Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Leo nimekutana na ma-chief wa surgical wame-suspect itakuwa ni kyphosis baada ys kuisoma x-ray tena,so nimeshauriwa kupta physio therapy kuchua diclofenac na kumeza ibuprofen.Je,yaweza kusaidia zaidi...

Ndio zitakupunguzia maumivu na inflammation.Kila la kher.
 
hapo tumekwenda sawa mumie thanks.
inapendeza kuona mtandaoni tunaweka mijadala kama hii inatufanya tupate elimu ya kutosha kwa njia bora zaid

Sio faizafoxy na darasa lake, kila kukicha soma darasa darasa weeee, hivi ndo vitu kusoma
 
Nini madhara ya ultrasound Kwa mama mjamzito?

Hakuna vielelezo kuwa inaweza kuwa na athari kwa mama mjamzito.Hishauriwi kufanyika zaidi ya mara 2-3 kwasababu ilishaleta athari kwenye ubongo wa mnyama.
 
Naomba kujua ni tiba IPI nzuri kwa mtoto aliyeungua na maji ya moto Sana kwenye mguu wake. ( very deep Barning)
 
Naomba kujua dawa ya kutibu muwasho sehemu za siri
 
ivi nini athari ya P2 au postanor katika mfumo mzima wa uzazi wa mwanamke.., na je inashauriwa kutumika mara kwa mara au inakipindi chake?
 
ivi nini athari ya P2 au postanor katika mfumo mzima wa uzazi wa mwanamke.., na je inashauriwa kutumika mara kwa mara au inakipindi chake?
 
mke wangu kajifungua ana siku 18 sasa ila wiki iliyopita ametokewa na uvimbe kwenye ziwa LA kulia kwa ndani. nn tatizo na tiba yake pls georgeousmimi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu habari yako na wanajamii forum wenzangu
Mie nina tatizo linalonisumbua ni kelele kusikika sikioni mwangu.kama wale wadudu wanaolia usiku
 
AZT au ARV hufanyaje kazi mwilini? Na nn side effects zake?
Na je, kipi bora kutumia ARV au kutumia njia nyingine za kuimarisha kinga ya mwili?
 
Kike,muda mrefu, hautoi machicha na hauna harufu.
 
Naomba kufahamu hili tatizo ni nini na tiba yake, ninapokua kwenye jua mwili huwaashwa au mwili ukichemka mfano baada ya kukimbia linakuja ilo tatizo la kuwaashwa na vipele flani hivi ukivipasua vinatoa majii baada ya muda baada ya mwili kupoa vinaisha na ule muwasho unaisha. Msaada please!!

Msaada tafadhali
 
ivi nini athari ya P2 au postanor katika mfumo mzima wa uzazi wa mwanamke.., na je inashauriwa kutumika mara kwa mara au inakipindi chake?
Hellow Mrs. Rama Postinor 2 ni levonorgestrel(progestin hormone) ambayo tunayo mwilini.Kazi yake ni kuzuia kupevushwa(ovulation) kwa yai.

Kubadilisha usafirishwaji wa mbegu za kiume hatimae kuzuia kurutubishwa kwa yai au kubadilisha mfumo wa kizazi(uterus) hatimae kuzuia yai lilorutubishwa kuegeshwa hapo.

Kuna athari ambazo ukizipata unashauriwa umuone daktari papo hapo nazo ni:

Kutoka damu kwa wingi,mfumo wa hedhi kubadilika badilika au kupoteza hedhi,kuumwa na eneo la tumbo au ukipata cramps. Athari za kawaida ambazo unazoweza kuzipata kutokana na jinsi mwili wako unavyoipokea dawa ni maumivu ya kawaida ya tumbo na maumivu kwenye matiti.

Nyingine ni kizunguzungu, maumivu ya kichwa, kichefchef na kutapika.
 
mke wangu kajifungua ana siku 18 sasa ila wiki iliyopita ametokewa na uvimbe kwenye ziwa LA kulia kwa ndani. nn tatizo na tiba yake pls georgeousmimi
Hellow uyui kwetu,mkeo ana nyonyesha kama kawaida au anapata shida kunyonyesha?Ni vyema mkaenda hospitali akachekiwe uvimbe alokuwa nao,mara nyingi unahusishwa na kansa ya matiti.
 
Last edited by a moderator:
Kike,muda mrefu, hautoi machicha na hauna harufu.
Usitumie sabuni kali kunawia ukeni,Tumia maji safi na ni vyema ukitafuta sabuni yenye pH ya 3,5 na nguo zako za ndani ni vyema ukizifua na sabuni isiyo na harufu,hakikisha zinakauka vizuri na usivae nguo za ndani zinazobana sana.Jaribu hayo kwanza.
 
Mkuu habari yako na wanajamii forum wenzangu Mie nina tatizo linalonisumbua ni kelele kusikika sikioni mwangu.kama wale wadudu wanaolia usiku
Ni vyema ukienda kuchekiwa sikio na specialist mkuu nina wasiwasi una matatizo kwenye ngoma ya sikio.
 
Back
Top Bottom