Nakiri kwamba naendelea kujifunza siasa za Tanzania

Nakubaliana kabisa na wewe kabisa, mchango wa Oscar Kambona kwa hili taifa ni mkubwa mno, tena mkubwa sana. Nadhani hakustahili kufanyiwa vile na kina Mzee Nyerere. Nadhani njia sahihi ilikuwa kumuweka pembeni kuliko kumchafua vile mtu aluetoa mchango mkubwa kwa taifa:​
  1. Kambona alivyoingia TANU ndani ya mwaka mmoja alikusanya wanachama 10000.​
  2. Ndiye aliyeunda mifumo ya usalama hapa nchini akishauri kwamba vijana wa TYL ndiyo waingizwe kwenye idara mpya ya usalama wa taifa. Yeye ndiye aliyeenda kwa waisraeli ili watoe mafunzo kwa watanzania.​
  3. Ndiye aliyezima uasi wa kijeshi wa KAR mwaka 1964 wakati Mzee Nyerere na Rashidi Kawawa wakiwa wamefichwa. Angekuwa ni mtu mbaya basi baadhi ya wanajeshi walipomwambia ajitangaze kuwa Raisi alikataa mzee wa watu.​
  4. Kambona ndiye ARCHITECH wa FOREIGN POLICY ya Tanzania, alichokuwa anakizungumza Kambona miaka ya 60's mwanzoni ndicho ambacho Mzee Nyerere alikuwa akikizungumza miaka yote ya utawala wake.​
Kambona was forced into the Dark-Side. Mambo mabaya aliyofanyiwa ndiyo yalipelekea Kambona aje kuwa na moyo mgumu vile. Mzee Nyerere alimwogopa Kambona hadi mwisho kwasababu yeye ni mmoja kati ya watu waliokuwa wanamfahamu Nyerere kiundani (Hulka na Madhaifu yake), jambo ambalo Nyerere hakulipenda ukizingatia alishajitengenezea A CULT OF PERSONALITY.​
 
Wazungu husema hivi "When children grow up, they always realize a parent who was a problem"​
 
Kikubwa zaidi Kambona alipinga Chama kuonekana kama a symbol of pride huku kikienezwa nchi nzima hadi vijijini badala ya Serikali kujikita katika kueneza huduma muhimi kama Barabara, Hospitali na Mashule.

No wonder leo kuna maeneo mengi nchini watu wanaenda kwa viongozi wa chama kutatuliwa matatizo yao badala ya kufuata mifumo sahihi ya kiserikali! Rejea ziara za Makonda na watu kwenda kwake.

Kambona alisema tusianzishe vijiji vya ujamaa badala yake tujikite katika katika mfumo tuliokuwa nao before 1967. Ukifuatilia siasa ya ujamaa ndo hii imetengeneza watu wavivu wasiofikiri vizuri ambao kwao kila kitu ni Serikali.

Imetengeneza watu wajinga waliojaa Serikalini ambao hawatumii akili zao vizuri zaidi ya kuwaza madaraka , posho na vyeo tu.
 
Mbona John Malecela nimemtaja au hujasoma vizuri nilichokiandika ?

Kuhusu makabila ya HAYA, CHAGGA na NYAKYUSA haiwezi kuwa rahisi kwa watu wao kufika juu kwasababu ya STERETYPES and ANTI-TRIBAL CANARDS. Haya makabila yalishakuwa BLACK-BALLED tokea awamu ya kwanza, na watanzania wamekuwa na hiyo minong'ono kama sehemu ya falsafa yao kwamba haya makabila yana hulka ya kupendeleana. Jambo ambalo halina ukweli wowote ule kwasababu imethibitika tatizo ni mfumo wa kusimamia nafasi za ummah na siyo kabila.

Maana mpaka sasa imethibitika kwamba hata Mkwere na Msukuma wakiingia kama hakuna mifumo imara ya usimamizi wa taasisi za ummah basi lazima upendeleo utaonekana. Hivyo HAYA, CHAGGA na NYAKYUSA ni kuonesha mfumo wa Ubaguzi ambavyo uko hapa nchini na unakubalika. Alipoinga Raisi Magufuli yakaonekana yaleyale dhidi ya WASUKUMA, na hata akaingia Raisi MHEHE yataonekana yaleyale dhidi ya WANYALUKOLO kama ilivyokuwa kipindi Mzee Philemon Luhanjo ni Katibu Mkuu Kiongozi (KMK).

Nakumbuka mwaka 2015, Ridhiwani Kikwete, mtoto wa Raisi wa wakati huo aliwahi kunukuliwa wazi akisema kwa kujivuna kabisa kwamba "Raisi wa Tanzania hawezi kutoka Kaskazini". Hili alilolisema hakukemewa na mtu, ila alitudhihirishia wengi kwamba hizo ndizo kauli ambazo zinazungumzwa pale wakubwa zake pale magogoni.

Kuhusu Mzee Nyerere na Sokione nadhanu umefanya kitu kiitwacho (CHERRY PICKING HISTORY). Mwishoni kabisa Mzee Nyerere hawakuelewana kabisa na Moringe Sokoine. Huwa nashangaa watanzania wanapoamini kwamba hata kifo chenye utata cha Sokoione kilitokea kwa bahati mbaya, ilhali waandishi nguli kama Mzee Ndimara Tegambagwe waliandika vizuri kuhusu kifo cha Sokione mwaka 1992, kwenye kazi yake iitwayo "WHO TELLS THE THRUTH IN TANZANIA ?" ambapo alizungumzia taarifa nyingi zilizozunguka kifo cha Sokione hadi mtu unabaki kushangaa tu.

Mwisho kabisa, Sokione alionekana kupinga baadhi ya sera za Nyerere wazi kabisa jambo ambalo lilimkera mno Mzee Nyerere kwasababu alikuwa hapendi kukosolewa. Mfano, kwenda BoT kumtishia Gavana Charles Nyirabu atoe fedha za kutibu mlipuko wa magonjwa ya mifugo la sivyo anamfukuza kazi. AU kwenye kampeni ya uhujumu uchumi iligusa hadi viongozi wakubwa wa Kanisa ambao ilisemekana walitumika kuwafichia baadhi ya viongozi pesa, Sokione akatishia kuwakamata maaskofu.

Mzee Sokione was a Hard-Worker but also an Erratic Maverick, kuna baadhi ya mambo alikuwa anafanya ni kinyume na utaratibu na ilibidi Mzee Nyerere amuite kumfunga Speed-Governor. Alipoenda Msumbiji kwa Samora Macheli, Nyerere alilalamika kwamba Waziri Mkuu wake anamsumbua, na kuulizwa na Samora kwanini asimfukuze ? Akajibu akimfukuza italeta matatizo kwasababu watu wanamkubali. Ukweli ni kwamba hata alipoondoka mwaka 1980 hawakuwa kwenye Good-Terms, japo aliamua kumrudisha mwaka 1983 kwasababu mambo yalikuwa yameanza kuwa magumu sana ndani ya utawala wa Nyerere.

Namalizia kwa kukubaliana na wewe kwamba, mambo mengine huwezi kuzuia yasiyokee ila unaweza kuyatawala(One cannot stop crisis but Manage It), hivyo nadhani ndiyo muhimu viongozi wetu wa Tanzania kufahamu.​
 
Nyerere aliondoa ubaguzi, wa kidini na kikabila, Ndio maana Mbowe alisoma Kagera, Lowasa alisoma Tabora , weusi walipata nafasi kwenye Shule za wahindi , Shule za wakatoliki au tuseme za kidini zilitaifishwa ili kuwezesha dini zingine wapare fursa
Anyway tumsamehe tu Nyerere lakini yeye ni chanzo cha Matatizo mengi Nchi hii.

Bahati mbaya ccm wameyakumbatia.
 
Pia JPM alijitambulisha kama Msukuma, kabila kubwa kuliko yote nchini, na halina utamaduni wa kubebana. Hatuoni kwamba huo mfumo wa kuogopa makabila makubwa unekufa automatic.
Mbona kulikuwa na Anti-Sukuma Sentiments through-out utawala wake, au ulikuwa huzioni ?

Nachelea kusema kwamba, WE CANNOT OUTLIVE TRIBALISM, na kusema kwamba makabila fulani yanapendeleana nadhani inaweza ukawa ni ukweli nusu. Nasema hivi kwasababu imethibitika kwamba watanzania wengi wakipata nafasi, hata awe anatokea kabila dogo ni lazima atavutia kwake na kupendelea baadhi ya watu. Kama siyo upendeleo wa kikabila basi upendeleo wa kidini.

Hapa tunafikia kwenye HITIMISHO kwamba tatizo siyo UKABILA peke yake, bali MIFUMO yetu ya nchi inayosimamia nafasi za umma haifanyi kazi. Katika nchi ambayo iliwahi kuwa na mvutano mkubwa wa kikabila (Ethnic Tensions), basi Singapore ilikuwa ni hatari. Ile nchi ina makabila makubwa mno na yenye nguvu sana (Ethnic Chinese, Indians and Malays). Wachina ndiyo wengi ambao ni zaidi ya asilimia 50%, jambalo mara ya kwanza lilizua hisia kwamba wao ndiyo watawala.

Ikafika kipindi polisi mwenye asili ya kichini akimkamata mhalifu wa mwenye asili ya kihindi inaonekana kuna uonevu. Hata Malays nao ambao ni waislamu walilamika hivyo-hivyo. Mwishoni Waziri Mkuu Lee-Kuan-Yew akafahamu kwamba tatizo siyo KABILA bali MFUMO, hivyo waliunda MFUMO mpya ambao ulihakikisha watu wanapata nafasi kutokana vigezo (MERIT BASED SYSTEM), ndiyo maana Singapore imefika hapa leo.

Bila MFUMO imara, hata Malaika akiwekwa awe Raisi anaweza akalevwa na mvinyo wa madaraka.​
 
Nakubaliana na wewe 100%. Tungepata watu kama wewe 100 ndani ya CCM, nchii ingesonga mbele. Viongozi wanafikiria matumbo yao kuliko masilahi ya nchi. Wanasahau kuwa binadamu atapita ila nchi itabaki.
Yu wapi Nyerere, Karume, Mkapa, magufuri Lowasa (to mention few). Wako wapi waliokuwa wanasimama Dar wanakohoa nchi nzima inatetemeka, walikuwa na ulinzi wa kutisha, waliokuwa na Mali za Kila aina.
Tunapomzika E.Lowasa tujifunze kuwa Dunia hii ni ya kupita. Usimtendee mwenzako usivyopenda kutendewa naye.
Brief summary yako izingatiwe na CCM wanaosema wanaipenda Tanzania, kumbe wanajitafutia matumbo yao na watoto wao na wajukuu wao. Wanasahau kuwa vyote hivyo wataviacha na Tanzania itabaki. Wanaangalia hatima ya familia zao na chama Chao, badala ya hatima ya nchi.
Mwisho siyo kweli kwamba unaendelea kujifunza siasa za nchi hii, Bali wewe ni mwalimu wa siasa za nchi hii. And Old is gold.
 
Mfumo imara nakuunga mkono. Na Lee-Kuan-Yew mwenyewe alikuwa ni mlowezi wa kichina lakini wakati anaanza hizo harakati za kuseti mifumo imara duniani kote aliitwa Ddikteta.

Hata kwetu akiibuka mtu mwenye nia njema atapingwa kitaifa na kimataifa.

Nashauri system iweke ushindani huru. Kama ni mtanzania mwenye asili ya kiarabu, au kutoka kabila kubwa au nje ya Muislam/Catholic na anauwezo wa kutuvusha apewe nafasi. Asipewe kwa sababu ya ukabila au udini wake bali kwa sababu ya uwezo na ubora wake.

Ila powertrend duniani inaonyesha no vigumu sasa hivi mfumo mmoja kuendelea kutawala kwa muda mrefu kama ambavyo imekuwa rahisi moaka ya 70,80,90. Hivyo natofautiana na mtazamo wako kuwa mfumo tulionao 2023+ ukiendelea tutahitaji miaka mingi sana ili mabadiliko yatokee. Mimi naamini kuna siku katikati ya mfumo huu korofi kadili maarifa yanavyoongezeka utajiua wenyewe au kutokea nje yake na kutoa nafasi kwa fikra tofauti hata kama itatokea kwa kuchelewa kidogo.
 
Naunga mkono hoja yako,iko haja ya ccm kukaa pembeni je baada ya CCM kukaa pembeni mbadala ni nani?,maana uchaguzi umekaribia
 
Kambona alitoa ushirikiano kwa kina Hanga na wenzake kufanikisha mapinduzi ya Zanzibar na baadae muungano kuzaliwa,ila kilichofuata ni historia.....huenda kilichompata Kambona ni Karma pia.

JokaKuu zitto junior Nguruvi3
 
Nilishawahi kuandika, kwenye siasa ukitenda uovu hasa wa usaliti au mauaji. Kaa ukijua nawe utafanyiwa vivyohivyo na yule ambaye ulimuamini.

Kuna kijana mmoja ambaye ninamtabiria ndiye atakaye endeleza laana ya kisasi cha usaliti na mauaji kwa masalia. Yupo na kila siku anaonyesha uwepo wake
 
Hili jambo la WAISLAMU na WAKATOLIKI kupokezana MADARAKA linaumiza mno.

YAANI WAISLAMU NA WAKATOLIKI wameshafanya nafasi ya URAIS kuwa yao.
Labda ungesema Waislamu na Wakatoliki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…