niliwahi kukopa, online app zaidi ya 5 mwanzo nikarudisha fresh kwa wakati nakopa huku nalipa huku mpaka wakanipandishia dau 200k, nilipokopa hikokiwango ndipo nikagundua kuwa nilikuwa napigwa riba kubwa bado service charge yaani nilipiga mahesabu nikaona hawawapuuzi ntawatajirisha,
nikakopa 200k waka nipatia kama 180k, sikupanga kutolipa ila mambo yangu yalienda kombo nikaona liwalo na liwe nikafuta app zote, call zao nikijua tu ni wao nakata afu sipokei tena, cha ajabu sijui enzi hizo walikuwa hawajaanza hizi mbinu za kuzalilisha watu mtandaoni maana walikuwa wanawapigia wadhamini wawili tu niliowaweka ambao ni madogo zangu,
nikawapanga madogo wawaambie hawanijui wala hawanitambui hivyo waache usumbufu afu na mi line nikaizima kama mwezi hivi ndo ikawa goodbye nikasepa na kibunda.
NB. Sijisifu kuwadhulumu ila nilipofanya mahesabu nikaona hawa jamaa katika marejesho wamenipiga mno hivyo sikufeel guilty kuwapiga namimi marambili yake tena bila kuzalilishwa kwa contact list.
Ukipata mwanya wa kumuumiza muumizaji kama hawa kausha damu waumize kweli usiwaonee huruma.