Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Helo Dr Nina tatizo.LA kutoka majipu kwenye kwapa tumboni maziwa mapajani ,nshatumia dawa nyingi kama antbiotic,antallegy lkn yanaenda yanarudi je nifanyeje ,Dr aliniambia damu yangu ina sukari.nyingi.
Kama damu yako ina sukari nyingi umechekiwa kisukari?Unapata tiba yoyote ya ugonjwa wa kisukari?
 
Sijaanza rasmi tiba lkn niliamua kuacha kutumia vitu vya sukari yamepungua lkn yanatoka moja moja
 
low sex drive kwa mwanamke nini solution,kukosa ham kabisa ya mapenzi
Hamu ya tendo la ndoa linahusisha vitu vingi kama uzalishaji wa homoni ya estrogen, nerve stimulation ya kwenye eneo la uke na vichocheo tofauti kwenye ubongo ambavyo vinasababisha muongezeko wa msukumo wa damu kwenye eneo hilo ambalo hupunguza muscle contraction kwenye uke na muongezeko wa vilainishi ambayo vinachochea ham.

Experience mbaya ya sexual activity inaweza kusababisha mtu asiweze kurelax na kuwa comfortable hatimae kutofurahia tendo zima kutokana na stress,uchovu n.k.Ili kufurahia tendo pande zote zinatakiwa ziwe tayari kimwili na kiakili kwaajili ya tendo hilo.

Matumizi ya baadhi ya dawa yanaweza kusababisha reduced libido kama SSRI(selective serotonin reuptake inhibitors) na baadhi ya betablockers.

Baadhi ya magonjwa yanaweza kusababisha mapungufu ya ham ya tendo kama kisukari,renal failure,kansa, magonjwa kwenye nervesystem n.k

Jaribu kuchunguza chanzo cha matatizo kabla kutafuta suluhisho.Kila la kheri
 
Doctor mie nina tatizo la kusikia kichefu chefu Wakt wa period pia mgogoro kuuma ili tatzo limeanza siku iz tu hosp nilienda nikaambiwa mirija ya uzazi imeziba na kwa sas nahitaji mtot sana doctor ni tiba gan ya mirija ya uzazi tofaut na operation nisaidie doctor ninahitaj san mtot NB.nimeolewa
Tiba sahihi ni hio uloshauriwa na daktari.Kila la kheri
 
Naomba unisaidie tiba ya kuzuia kutokwa na vijinyama(rectum) wakati wa haja kubwa (BAWASIRI).
Tumia scheriproct supp au ointment.Supp weka mara moja kwa siku kwenye sehem ya haja kubwa.

Ointment paka eneo la nje mara mbili kwa siku kwa muda wa wiki moja, endelea na tiba mpaka wiki moja baada ya kupata nafuu.

Kama hujapata suppositori unaweza kutumia ointment kuingiza sehem ya hajakubwa.
 
Doctor mimi tatizo lango ni presha ya kupanda ambayo imenipata baada ya kutumia vidonge vya kuongeza nguvu za kiume"CUPID"kabla ya hapo ckuwa na tatizo hilo.nimekwenda kupima hospitl majibu yametoka cna kisukari wala lehemu lakini moyo unanisumbua sanaPresha hupanda ghafla lakini hata dakika moja haifiki inarudi kua kawaida.ushauri wa doctor anasema ni hormones imbalance kwa sababu hivyo vidonge kazi yake ni kuboost hormones.umri wangu ni miaka 48.nisaidie tafadhali moyo unanitesa saana hata kuendesha gari nimeacha kwa kuogopa kupata ajali.masuala ya kitandani niko vizuri tu hata mara 3 kwa ucku mmoja ninaweza kufanya.
Hello,Sildenafil inaweza kusababisha presha ya kupanda kama athari ya dawa.Vilevile kuna baadhi ya watu ambao hupatwa na hali kama yako ya presha kupanda au maumivu kwenye moyo baada ya tendo.

Dawa hii inapaswa itumike kwa umakini kwatu wenye matatizo ya moyo hasa ambao walikuwa na preexisting cardiovascular problem(hyphertrophic cardiomyopathy).

Ni vyema ukaonane na specialist wa masuala ya moyo ili uchukuliwe EKG na vipimo vingine na upate tiba sahihi ya tatizo lako.
 
Je nifanyeje ss
Unatakiwa upatiwe tiba ya kisukari.Kuna aina mbili ya kisukari DIABETES TYPE 1 and 2.Ni muhimu ukijulikana una ipi ili kupata tiba sahihi.Wenye Diabetes type 1 hawana uzalishaji wa homoni ya insulin na wenye Diabetes type 2 wana uzalishaji wa insulin lakini yenye mapungufu au ya kiwango kidogo kutokana na sababu tofauti.Tiba zake ni tofauti vilevile.
 
Unatakiwa upatiwe tiba ya kisukari.Kuna aina mbili ya kisukari DIABETES TYPE 1 and 2.Ni muhimu ukijulikana una ipi ili kupata tiba sahihi.Wenye Diabetes type 1 hawana uzalishaji wa homoni ya insulin na wenye Diabetes type 2 wana uzalishaji wa insulin lakini yenye mapungufu au ya kiwango kidogo kutokana na sababu tofauti.Tiba zake ni tofauti vilevile.

Kwa hyo sukari inaweza Kuwait SBB ya majipu
 
Hizi dawa za mseto zimeandikwa day1 zimekaa 4, day2 zimekaa 4 na kuendelea lakini hosp. Wanasema unameza nne kwa mara moja, maana yake kwa siku 8, sijaelewa hapo doctor
Vidonge vinne kwanza,vidonge vinne baada ya masaa 8,ikisha vinne kila baada ya masaa 12 mpaka viishe.
 
Mr.George!, Hongera sn kwa kipaji cha ualimu,
Swali; KIFAFA ni nini
Inatibikaje
Umri gani upatwa na KIFAFA
Malyenge ni ugonjwa?
Nitashukuru.
 
Hello,Sildenafil inaweza kusababisha presha ya kupanda kama athari ya dawa.Vilevile kuna baadhi ya watu ambao hupatwa na hali kama yako ya presha kupanda au maumivu kwenye moyo baada ya tendo.Dawa hii inapaswa itumike kwa umakini kwatu wenye matatizo ya moyo hasa ambao walikuwa na preexisting cardiovascular problem(hyphertrophic cardiomyopathy).Ni vyema ukaonane na specialist wa masuala ya moyo ili uchukuliwe EKG na vipimo vingine na upate tiba sahihi ya tatizo lako.

Asante kwa ushauri, ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom