.
 
Nakiri kuwa dada huyu ameniumiza mno.simjui binafsi ila kupitia wimbo wake.niliposikia yuko upinzani nilielewa na kufarijika na nilijenga imani kubwa kwake.
Dada nakaaya umeniliza machozi kama wewe ni mwanaharakati kweli,kitendo hicho ni usaliti kwa nafsi yako na wananchi.any way ungana na kina nape,bashe ,j.makamba,nk labda utatoa remix ya wimbo wako uubadilishe kidogo.vinginevyo,utabaki kukusuta daima
 
Nakaaya Sumari amerudisha kadi ya Chadema jioni ya leo na kumkabidhi JK kwenye mkutano wake ulio fanyika leo mkoani Arusha, JK amempongeza sana kwa kitendo hicho na kumwambia karibu mama CCM ndicho chama pekee Tanzania.

Wahenga walisema, ndege wafananao huruka pamoja. Msishangae sana kuhusu Nakaaya na JK, hawa wanafanana, ingawa si kwa "daraja" moja.

Nyepesi/nyeti nilizozinyaka - katika safari yangu ndefu ya UCHOKONOZI - nimenyetishwa kwamba miaka kadhaa, Nakaaya, wakati akiwa mwajiriwa (cashier/teller) wa benki ya Standard Chartered, jijini Dar es Salaam, aliwahi kukumbwa na kashfa ya wizi wa pesa kadhaa wakati akiwa kazini. Habari za kuaminika (source withheld) zinadai kwamba wakati huo Nakaaya alikuwa anatumia jina lake la Glory/Gloria, lakini baada ya kukumbwa na kasha hiyo iliyomfikisha lupango (na kesi kuzimwa kiaina), aliacha kutumia jina hilo na kuanza kutumia hilo la nyumbani, Nakaaya.

Wenye data zaidi mnaombwa kufuatilia. Tunataka kujua ukweli wa madai haya.

Asanteni.

<(MCHOKONOZI)>
 
haki yanani JF kwa data mnanimaliza.
mimi leo niko na raha zangu tele, namtakia kila la heri Nakaaya kokote kule aendako
 
Opportunist & kutafuta attention. Kwani ni lazima usubiri mpaka raisi aje ndiyo uhame chama?
 
haki yanani JF kwa data mnanimaliza.
mimi leo niko na raha zangu tele, namtakia kila la heri Nakaaya kokote kule aendako

Mhh,

Safari moja huanzisha nyingine.

Nadhani hii ingekuwa mada inayojitegemea. Lakini pia isuhusishwe na kuhama kwake CHADEMA kwani inaweza kuonekana kama watu wanamkomoa. Hilo bomu linaweza kuwekwa kapuni kwanza, kama ambavyo Shujaa Dr Slaa anavyoweka vitu vingine kiporo.

Kwa sasa tukubaliane kuwa Nakaaya kafanya uamuzi ulio bora kwake ila unaoweza ku-damage reputation yake kwenye jamii ambayo alijipambanua kama mpiganaji. Na kwa CHADEMA ni habari nzuri kwani shamba linazidi kusafishika ili siku moja kiwe ni chama cha watu wanaopigania kile wanachokiamini na siyo kile watakachopata baada ya mapambano!
 
Wakuu zangu ebu niulize kitu kimoja, Hawa watu wakitoka CCM kuingia Chadema wanaitwa ni watu wenye tamaa waliokosa Uongozi, lakini nachoshangaa CCM hiyo hiyo inapokea watu kutoka vyama vingine sijui hawa wako vipi?!. Hivi huyu binti hafikirii huko CCM anachukuliwa vipi ndani ya CCM?
 
...nadiriki kusema kuwa ni watanzania wachache sana wenye 'independent thinking'. wanaoamua mambo kwa utashi wao wenyewe bila kufuata mkumbo na kujali maslahi ya wengine. Kutokana na ubinafsi uliokithiri kwenye jamii, kila mmoja anaona ni sawa aki'cling' na system itakayomwezesha kutanua. Watu hao wapo mtaani, makazini, wanaweza kujipendekeza kwa bosi dhalimu ili afaidike. Ndio maana utakuta watu hawaelewi wala kusikia kuhusu kuuondoa utawala wa kidhalimu wa CCM, kwa sababu kwa namna moja au nyingine wanapata hata kwa kuomba kwa wale wanaoliibia taifa, bila kuelewa kuwa hao wanaowagawia wanatuibia sisi sote. Tuna shida na namna tunavyotoa elimu yetu, hatufundishi watu kuwa huru kwa mawazo na kimtazamo. Utakuta wengi wanashabikia vitu vya bure hata kama ni kwa kuuza uhuru wetu, ndio maana kwa Kikwete kwake kuomba ni moja ya sifa ya Rais wa nchi. Kwa hiyo siwashangai wasanii kama hawa, wapo kuangalia namna gani wanafaidika. Inasikitisha kutambua kuwa tuna tatizo kubwa katika jamii yetu.
 
Wanaojiunga na CCM kipindi hiki, poleni sana, CCM iko mwishoni sana kuanguka hata kama hamna vyama vya upinzani, ni lazima CCM kuanguka, muda unaruhusu CCM kuanguka. CCM haina muda mrefu wa kuanguka.

Dalili ya CCM kuanguka ni pamoja kubeba watu kwenye magari tayari kupelekwa kwenye kampeni kama magunia, kukakataa kushiriki kwenye midahalo, kukataa kuumlizwa maswali wakati wa kampeni, rushwa kuongezeka sana.

Narudia kusema CCM imebakiza muda mfupi sana. Tusubiri, mimi ninaipigania nchi yangu.

Fita ni fita muraaa tumia kira siraha kumuhangamiza adui na kupata ushindti. Ikibidi tumia hata tusipiki umtoboe macho!!!!

Nyie arm-chair generals ndiyo mtalipa gharama za kushindwa vita hivi.

Nakaaya karibu nyumbani mama,
pole,
kupotea njia ndiyo kujua unakokwenda
 
Wakuu zangu ebu niulize kitu kimoja, Hawa watu wakitoka CCM kuingia Chadema wanaitwa ni watu wenye tamaa waliokosa Uongozi, lakini nachoshangaa CCM hiyo hiyo inapokea watu kutoka vyama vingine sijui hawa wako vipi?!. Hivi huyu binti hafikirii huko CCM anachukuliwa vipi ndani ya CCM?

Huyu dada simfahamu akili yake ila ninaamini kuwa ana frustration fulani kutokana na kubinywa sehemu nyingi kwenye maisha yake. Baada ya kumpta mmarekani na kuamua kumnyima pera Mzee Minja wa pale kampuni ya bia, alijikuta anakosa mikataba yote inayohusiana na kampuni hiyo ya bia. Mmarekani wake akamdanganya kuwa atampa mkataba wa Sony ambao ulikuwa hewa. Kwa vile bwana Minja anaonekana kama ana konekshesni sana huko CCM (by inference), nadhani dada huyu aliingia Chadema akiwa na hasira dhidi ya Minja na vile vile akitegemea straight line programming ya kuwa mheshimiwa. Kukuta kuwa hata chadema inabidi atumie OOP kuupata uheshimiwa, halafu akapata ofa yoyote huko CCM kuwa anaweza kujumuika na akina Kamata, huenda ndiyo maana ameamua kujaribu bahati yake huko. Ikiharibika huenda akahamia CUF ua TLP. Mimi nampongeza kwa juhudi zake kujaribu kutafuta panapofaa zadi katika maisha yake.
 
Mami Kichuguu, hii habari yako sasa ndiyo imenifungua macho. Naweza kukubaliana nayo kwa asilimia kubwa saana kuwa ndiyo ukweli wenyewe. Huyu dada kaona mambo yamekwama na atakufa njaa.....

Juzi tulisikia maelezo kutoka kwa Prof. Baregu kuwa CCM inatumia Ujinga, Njaa na umasikini wa Watanzania ili kuwapata kwenye kura na huu ni mfano HAI kabisa wa ukandamizaji wa CCM. Kuna haja na huyu Mzee Minja kumulikwa mara Slaa akipanda jukwaani kwani watu kama yeye na hawa akina Ruge, Kusaga nk ndiyo kundi hilo hilo ambalo Mr Sugu anaimba kuwa Wanawala Wasanii....
 
Nashangaa sana kuona hii nayo imekuwa ni issue humu, mpaka watu wazima tunachukua muda wetu na kuijadili. This chick is an opportunist na sidhani kama alikuwa amefanya kitu chochote cha manufaa kwa Chadema kama chama na wanancho wa Arusha in general. Kwa hiyo mwache aende kwa MAFISADI.

I say GOOD RIDDANCE!!
 
Kweli kwa jinsi wanavyoonyesha huyu karubuniwa au ni wale wa kufuata mkumbo. Inawezekana amefanya hivyo ili naye apate kuingia kwenye team ya Kampeni kama wasanii wengine kwa tamaa ya fedha!
Hiyo lakini isiumize wapenda mabadiliko mana Nakaaya ni mtu mdogo sana, Chadema iliondokewa na viongozi wake kama Aman Kaborou ambao ni muhimu na hakikutetereka. Umebaki mwezi mmoja tu na sifa zake zitayoyoma pale CCM itakapoanguka!
Pia nadhani tunaweza kujaribu kuwa positive, mana kurudisha kadi sio kurudisha mapenzi. Nakaaya anaweza akawa amefanya hivyo kwa tamaa za fedha lakini siku ya kupiga kura huwa hatuonyeshi kazi za vyama. Ni dhahiri kabisa kuna wana CCM wengi tu watapiga kura kwa Chadema!
 
Kama alitegemea kuuza albums zake kupitia mgongo wa CHADEMA; KALIWA........RIGARWIDE RIMEMSHINDA SAKURU-RHOBI
 
Mkuu, mie nilikuwa Jandoni ati sasa haya ya Mtu Mzima vipi tena?

Sema ni watu wa makamo .......................
Nashangaa sana kuona hii nayo imekuwa ni issue humu, mpaka watu wazima tunachukua muda wetu na kuijadili. This chick is an opportunist na sidhani kama alikuwa amefanya kitu chochote cha manufaa kwa Chadema kama chama na wanancho wa Arusha in general. Kwa hiyo mwache aende kwa MAFISADI.

I say GOOD RIDDANCE!!

Kazi na dawa. Utani kidogooo... Miaka ya 80 niliona Wasukuma wakicheza ngoma zao na ikifika kipindi Ngosha wanafanya break na unasikia jamaa anapasua Kikohoo na mwingine anamjibu "Ulikolola, ulikolola, umila li Gofita" akiwa na maana "unakohoa, unakohoa, tumia Cofta"
 
Nakaaya Sumari amerudisha kadi ya Chadema jioni ya leo na kumkabidhi JK kwenye mkutano wake ulio fanyika leo mkoani Arusha, JK amempongeza sana kwa kitendo hicho na kumwambia karibu mama CCM ndicho chama pekee Tanzania.

The lady is entitled to her decision!
Lakini anatia huruma maana anakula matapishi yake!
Huyu mi namchukulia kama adui wa wanamageuzi, maana alihubiri kitu ambacho hata yeye binafsi hakiamini!
Hata ikitokea nikakutana nae nitamchunguza kuhakikisha kama hana pembe kichwani!
 
Wale wa kupokea "vipande thelathini" wapo wengi. Lakini hiyo ndiyo matokea ya chekecheke la CHADEMA. Kuna watu wanaamini ukiwa chama cha upinzani lazima na wewe uwe kiongozi. Kiongozi mzuri ni yule anayekubali kwanza kuongozwa na wengine kabla hawajamkabidhi dhamana mikononi mwake.
 
Back
Top Bottom