Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Naomba kujua ni tiba IPI nzuri kwa mtoto aliyeungua na maji ya moto Sana kwenye mguu wake. ( very deep Barning)
Mkuu hosp ndio wanampatia tiba mtu aliyeungua,Ukipatwa na deep burning upasujani ni lazima ufanyike ili kujaribu kuliziba eneo liloungua,deep burning inasababisha layers zote za ngozi zinakuwa zimeungua.

Good burn dressing na usafi wa eneo hilo pia ni muhimu huwa inatumika sana sterile vaseline compress ilikuzuia dressings kushikana na ngozi,na pia unaweza kupatiwa antibiotics ili kuepuka infection.

Inachukua muda mpaka eneo kupona na haliwezi kupona kama upasuaji haujafanyika.
 
Usitumie sabuni kali kunawia ukeni,Tumia maji safi na ni vyema ukitafuta sabuni yenye pH ya 3,5 na nguo zako za ndani ni vyema ukizifua na sabuni isiyo na harufu,hakikisha zinakauka vizuri na usivae nguo za ndani zinazobana sana.Jaribu hayo kwanza.

Asante sna nami umenisaidia nilikuwa nasubiri jibu
Barikiwa sn
 
Hellow uyui kwetu,mkeo ana nyonyesha kama kawaida au anapata shida kunyonyesha?Ni vyema mkaenda hospitali akachekiwe uvimbe alokuwa nao,mara nyingi unahusishwa na kansa ya matiti.

ananyonyesha ila tatizo lilipotokea hanyonyeshi tena ziwa hilo lenye uvimbe
 
Last edited by a moderator:
ananyonyesha ila tatizo lilipotokea hanyonyeshi tena ziwa hilo lenye uvimbe
Ana inflammation kwenye ziwa,hii inaweza kutokana na kutonyonyesha kwa ziwa hilo na kusababisha maziwa kuchacha na vijidudu(bacteria) kutawala.

Kuvimba na eneo hilo kunaweza kusababishwa na vitu tofauti kimojawapo ni kwamba kuna sehem katika mfumo wa utengenezaji wa maziwa upo blocked, hali hii isipotibiwa inaweza kusababisha mkusanyiko wa usaha(jipu) kwenye tissues(breast abscess).

Ni muhimu kama hanyonyeshi ajaribu kulikamua hilo ziwa kila baada ya masaa mawili na hakutakiwa aache kunyonyesha kwa ziwa hilo, angeendelea kunonyesha ni njia mojawapo ya uponyaji, kizuizi pekee cha kuacha kunyonyesha ni kama angelikuwa na breast abscess iliyotunga usaha na usaha unatokea kwenye ziwa.

Ili kujichunguza kama ana usaha kwenye uvimbe ajaribu kukamua ziwa kwenye kipande cha pamba akiona kuna mchanganyiko wa usaha na maziwa ndio angepaswa aache kunyonyesha na kupatiwa anitbiotic cure.

Muhimu asiache kujichunguza hilo ziwa na kama huo uvimbe upo muda mrefu anapaswa aende hospitali akafanyie utafiti wa kina.
 
Usitumie sabuni kali kunawia ukeni,Tumia maji safi na ni vyema ukitafuta sabuni yenye pH ya 3,5 na nguo zako za ndani ni vyema ukizifua na sabuni isiyo na harufu,hakikisha zinakauka vizuri na usivae nguo za ndani zinazobana sana.Jaribu hayo kwanza.

Ahsante sana kwa ushauri. Bado naomba msaada zaidi wa kujua aina za sabuni ambazo hazitoi harufu. Na, je, sabuni zenye ph ya 3.5 ndio zipi? Sijaelewa kabisa hapa.

Ahsante.
 
Ahsante sana kwa ushauri. Bado naomba msaada zaidi wa kujua aina za sabuni ambazo hazitoi harufu. Na, je, sabuni zenye ph ya 3.5 ndio zipi? Sijaelewa kabisa hapa. Ahsante.
Rudi post nr. 391,ukurasa wa 20.
 
AZT au ARV hufanyaje kazi mwilini? Na nn side effects zake?
Na je, kipi bora kutumia ARV au kutumia njia nyingine za kuimarisha kinga ya mwili?
Hellow Sukari Yenu,
Swali lako ni zito,nitajaribu kufafanua kwa kina kadri niwezavyo.
hiv-virus-structure-anatomy-picture-reference.jpg
Hii ni picha ya HIV-virusi na envelopes zake.

Ili ufahamu kwa upana ARV zinavyofanya kazi unapaswa ujue kwanza HIV-virusi anajizalishaje(HIV -replication cycle).

HIV huathiri CD4-receptor bearing cells ambazo ni Th cells,monocytes,dendritic cells na microglia kupitia kwenye chemokine receptor(CCR5).CD4 molecule ndio eneo ambalo HIV glycoprotein envelope gp120 anajiungia nalo mwanzo ikisha kunakuwa na muunganiko wa viral envelope na cell membrane kupitia kwenye gp41 ikisha kunakuwa na replication ya viral DNA/RNA.

Dawa za ukimwi zilizopo zinaathiri replication stages tofauti za virusi na dhumuni ni kuzuia virusi asiendelee kuzaliana.

Dawa ambazo zinatumika kutibu ukimwi zimegawanyika katika makundi manne
  1. NUCLEOSIDE AND NUCLEOTIDE REVERSE TRANSCRIPTASE INHIBITORS(NRTIs):Nazo ni kama zidovudine,zalcitabine,didanosine,lamivudine,stavudine abacavir,emticitabine,tenofovir.Nitaongelea kwa upana zidovudine hii,inazuia enzyme reverse trancriptase kwenye viral replication cycle,inazuia kutengenezwa kwa DNA kutoka kwenye viral-RNA na ni chain-terminator.Jaribu kutathmini picha ya pili.Dawa hizi zinatumika kutibu waathirika wa HIV-2.Zidovudine ni analogue ya nucleoside thymidine ambayo ina hydroxyl group ilikuwa replaced na azido group.Hii azido group inatengeneza phosphodiesterase linkages na kuzuia kutengenezwa kwa DNA ya virusi.Athari yake kubwa ni Bone marrow suppression(kupungua kwa chembechembe nyeupe,nyekundu(anemia) za damu) na pia kichefchef,kutapika,uchovu na kujisikia kuumwa.Hizo athari nilizozitaja ni kawaida kupatikana kipindi cha mwanzo cha tiba na ni muhimu vipimo vya damu vya mara kwa mara vichukuliwe.Athari nyingine ni pancreatitis(inflammation kwenye pancreas),athari kwenye nerves na kuongezeka uzito.Matumizi ya muda mrefu ya dawa hizi yanaweza kusababisha lactic acidosis ambayo inaweza kupelekea multi-organ failure.
  2. NON-NUCLEOTIDE REVERSE TRANSCRIPTASE INHIBITORS:Nazo ni nevirapine na efavirenz.Hizi zinatumika pamoja na nucleoside analogues kama chaguo la kkwanza.Nazo ni non competetive reverse transcriptase inhibitors,zinazuia hio enzyme kwa kujinga kwenye enzyme catalytic site.Zinatumika kutibu waathirika wa HIV-1 RNA,haitibu waathirika wa HIV-2.Athari zake za kawaida ni upele,ndoto na matatizo kwenye kulala.
  3. PROTEASE INHIBITORS:Nazo ni nelfinavir,saquinavir,indinavir,ritonavir,lopinavir plus ritonavir,atazanavir,amprenavir.Hizi zina zuia enzyme inayoitwa protease ambayo inaact kwenye cleavage ya gag na gag-pol polyproteins ambazo ni muhimu kwa replication ya virus,dawa hii inatumika pamoja na nucleoside analogues.Athari zake ni gastrointestinal disturbance,kuongezeka kwa uzito na inaweza kusababisha insulin resistance na hatimae kisukari.
  4. FUSION INHIBITORS:Enfuvirtde ambayo inajulikana pia kama T-20 nazo inablock HIV kabla haijaingia kwenye mwili wa host ili kujiunga na gp41.Hii inatumika kama sindano.
  5. Dawa nyingineni Raltegravir(Integrase inhibitor),maraviroc na daltegravir.
Hakuna dawa zisizokuwa na athari mkuu.Muhimu ukipatiwa tiba uangalie kipi ni cha muhimu kutibu ugonjwa na kuongeza siku za kuishi na quality ya maisha au kujali kuhusu athari.Athari za dawa zinatibika vilevile.Dawa za ukimwi zinazuia virusi asiendelee kuzaliana na hatimae kuongeza quality ya maisha na muda wa kuishi.Lishe bora na afya kwa ujumla ni muhimu kwa mwanaadamu yoyote sio waathirika wa UKIMWI tu.Hata mtu ambaye hajaathirika kama hana lishe bora na ana afya dhoofu hatoishi maisha marefu.
hiv-virus-structure-anatomy-picture-reference.jpg
gr2.jpg
REP.png
 
Msaada tafadhali
Hello pazimanian devil,Una tatizo linaloitwa MILIARIA CRYSTALLINA.

Ni aina ya upele unaosababishwa na blockage kwenye sweatglands kwenye layer ya juu ya ngozi epidermis.Ngozi ina aina mbili ya sweat glands nazo ni eccrine na apocrine.

Eccrine ipo kwenye sehemu za wazi za mwili zisizo na vinyoleo vingi. Apocrine ipo kwenye maeneo yenye vinyoleo kama kichwani,kwenye makwapa na sehemu za siri.

Mwili unapopata joto autonome nervesystem inachochea Eccrine sweatglands kutengeneza jasho. Ambapo jasho linatoka kupitia kwenye sweatchannels na kupunguza joto la mwili.

Ukipata heat rash eccrine sweatglands inakuwa blocked ambapo baadala ya jasho kutoka nje ya ngozi linabaki chini ya ngozi na kusababisha inflammation.

Inasemekana bacteria aina ya stapylococcus epidermis anaweza kuchangia pia huyu bacteria tunae kwenye ngozi na hana madhara bali jasho likiongezeka nae anatengenza vitu vyenye mvutano na kusababisha blockage kwenye sweatglands.

Hauhitaji tiba ya kutibu ugonjwa huu unachoweza kufanya ni kuepuka joto na mvuke au uoge na maji baridi ukitoka mazoezini tu.Ni vyema pia ukikaa kwenye chumba cha air condition kwa masaa kadhaa ili kuupoza mwili.
 
Gorgeousmimi naomba uniambie nna tatizo gani. Koo linawasha kwa muda sasa hata nikinywa dawa za kikohozi no changes.

Nilifanya check up niambiwa choo kichafu,nikatumia dawa but again no changes. Nikapima kipimi cha ESR na kutumia dawa pia. No changes at all! Help me plse!
 
Ana inflammation kwenye ziwa,hii inaweza kutokana na kutonyonyesha kwa ziwa hilo na kusababisha maziwa kuchacha na vijidudu(bacteria) kutawala.Kuvimba na eneo hilo kunaweza kusababishwa na vitu tofauti kimojawapo ni kwamba kuna sehem katika mfumo wa utengenezaji wa maziwa upo blocked,hali hii isipotibiwa inaweza kusababisha mkusanyiko wa usaha(jipu) kwenye tissues(breast abscess).Ni muhimu kama hanyonyeshi ajaribu kulikamua hilo ziwa kila baada ya masaa mawili na hakutakiwa aache kunyonyesha kwa ziwa hilo,angeendelea kunonyesha ni njia mojawapo ya uponyaji,kizuizi pekee cha kuacha kunyonyesha ni kama angelikuwa na breast abscess iliyotunga usaha na usaha unatokea kwenye ziwa .Ili kujichunguza kama ana usaha kwenye uvimbe ajaribu kukamua ziwa kwenye kipande cha pamba akiona kuna mchanganyiko wa usaha na maziwa ndio angepaswa aache kunyonyesha na kupatiwa anitbiotic cure.Muhimu asiache kujichunguza hilo ziwa na kama huo uvimbe upo muda mrefu anapaswa aende hospitali akafanyie utafiti wa kina.

asante kaka ila kajifungua tar 14-5-2015 na tar 22 ndio maumivu na. uvimbe ukaanza
 
Gorgeousmimi naomba uniambie nna tatizo gani. Koo linawasha kwa muda sasa hata nikinywa dawa za kikohozi no changes. Nilifanya check up niambiwa choo kichafu,nikatumia dawa but again no changes. Nikapima kipimi cha ESR na kutumia dawa pia. No changes at all! Help me plse!
Koo linawasha tu au linaaambatana na kikohozi/kifua?Je sauti nayo ni kavu?
 
Linaambatana na kikohozi na makohozi mengi asubuhi nnapopiga mswaki. Sauti haijabadilika!
 
Linaambatana na kikohozi na makohozi mengi asubuhi nnapopiga mswaki. Sauti haijabadilika!
Unavuta sigara?Kama unavuta utakuwa na ugonjwa unaoitwa Chronic obstructive pulmonary disease.

Na kama kama huvuti nimekuweka katika mafungu matatu nayo ni aidha chronic tonsolitis, pharyngitis au GERD(Gastroesophageal reflux disease)
Pharyngitis inasababishwa na viral infection ambayo inaweza kuchochewa na inndoor climate (ukiondoa fungus na mabadiliko ya temperature).

Muwasho kwenye koo unaweza kuchochewa na allergens pia.Ni vyema ukijaribu dawa ya kutibu allergy (antihistamins) kwa muda wa wiki moja ili uone kama utapata nafuu yoyote.

Gastroesophageal reflux disease kama heartburn inaweza kupeleka vilevile chronic pharyngitis kwasababu gastric acid inachosha mucosa iliyopo shingoni.

Kutibu hili ni kwa Proton Pump Inhibitors,au Histamin [SUB]2-[/SUB]receptor antagonists,au antacids.

Tonsolitis inaweza kuwa chanzo kingine, kutibu hili ni kwa kuondoa tonsils kwa surgery.
 
Sivuti sigara! Nashukuru kwa ushauri,ntatafuta dawa nijaribu.
 
human papilloma virus , je ugonjwa huu unatibika , na je chanzo chake nini??
 
Nina mtoto ana umri wa miezi 4, anatatizo la kutopata haja kubwa. Toka tatizo hilo linampata ni siku mbili zimepita.

Nimekwenda hosptali wameniambia hana tatizo lolo, na mtoto hajachemka ana joto la kawaida, ila analialia sana. Tafadhali naomba msaada wako.
 
Nina mtoto ana umri wa miezi 4, anatatizo la kutopata haja kubwa. Toka tatizo hilo linampata ni siku mbili zimepita. Nimekwenda hosptali wameniambia hana tatizo lolo, na mtoto hajachemka ana joto la kawaida, ila analialia sana. Tafadhali naomba msaada wako.
Hello mtoto wa miezi minne anaweza kutumia prunes juice au mixture.Ikishindikana mpe 1-2ml duphalac kwa siku mchanganyie na maziwa kwa siku 3-4 asipokuwa na nafuu muongezee upto 6ml per day kwa muda wa wiki.
 
Back
Top Bottom