Nakiri kwamba naendelea kujifunza siasa za Tanzania

Umeongea vizuri sana mkongwe. Ila umesahau jambo moja. Shida kwenye nchi yetu ilianza pale Nyerere alipokataa mawazo ya watu waliokuwa wanaona mbele kuliko yeye hasa Kambona.

Kwa jinsi Nyerere alivyomfanyia Kambona ndo laana ya hii nchi ilipoanzia. Kama hatujatubu ile dhambi, maendeleo ya kweli tuyasahau milele.

Kambona alipinga sana siasa za kukieneza zaidi Chama cha Mapindizi kuliko Serikali na huduma zake. Wakamuona mzandiki hafai, Kambona alipinga nchi kujiingiza kwenye siasa za ujamaa wakamuona chizi wakamfanya hadi akimbie nchi.

Ukitizama kwa makini mambo aliyopinga Kambona hadi kukorofishana na Nyerere ndo msingi na chanzo kikuu cha matatizo yanayotukabili hii leo.
Kambona alitaka tuwe kama Kenya. Hivi unadhani wakenya wote wanafurahia maisha ya kuwa wakenya??? Thubutu!!! Ukichunguza sana utagundua Nyerere alisaidia Sana kupunguza utofauti mkubwa wa kipato ambao uleta dhuruma kwa wasio na mali na wenye mali kuzidi kujilimbikizia mali!
 
Tatizo la nchi hii ni kuwa tumechelewa kwenye Elimu na Umasikini. Bila kupata suluhisho la hivyo demokrasia,katiba mpya nk ni bure. Hivi vitu ni muhimu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii vinginevyo itabaki kuwa mtaji wa watawala. Ukitaka kumtawala mtu mnyime elimu na hapo mbakizie umasikini. Uchambuzi huo ungejikita kwenye hayo mambo mawili yaani ujinga na umasikini ni shida kubwa.Lowasa alikuwa sahihi.
 
Watanzania wote wanafurahia maisha ya kuwa Watanzania??
 
Mbona John Malecela nimemtaja au hujasoma vizuri nilichokiandika ?

Kuhusu makabila ya HAYA, CHAGGA na NYAKYUSA haiwezi kuwa rahisi kwa watu wao kufika juu kwasababu ya STERETYPES and ANTI-TRIBAL CANARDS. Haya makabila yalishakuwa BLACK-BALLED tokea awamu ya kwanza, na watanzania wamekuwa na hiyo minong'ono kama sehemu ya falsafa yao kwamba haya makabila yana hulka ya kupendeleana. Jambo ambalo halina ukweli wowote ule kwasababu imethibitika tatizo ni mfumo wa kusimamia nafasi za ummah na siyo kabila.

Maana mpaka sasa imethibitika kwamba hata Mkwere na Msukuma wakiingia kama hakuna mifumo imara ya usimamizi wa taasisi za ummah basi lazima upendeleo utaonekana. Hivyo HAYA, CHAGGA na NYAKYUSA ni kuonesha mfumo wa Ubaguzi ambavyo uko hapa nchini na unakubalika. Alipoinga Raisi Magufuli yakaonekana yaleyale dhidi ya WASUKUMA, na hata akaingia Raisi MHEHE yataonekana yaleyale dhidi ya WANYALUKOLO kama ilivyokuwa kipindi Mzee Philemon Luhanjo ni Katibu Mkuu Kiongozi (KMK).

Nakumbuka mwaka 2015, Ridhiwani Kikwete, mtoto wa Raisi wa wakati huo aliwahi kunukuliwa wazi akisema kwa kujivuna kabisa kwamba "Raisi wa Tanzania hawezi kutoka Kaskazini". Hili alilolisema hakukemewa na mtu, ila alitudhihirishia wengi kwamba hizo ndizo kauli ambazo zinazungumzwa pale wakubwa zake pale magogoni.

Kuhusu Mzee Nyerere na Sokione nadhanu umefanya kitu kiitwacho (CHERRY PICKING HISTORY). Mwishoni kabisa Mzee Nyerere hawakuelewana kabisa na Moringe Sokoine. Huwa nashangaa watanzania wanapoamini kwamba hata kifo chenye utata cha Sokoione kilitokea kwa bahati mbaya, ilhali waandishi nguli kama Mzee Ndimara Tegambagwe waliandika vizuri kuhusu kifo cha Sokione mwaka 1992, kwenye kazi yake iitwayo "WHO TELLS THE THRUTH IN TANZANIA ?" ambapo alizungumzia taarifa nyingi zilizozunguka kifo cha Sokione hadi mtu unabaki kushangaa tu.

Mwisho kabisa, Sokione alionekana kupinga baadhi ya sera za Nyerere wazi kabisa jambo ambalo lilimkera mno Mzee Nyerere kwasababu alikuwa hapendi kukosolewa. Mfano, kwenda BoT kumtishia Gavana Charles Nyirabu atoe fedha za kutibu mlipuko wa magonjwa ya mifugo la sivyo anamfukuza kazi. AU kwenye kampeni ya uhujumu uchumi iligusa hadi viongozi wakubwa wa Kanisa ambao ilisemekana walitumika kuwafichia baadhi ya viongozi pesa, Sokione akatishia kuwakamata maaskofu.

Mzee Sokione was a Hard-Worker but also an Erratic Maverick, kuna baadhi ya mambo alikuwa anafanya ni kinyume na utaratibu na ilibidi Mzee Nyerere amuite kumfunga Speed-Governor. Alipoenda Msumbiji kwa Samora Macheli, Nyerere alilalamika kwamba Waziri Mkuu wake anamsumbua, na kuulizwa na Samora kwanini asimfukuze ? Akajibu akimfukuza italeta matatizo kwasababu watu wanamkubali. Ukweli ni kwamba hata alipoondoka mwaka 1980 hawakuwa kwenye Good-Terms, japo aliamua kumrudisha mwaka 1983 kwasababu mambo yalikuwa yameanza kuwa magumu sana ndani ya utawala wa Nyerere.

Namalizia kwa kukubaliana na wewe kwamba, mambo mengine huwezi kuzuia yasiyokee ila unaweza kuyatawala(One cannot stop crisis but Manage It), hivyo nadhani ndiyo muhimu viongozi wetu wa Tanzania kufahamu.​

Bila machafuko ama mapinduzi ya kijeshi, tutaendelea na mifumo hii hii mibovu.
 
Kila kunavyo kucha watanzania tunajua ukweli na chanzo cha umasikini nchini.

Ikiwa Mw Nyerere alikuwa na mtazamo wake kwa nia njema bahati mbaya mtazamo huohuo ndio umeleteleza shida nyingi nchini .

Ipo sababu watanzania kuleta mabadiliko ya kweli ya kimufumo na utawala ,tukianza na upatikanaji wa katiba mpya , mifumo ya chaguzi zetu.

Ni hatari sana kiongozi wa nchi,jimbo,kata,au mtaa kupatikana kwa mifukoni mwa watu au mtu mmoja kwa faida yake.

Viongozi hao hawawezi kuwa na masilahi na nchi ,badala yake watataka kurudisha faida kwa walio wapa nafasi na kuwasahau wananchi .

WATANZANIA TUSIJIVUNIE VYWAMA VYETU ,BALI TUWAPIME WANAO TAKA KUTUONGOZA NA TUJIRIDHISHE KUWA WANATUFAA
 
Poleni na misiba mikubwa ya kitaifa.

Nikiri kwamba kila siku naendelea kujifunza kuhusu siasa za taifa changa la Tanzania. Mambo makubwa ambayo mpaka sasa nikiri nimeshuhudia yakitokea bila chenga ni kwamba APANDACHO MTU NDICHO HUVUNA, na MWANADAMU HAWEZI KULINGANA NA MUNGU. Nitaelezea mtazamo wangu kwa ufupi:

Mosi, dhambi ya ubaguzi ambayo ilipandwa kwenye hili taifa dhidi ya makundi ya watu fulani itaendelea kulitafuna hili taifa endapo hatutakubali kubadilika. Ubaguzi ambao upo hapa nchini umekuwa wa kisera (Systemic Discrimination) na watu wameshakubaliana nao kwamba ndiyo utamaduni wetu wa kisiasa. Jambo hili siyo sawa hata kidogo, The Anti-Chagga, The Anti-Nyakyusa and The Anti-Haya Canards rooted at the founding cores of this nation state are very vile and devilish.

Ukifikiria kwa umakini na kuchambua historia ya nchi hii, utafahamu kwamba yale ambayo yaliogopwa kutokea endapo atapatikana Raisi Mchagga, Mnyakyusa au Mhaya yamefanywa hata alipokuwepo Raisi Mmakonde, Mzanzibar, Mkwele na Msukuma. Upendeleo (Nepotism and Cronyism) umeonekana, kama siyo katika minajili ya kikabila na kikanda, basi katika minajili ya kidini. Mifano iko mingi ya maraisi kuvutia kwao aidha kikabila, kikanda au kidini.

Sasa kwanini minong'ono na chuki za chini-chini ziendelee kuwa dhidi ya haya makabila matatu ilhali imethibitika kwamba kila mtu akikalia kiti cha uraisi, hata atoke kabila dogo, kama nchi haina mifumo imara ya kiutawala rushwa na upendeleo vitakuwepo tu. Halafu katabia kingine cha watanzania weusi kupenda kubagua watanzania wenye asili ya asia nako kametusababishia matatizo makubwa.

Huwa najiuliza maswali machache tu, hivi mtu kama Salim Ahmed Salim angekuwa Raisi mwaka 2005, leo hii Tanzania tungekuwepo hapa kweli ? Au mtu aina ya Prof Mark Mwandosya angekuwa Raisi leo hii Tanzania ingakuwa wapi ? Ila ni kwamba, hawa watu mbali na kufanya vyote kwa nchi, kiti cha Uraisi wasingeweza kuachiwa. Haya angalia leo hii tuko wapi.

Pili, hakuna baya utakalolifanya halafu lisikurudie. Hili ntalithibitisha kwa mifano hai kabisa. Marehemu Mzee Nyerere alifanya mazuri mengi, lakini mwishoni mwake alifanya makosa mengi mno ambayo aliyajutia na yalikuja kumrudi mwenyewe. Kuhusu Zanzibar alijutia sana hadi dakika za mwisho, na Mzee Dr Kitine alipoonana naye uwanja wa ndege wakati anaenda kutibiwa nchini Uingereza walizungumza sana kuhusu Zanzibar.

Naamini, kama mambo yangekuwa ni mazuri kuhusu Zanzibar asingeongelea hata kuhusu wao kuwa huru. Muungano haujarekebishwa, na umegeuka donda-ndugu (gangrene) ambalo linaitesa taifa hadi sasa, na nashukuru kwamba watanganyika kizazi kipya wameanza kuelewa kile ambacho G55, CHADEMA na TUME YA WARIOBA wamekuwa wakikizungumzia kuhusu muundo wa muungano. Tungeyamaliza haya mapema, nadhani leo hii taifa lisingekuwa na nyufa na chuki za chini-chini kama ilivyo leo.

Jingine ni suala la Uraisi mwaka 1995, ndani ya CCM na UPINZANI. Tunasema Mzee Nyerere, Fumbled the Bag. Alitumia nguvu yake kubwa ya kiushawishi kuwaumiza wanasiasa wengi kiasi cha kuwageuza moyo na kuwafundisha kwamba michezo michafu inalipa. PRECEDENT ya Mzee Nyerere kumuweka Raisi Mkapa kwa gharama yoyote ile, ilikuwa sahihi kwa muda mfupi (Tactical) lakini mbaya kwa muda mrefu (A Strategic Failure).

Tanzania ilikuwa ndiyo inajifunza kufanya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, 1990-1995 was an advent of multi-party democracy in Tanzania. It simply was a defining moment that could reverberate generations to come. Ilitakiwa CCM chini ya ushawishi wa Baba wa Taifa ioneshe mfano na kuongoza njia, ili kujenga msingi imara wa utawala hapa nchini. Kama watanzania hasahasa wale waliopo ndani ya CCM wangeona kwamba demokrasia inafanya kazi, na wale wenye vigezo ndiyo wanapita na siyo CLIENTISM ambayo Mzee Nyerere aliitumia binafsi naamini hata wale waovu wangeona iabu na CCM ingekuwa imejijengea utamaduni imara sana.

Ila wote tunafahamu baadhi ya wanasiasa akiwemo Mzee John Malecela, Horace Kolimba na Jakaya Kikwete walichofanywa. Huwa najiuliza swali hili: Hivi Jakaya angekuwa Raisi wakati Mzee Nyerere yupo hai angeweza kweli kuunda mtandao ambao wa kutafuta madaraka kwa namna yoyote ile, hata kuumiza watu wengi na kuuza roho yake kwa Ibilisi ili mradi awe Raisi ? Bado najiuliza. Huwa tunaulaumu MTANDAO kwa jinsi ulivyoharibu CCM na nchi, lakini huwa hatupendi kuzungumzia nini kilichopelekea mtandao kuundwa.

Siasa za ndani ya CCM za mwaka 1995 zilichangia sana MTANDAO kuundwa. Vijana ambao walinyimwa haki zao kihalali mwaka 1995 waliamua kujipanga kuhakikisha jambo kama lile halitokei tena mwaka 2005. Bahati mbaya sana walivyounda ule MTANDAO ndipo safari yao ya kumkabidhi IBILISI roho zao ilianza. Nachelea kusema, siyo vizuri kuwasema marehemu, lakini mpaka leo hii wanamtandao wote hawapo hai na maisha yao yalijaa mno uchungu na maumivu. Wamebakia Mzee Jakaya Kikwete na Rostam Aziz.

Wazungu husema, THERE'S NO HONOUR AMONG THIEVES. Punde tu baada ya kutimiza adhma yao ya kuupata Uraisi kwa gharama zozote zile, MTANDAO ulikumbwa na vita kubwa ya wenyewe kwa wenyewe (A Civil War) ambayo ililitesa taifa hili na kutufikisha hapa tulipo leo. Matatizo yote yale ambayo tunakumbwa nayo leo hii ya UFISADI, UKOSEKANAJI WA UMEME, UONGOZI DUNI, MAKUNDI NDANI YA CHAMA, SIASA ZA VISASI, MFUMUKO WA BEI na MATATIZO MENGINE YA KIUCHUMI yalichochewa sana na VITA YA WANA-MTANDAO ambayo ilianza mwaka 2006, ikachukua sura mpya mwaka 2008, na kuleta matokeo mabaya kwenye uchaguzi wa 2010 na mwishowe kufikia mwisho mbaya mwaka 2015 ambapo Tanzania Citizenry was a living collateral damage.

Namalizia hoja hii kwa kusema, Mzee Nyerere alimuweka Mkapa kwa hila, lakini akaanza kujuta na kutaka Mkapa asigombee mwaka 2000. Bahati mbaya wakapishana pakubwa na kuanza kufanyiana siasa za CLOAK & DAGGER ambazo hazikuisha vizuri. Raisi Mkapa alipishana na Mzee Nyerere, na hakuweza kuwa na uvumilivu mkubwa ambao Mzee Mwinyi alikuwa nao, akaonesha wazi-wazi kabisa kukerwa na Mzee Nyerere. Wasomi wengi ambao walikuwa wanamshauri Mzee Nyerere kuhusu kupinga sera za Ubinafsishaji walikiona cha MTEMA KUNI. Mzee Nyerere alilalamika wazi-wazi kwamba kwanini Mkapa anamfedhehesha huku akiwa hai.

Haikuishia hapo, mwaka 2015 kama ilivyokuwa mwaka 1995, Raisi Jakaya akafanya kilekile ambacho yeye mwenyewe alifanyiwa mwaka 1995. Alikata majina ya watu bila hata kuwasikiliza. Kulikuwa na wagombea wazuri mno mbali ya Mzee Lowassa (RIP), kina Prof Mwandosya, Dr Mahiga, Dr Mwele, Jaji Ramadhani, Dr Kitine nk. ambao hawakupewa nafasi. Raisi Mkapa akaamua kutumia karata yake ya ushawishi kuhakikisha kwamba Raisi Magufuli anapenya na Mzee Kikwete akaridhia baada ya kuona mtumbwi unazama na wana-MTANDAO wenzake wanaelekea kumshinda.

Mambo ni mengi mno, aliyewekwa na Raisi Mkapa na Raisi Kikwete akawageuka na kuanza kuwanyoosha, kama ambavyo Mkapa aligeuka kumnyoosha Nyerere aliyemuweka. Mengine tunamwachia Mungu. Ila naomba ujiulize hili swali:

Hivi wangetenda mema mwaka 1995 tungefika huku leo ? Amini, Amini nawaambia. Kama ilivyokuwa mwaka 1995 vijana kuunda MTANDAO, vivyo hivyo mwaka 2015 vijana wameunda MTANDAO mwingine, tofauti ni kwamba sasa hivi iko MITANDAO MINGI na MIZITO.

Tatu, na mwisho kabisa. Mwanadamu usijifanye MUNGU (Never Play GOD), kwasababu mbali na kuwa na uwezo wa kubadilisha mambo, hakuna mwanadamu dunia hii anayeweza kuzuia mabadiliko (No Man Can Ever Stop Changes). Kama tu mwanadamu hawezi kuzuia ukuaji wake binafsi, sembuse taasisi kubwa kama dola. Hivyo basi, hatuwezi kuzuia mabadiliko ila tunaweza kuyamudu (We Can't Stop Changes, But We Can Manage Them). And how do we manage changes? Through thorough preparations. Sisi kama kizazi kipya inabidi tujifunze na kuangalia ni wapi wazee walijikwaa.

Kama tukiendelea kuamini hizi falsafa ovu ambazo tulizikuta, basi hili taifa halitakuwa na amani kwa muda mrefu. Mbinu ambazo zilitumika kuwashughulikia watanzania milion 10-20 kipindi cha TANU/CHAMA KIMOJA haziwezi kuendelea kutumia kudhibiti taifa la kiutandawazi lenye watu zaidi ya milioni 60, ambao wanaingia na kutoka nje ya nchi kila uchwao.

Zile falsafa za kuamini kwamba watu wa UKANDA FULANI, KABILA FULANI, ASILI FULANI, JINSIA FULANI au DINI FULANI ndiyo wanaotakiwa sana kupewa nafasi nyeti kitaifa huku wengine wa kundi jingine wakibaguliwa wazi-wazi utadhani siyo WATANZANIA, kwamba ni wenye hulka ya wizi na kupendeleana ilhali tunasahau kwamba wako wengi na walitangulia kusoma tokea ukoloni. Ukweli mchungu ni kwamba matatizo yanayotokea hapa nchini hayajaletwa na CHAGGAS, NYAKYUSA AU HAYAS. Ni sawa na ule upumbavu wa kuamini kwamba WASUKUMU wa Raisi Magufuli ndiyo wameleta matatizo, jambo ambalo ukiliangalia kimapana halina ukweli wowote zaidi ya STIGMA and STEREOTYPE.

AU kuamini kwamba WAHINDI na WAARABU ndiyo chanzo cha umasikini wa mtu mweusi, ilhali tunasahau ukweli mchungu kwamba hao WAHINDI waliokimbia Tanzania miaka ya 60's na 70's kuelekea Uingereza na America Kaskazini bado wamefika huko na kuendelea kuwashinda hata hao wazungu na jehuri zao. Jiji la London lina wahindi wengi matajiri wa kutupwa ambao walitokea Tanganyika, Kenya na Uganda. Hili ni jambo linalofikirisha.

Ukienda Marekani, ukakutana na Diaspora wa Tanzania, wengi wao ni Wazenji, Wachagga, Wanyakyusa na Wahaya. Sasa unabaki kujiuliza, hii chuki ilitokea wapi, mbona hata huku kwa wazungu bado hawa watu wanafanikiwa mno. Mwisho unakuja kufahamu kwamba, kuna kitu hawa wenzetu walikifahamu muda mrefu, ambacho hata wengi wakikifahamu watafanikiwa tu.

MUHIMU KUKUMBUKA: Mwaka 2024 kutakuwa na uchaguzi mdogo, Mwaka 2025 uchaguzi mkuu. Mambo yatakayofanyika kipindi hiki yawe mema au mabaya, fahamu kwamba tutaishi nayo miaka mingi sana ijayo, kama ambayo tunaishi na yale ya mwaka 1995, 2005 na 2015. Niseme tu, The Domino Effects of 2015 will be profound and long-lasting. Kazi kwetu watanzania.....

APANDACHO MTU NDICHO ATAVUNA, huwezi panda Magugu ukavuna Mtama.

Niwatakie Usiku mwema....​
CCM ni laana
 
Tatizo la nchi hii ni kuwa tumechelewa kwenye Elimu na Umasikini. Bila kupata suluhisho la hivyo demokrasia,katiba mpya nk ni bure. Hivi vitu ni muhimu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii vinginevyo itabaki kuwa mtaji wa watawala. Ukitaka kumtawala mtu mnyime elimu na hapo mbakizie umasikini. Uchambuzi huo ungejikita kwenye hayo mambo mawili yaani ujinga na umasikini ni shida kubwa.Lowasa alikuwa sahihi.
Elimu inasingiziwa Sana

Tatizo kubwa la nchi hii ni NJAAAAAAA.

Watu wanaumizwa hata kusussa wanashindwa. Wakioewa vibia vya buku buku au elfu 20 wanagawa mpaka mikundu sembuse kura?
 
Ulichoongea ni kweli kiasi Fulani. Mfano, Maalimu Seifu aliongoza kwa kura, mwaka 1995 na kuonekana kuwa atashinda uchaguz. Nakumbuka, TV moja siikumbuki ilitangaza matokeo hayo, na ikawa inafikiriwa kuwa ni sawa kufanya hivyo. Lakin, TV hiyo ilifungiwa kwa muda na kutozwa faini ya shs 800,000.Na mpaka leo, matokeo ya upinzani kushinda hayatangazwi. Lakin pia, mitandao ya kishetani inaonekana ilianza, siku nyingi kwa kuwa, kifo cha Edward Sokoine pia kilikuwa cha utata na ilidhaniwa kusababishwa na mtandao wa watu fulani wakati huo. Aidha natofautiana na ww kuhusu makabila matatu, Chagga,Haya na Nyakwisa kunyimwa utawala kama uraisi hapa kwetu Tanzania,kwa hoja kuu zifuatazo: Moja, bado hajatokea mtu wa, kabila hizo mchapa kazi na mshindani na aliyepangwa na mwenyez Mungu.Kama akitokea na hasa kwenye CCM ni dhahiri atapata nafasi. Nasema hivyo kwa kuwa katika hiyo orodha uliyotoa,pia wasukuma walikuwepo. Lakin baada ya kutokea Magufuli akiwa, mchapa kazi na ukiwa mpango wa Mungu, akawa Rais na pia wasukuma wakatolewa kwenye orodha hiyo. Pili, Kama hoja hiyo ni kweli, mbona kuna makabila hayajapata, nafasi na haukuyataja kuwa yananyimwa nafasi ya urais.Mfano:Watu wa Kigoma, Wahehe,Wagogo, na nk.Je, hayo makabila matatu yana nini mpaka ukashawishika kuyataja kuwa yananyimwa nafasi.? Mwisho:Ni mefurahishwa, sana na hoja zako nzito na za kweli kasoro ya kwanza tu. Asante.
Mwandishi ametaja makabila matatu hayo ,kwa kurejerea matamshi ya Nyerere kwani yeye ndiye aliye weka [emoji359] kwa maneno na vitendo .
 
Umeongea vizuri sana mkongwe. Ila umesahau jambo moja. Shida kwenye nchi yetu ilianza pale Nyerere alipokataa mawazo ya watu waliokuwa wanaona mbele kuliko yeye hasa Kambona.

Kwa jinsi Nyerere alivyomfanyia Kambona ndo laana ya hii nchi ilipoanzia. Kama hatujatubu ile dhambi, maendeleo ya kweli tuyasahau milele.

Kambona alipinga sana siasa za kukieneza zaidi Chama cha Mapindizi kuliko Serikali na huduma zake. Wakamuona mzandiki hafai, Kambona alipinga nchi kujiingiza kwenye siasa za ujamaa wakamuona chizi wakamfanya hadi akimbie nchi.

Ukitizama kwa makini mambo aliyopinga Kambona hadi kukorofishana na Nyerere ndo msingi na chanzo kikuu cha matatizo yanayotukabili hii leo.
Nchi zilizofata siasa za ubepari ndio zimeendelea kama kenya, uganda, congo, zimbabwwe wapo kama Dubai matatizo kama maji umeme elimu njaa magonjwa waliyafuta sababu ya ubepari... Nyerere ndio katufikisha hapa...sawa great thinkers endeleeni na mjadala
 
Taifa ambalo limeshindwa kuweka strong foundation,basi haliwezi kuwa na taasisi imara bali uimara wake hutegemea maoni ya mtu binafsi kama msingi wa kila jambo.

Mwl.Nyerere alikuwa na tabia na hulka ya kuingia na matokeo yake kabla ya jambo kutoa,na jambo hili ndo wangine wamefuata mfumo huo huo.

Hii mada inahitaji utulivu wa akili mkubwa.
 
Poleni na misiba mikubwa ya kitaifa.

Nikiri kwamba kila siku naendelea kujifunza kuhusu siasa za taifa changa la Tanzania. Mambo makubwa ambayo mpaka sasa nikiri nimeshuhudia yakitokea bila chenga ni kwamba APANDACHO MTU NDICHO HUVUNA, na MWANADAMU HAWEZI KULINGANA NA MUNGU. Nitaelezea mtazamo wangu kwa ufupi:

Mosi, dhambi ya ubaguzi ambayo ilipandwa kwenye hili taifa dhidi ya makundi ya watu fulani itaendelea kulitafuna hili taifa endapo hatutakubali kubadilika. Ubaguzi ambao upo hapa nchini umekuwa wa kisera (Systemic Discrimination) na watu wameshakubaliana nao kwamba ndiyo utamaduni wetu wa kisiasa. Jambo hili siyo sawa hata kidogo, The Anti-Chagga, The Anti-Nyakyusa and The Anti-Haya Canards rooted at the founding cores of this nation state are very vile and devilish.

Ukifikiria kwa umakini na kuchambua historia ya nchi hii, utafahamu kwamba yale ambayo yaliogopwa kutokea endapo atapatikana Raisi Mchagga, Mnyakyusa au Mhaya yamefanywa hata alipokuwepo Raisi Mmakonde, Mzanzibar, Mkwele na Msukuma. Upendeleo (Nepotism and Cronyism) umeonekana, kama siyo katika minajili ya kikabila na kikanda, basi katika minajili ya kidini. Mifano iko mingi ya maraisi kuvutia kwao aidha kikabila, kikanda au kidini.

Sasa kwanini minong'ono na chuki za chini-chini ziendelee kuwa dhidi ya haya makabila matatu ilhali imethibitika kwamba kila mtu akikalia kiti cha uraisi, hata atoke kabila dogo, kama nchi haina mifumo imara ya kiutawala rushwa na upendeleo vitakuwepo tu. Halafu katabia kingine cha watanzania weusi kupenda kubagua watanzania wenye asili ya asia nako kametusababishia matatizo makubwa.

Huwa najiuliza maswali machache tu, hivi mtu kama Salim Ahmed Salim angekuwa Raisi mwaka 2005, leo hii Tanzania tungekuwepo hapa kweli ? Au mtu aina ya Prof Mark Mwandosya angekuwa Raisi leo hii Tanzania ingakuwa wapi ? Ila ni kwamba, hawa watu mbali na kufanya vyote kwa nchi, kiti cha Uraisi wasingeweza kuachiwa. Haya angalia leo hii tuko wapi.

Pili, hakuna baya utakalolifanya halafu lisikurudie. Hili ntalithibitisha kwa mifano hai kabisa. Marehemu Mzee Nyerere alifanya mazuri mengi, lakini mwishoni mwake alifanya makosa mengi mno ambayo aliyajutia na yalikuja kumrudi mwenyewe. Kuhusu Zanzibar alijutia sana hadi dakika za mwisho, na Mzee Dr Kitine alipoonana naye uwanja wa ndege wakati anaenda kutibiwa nchini Uingereza walizungumza sana kuhusu Zanzibar.

Naamini, kama mambo yangekuwa ni mazuri kuhusu Zanzibar asingeongelea hata kuhusu wao kuwa huru. Muungano haujarekebishwa, na umegeuka donda-ndugu (gangrene) ambalo linaitesa taifa hadi sasa, na nashukuru kwamba watanganyika kizazi kipya wameanza kuelewa kile ambacho G55, CHADEMA na TUME YA WARIOBA wamekuwa wakikizungumzia kuhusu muundo wa muungano. Tungeyamaliza haya mapema, nadhani leo hii taifa lisingekuwa na nyufa na chuki za chini-chini kama ilivyo leo.

Jingine ni suala la Uraisi mwaka 1995, ndani ya CCM na UPINZANI. Tunasema Mzee Nyerere, Fumbled the Bag. Alitumia nguvu yake kubwa ya kiushawishi kuwaumiza wanasiasa wengi kiasi cha kuwageuza moyo na kuwafundisha kwamba michezo michafu inalipa. PRECEDENT ya Mzee Nyerere kumuweka Raisi Mkapa kwa gharama yoyote ile, ilikuwa sahihi kwa muda mfupi (Tactical) lakini mbaya kwa muda mrefu (A Strategic Failure).

Tanzania ilikuwa ndiyo inajifunza kufanya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, 1990-1995 was an advent of multi-party democracy in Tanzania. It simply was a defining moment that could reverberate generations to come. Ilitakiwa CCM chini ya ushawishi wa Baba wa Taifa ioneshe mfano na kuongoza njia, ili kujenga msingi imara wa utawala hapa nchini. Kama watanzania hasahasa wale waliopo ndani ya CCM wangeona kwamba demokrasia inafanya kazi, na wale wenye vigezo ndiyo wanapita na siyo CLIENTISM ambayo Mzee Nyerere aliitumia binafsi naamini hata wale waovu wangeona iabu na CCM ingekuwa imejijengea utamaduni imara sana.

Ila wote tunafahamu baadhi ya wanasiasa akiwemo Mzee John Malecela, Horace Kolimba na Jakaya Kikwete walichofanywa. Huwa najiuliza swali hili: Hivi Jakaya angekuwa Raisi wakati Mzee Nyerere yupo hai angeweza kweli kuunda mtandao ambao wa kutafuta madaraka kwa namna yoyote ile, hata kuumiza watu wengi na kuuza roho yake kwa Ibilisi ili mradi awe Raisi ? Bado najiuliza. Huwa tunaulaumu MTANDAO kwa jinsi ulivyoharibu CCM na nchi, lakini huwa hatupendi kuzungumzia nini kilichopelekea mtandao kuundwa.

Siasa za ndani ya CCM za mwaka 1995 zilichangia sana MTANDAO kuundwa. Vijana ambao walinyimwa haki zao kihalali mwaka 1995 waliamua kujipanga kuhakikisha jambo kama lile halitokei tena mwaka 2005. Bahati mbaya sana walivyounda ule MTANDAO ndipo safari yao ya kumkabidhi IBILISI roho zao ilianza. Nachelea kusema, siyo vizuri kuwasema marehemu, lakini mpaka leo hii wanamtandao wote hawapo hai na maisha yao yalijaa mno uchungu na maumivu. Wamebakia Mzee Jakaya Kikwete na Rostam Aziz.

Wazungu husema, THERE'S NO HONOUR AMONG THIEVES. Punde tu baada ya kutimiza adhma yao ya kuupata Uraisi kwa gharama zozote zile, MTANDAO ulikumbwa na vita kubwa ya wenyewe kwa wenyewe (A Civil War) ambayo ililitesa taifa hili na kutufikisha hapa tulipo leo. Matatizo yote yale ambayo tunakumbwa nayo leo hii ya UFISADI, UKOSEKANAJI WA UMEME, UONGOZI DUNI, MAKUNDI NDANI YA CHAMA, SIASA ZA VISASI, MFUMUKO WA BEI na MATATIZO MENGINE YA KIUCHUMI yalichochewa sana na VITA YA WANA-MTANDAO ambayo ilianza mwaka 2006, ikachukua sura mpya mwaka 2008, na kuleta matokeo mabaya kwenye uchaguzi wa 2010 na mwishowe kufikia mwisho mbaya mwaka 2015 ambapo Tanzania Citizenry was a living collateral damage.

Namalizia hoja hii kwa kusema, Mzee Nyerere alimuweka Mkapa kwa hila, lakini akaanza kujuta na kutaka Mkapa asigombee mwaka 2000. Bahati mbaya wakapishana pakubwa na kuanza kufanyiana siasa za CLOAK & DAGGER ambazo hazikuisha vizuri. Raisi Mkapa alipishana na Mzee Nyerere, na hakuweza kuwa na uvumilivu mkubwa ambao Mzee Mwinyi alikuwa nao, akaonesha wazi-wazi kabisa kukerwa na Mzee Nyerere. Wasomi wengi ambao walikuwa wanamshauri Mzee Nyerere kuhusu kupinga sera za Ubinafsishaji walikiona cha MTEMA KUNI. Mzee Nyerere alilalamika wazi-wazi kwamba kwanini Mkapa anamfedhehesha huku akiwa hai.

Haikuishia hapo, mwaka 2015 kama ilivyokuwa mwaka 1995, Raisi Jakaya akafanya kilekile ambacho yeye mwenyewe alifanyiwa mwaka 1995. Alikata majina ya watu bila hata kuwasikiliza. Kulikuwa na wagombea wazuri mno mbali ya Mzee Lowassa (RIP), kina Prof Mwandosya, Dr Mahiga, Dr Mwele, Jaji Ramadhani, Dr Kitine nk. ambao hawakupewa nafasi. Raisi Mkapa akaamua kutumia karata yake ya ushawishi kuhakikisha kwamba Raisi Magufuli anapenya na Mzee Kikwete akaridhia baada ya kuona mtumbwi unazama na wana-MTANDAO wenzake wanaelekea kumshinda.

Mambo ni mengi mno, aliyewekwa na Raisi Mkapa na Raisi Kikwete akawageuka na kuanza kuwanyoosha, kama ambavyo Mkapa aligeuka kumnyoosha Nyerere aliyemuweka. Mengine tunamwachia Mungu. Ila naomba ujiulize hili swali:

Hivi wangetenda mema mwaka 1995 tungefika huku leo ? Amini, Amini nawaambia. Kama ilivyokuwa mwaka 1995 vijana kuunda MTANDAO, vivyo hivyo mwaka 2015 vijana wameunda MTANDAO mwingine, tofauti ni kwamba sasa hivi iko MITANDAO MINGI na MIZITO.

Tatu, na mwisho kabisa. Mwanadamu usijifanye MUNGU (Never Play GOD), kwasababu mbali na kuwa na uwezo wa kubadilisha mambo, hakuna mwanadamu dunia hii anayeweza kuzuia mabadiliko (No Man Can Ever Stop Changes). Kama tu mwanadamu hawezi kuzuia ukuaji wake binafsi, sembuse taasisi kubwa kama dola. Hivyo basi, hatuwezi kuzuia mabadiliko ila tunaweza kuyamudu (We Can't Stop Changes, But We Can Manage Them). And how do we manage changes? Through thorough preparations. Sisi kama kizazi kipya inabidi tujifunze na kuangalia ni wapi wazee walijikwaa.

Kama tukiendelea kuamini hizi falsafa ovu ambazo tulizikuta, basi hili taifa halitakuwa na amani kwa muda mrefu. Mbinu ambazo zilitumika kuwashughulikia watanzania milion 10-20 kipindi cha TANU/CHAMA KIMOJA haziwezi kuendelea kutumia kudhibiti taifa la kiutandawazi lenye watu zaidi ya milioni 60, ambao wanaingia na kutoka nje ya nchi kila uchwao.

Zile falsafa za kuamini kwamba watu wa UKANDA FULANI, KABILA FULANI, ASILI FULANI, JINSIA FULANI au DINI FULANI ndiyo wanaotakiwa sana kupewa nafasi nyeti kitaifa huku wengine wa kundi jingine wakibaguliwa wazi-wazi utadhani siyo WATANZANIA, kwamba ni wenye hulka ya wizi na kupendeleana ilhali tunasahau kwamba wako wengi na walitangulia kusoma tokea ukoloni. Ukweli mchungu ni kwamba matatizo yanayotokea hapa nchini hayajaletwa na CHAGGAS, NYAKYUSA AU HAYAS. Ni sawa na ule upumbavu wa kuamini kwamba WASUKUMU wa Raisi Magufuli ndiyo wameleta matatizo, jambo ambalo ukiliangalia kimapana halina ukweli wowote zaidi ya STIGMA and STEREOTYPE.

AU kuamini kwamba WAHINDI na WAARABU ndiyo chanzo cha umasikini wa mtu mweusi, ilhali tunasahau ukweli mchungu kwamba hao WAHINDI waliokimbia Tanzania miaka ya 60's na 70's kuelekea Uingereza na America Kaskazini bado wamefika huko na kuendelea kuwashinda hata hao wazungu na jehuri zao. Jiji la London lina wahindi wengi matajiri wa kutupwa ambao walitokea Tanganyika, Kenya na Uganda. Hili ni jambo linalofikirisha.

Ukienda Marekani, ukakutana na Diaspora wa Tanzania, wengi wao ni Wazenji, Wachagga, Wanyakyusa na Wahaya. Sasa unabaki kujiuliza, hii chuki ilitokea wapi, mbona hata huku kwa wazungu bado hawa watu wanafanikiwa mno. Mwisho unakuja kufahamu kwamba, kuna kitu hawa wenzetu walikifahamu muda mrefu, ambacho hata wengi wakikifahamu watafanikiwa tu.

MUHIMU KUKUMBUKA: Mwaka 2024 kutakuwa na uchaguzi mdogo, Mwaka 2025 uchaguzi mkuu. Mambo yatakayofanyika kipindi hiki yawe mema au mabaya, fahamu kwamba tutaishi nayo miaka mingi sana ijayo, kama ambayo tunaishi na yale ya mwaka 1995, 2005 na 2015. Niseme tu, The Domino Effects of 2015 will be profound and long-lasting. Kazi kwetu watanzania.....

APANDACHO MTU NDICHO ATAVUNA, huwezi panda Magugu ukavuna Mtama.

Niwatakie Usiku mwema....​
Mkuu Malcom kiaje?

Umeweka bandiko murua sana na umetumia haki yako ya kuelimika kuchambua hilo.

Hata mie juzi niliweka mada kuhusu "Kleptocracy" ambayo ni zao la hiyo mitandao mizito uloitaja.

Hayati Mwalimu alilia sana khasa aliposikia Mkapa RIP auza NBC ambayo ni marehemu Nsekela ndie alieiimarisha kuwa benki kubwa ya biashara nchini, lakini ile ilikuwa ni twasema " architect of his own downfall".

Lakini marehemu Mkapa nae alikuwa ashatekwa na moja ya mitandao hiyo na ndo hao (wanamitandao) walipojawa na hofu tukaanza kuwapoteza watu muhimu katika nchi hii kama mzee Kombe.

Twahitaji kuuma risasi au raisi wa 2025-2030 ahitaji kuuma risasi awezeshe kuwepo na kura ya maoni itayoridhia mabadiliko ya katiba.

Pili, aseme liwalo na liwe arudi kwenye mipango ya JPM kuhusu nchi hii na abomoe mitandao yote kwa kutumia (samahani kwa kusema hili) "Putin Style" au "Xi Jingping Style".

Hii mitindo waweza kuichanganya au kutumia mmojawapo kulingana na mahitaji yako.

Nasema iwe Putin Style kwa maana kwamba vyombo vyetu vya usalama bado sana na ni lazima vipewe nafasi virudi katika ile "level" inotakiwa ambayo itazuia mtu kama CDF kutoa kauli tata mikutanoni.

"Going forward" hio ndo njia sahihi kwani Putin aongoza zaidi ya raia milioni 147 na Jingping raia zaidi ya bilioni 1, seuse sisi Tanzania wenye raia milioni 60?
 
Umeongea vizuri sana mkongwe. Ila umesahau jambo moja. Shida kwenye nchi yetu ilianza pale Nyerere alipokataa mawazo ya watu waliokuwa wanaona mbele kuliko yeye hasa Kambona.

Kwa jinsi Nyerere alivyomfanyia Kambona ndo laana ya hii nchi ilipoanzia. Kama hatujatubu ile dhambi, maendeleo ya kweli tuyasahau milele.

Kambona alipinga sana siasa za kukieneza zaidi Chama cha Mapindizi kuliko Serikali na huduma zake. Wakamuona mzandiki hafai, Kambona alipinga nchi kujiingiza kwenye siasa za ujamaa wakamuona chizi wakamfanya hadi akimbie nchi.

Ukitizama kwa makini mambo aliyopinga Kambona hadi kukorofishana na Nyerere ndo msingi na chanzo kikuu cha matatizo yanayotukabili hii leo.
Sithani kama ujamaa pekee ndoyakulaumiwa nchi kutosonga mbele. Swali ni je? baada ya sisi kuingia kwenye ubepari mpaka sasa tumekuwa matajiri?
 
Poleni na misiba mikubwa ya kitaifa.

Nikiri kwamba kila siku naendelea kujifunza kuhusu siasa za taifa changa la Tanzania. Mambo makubwa ambayo mpaka sasa nikiri nimeshuhudia yakitokea bila chenga ni kwamba APANDACHO MTU NDICHO HUVUNA, na MWANADAMU HAWEZI KULINGANA NA MUNGU. Nitaelezea mtazamo wangu kwa ufupi:

Mosi, dhambi ya ubaguzi ambayo ilipandwa kwenye hili taifa dhidi ya makundi ya watu fulani itaendelea kulitafuna hili taifa endapo hatutakubali kubadilika. Ubaguzi ambao upo hapa nchini umekuwa wa kisera (Systemic Discrimination) na watu wameshakubaliana nao kwamba ndiyo utamaduni wetu wa kisiasa. Jambo hili siyo sawa hata kidogo, The Anti-Chagga, The Anti-Nyakyusa and The Anti-Haya Canards rooted at the founding cores of this nation state are very vile and devilish.

Ukifikiria kwa umakini na kuchambua historia ya nchi hii, utafahamu kwamba yale ambayo yaliogopwa kutokea endapo atapatikana Raisi Mchagga, Mnyakyusa au Mhaya yamefanywa hata alipokuwepo Raisi Mmakonde, Mzanzibar, Mkwele na Msukuma. Upendeleo (Nepotism and Cronyism) umeonekana, kama siyo katika minajili ya kikabila na kikanda, basi katika minajili ya kidini. Mifano iko mingi ya maraisi kuvutia kwao aidha kikabila, kikanda au kidini.

Sasa kwanini minong'ono na chuki za chini-chini ziendelee kuwa dhidi ya haya makabila matatu ilhali imethibitika kwamba kila mtu akikalia kiti cha uraisi, hata atoke kabila dogo, kama nchi haina mifumo imara ya kiutawala rushwa na upendeleo vitakuwepo tu. Halafu katabia kingine cha watanzania weusi kupenda kubagua watanzania wenye asili ya asia nako kametusababishia matatizo makubwa.

Huwa najiuliza maswali machache tu, hivi mtu kama Salim Ahmed Salim angekuwa Raisi mwaka 2005, leo hii Tanzania tungekuwepo hapa kweli ? Au mtu aina ya Prof Mark Mwandosya angekuwa Raisi leo hii Tanzania ingakuwa wapi ? Ila ni kwamba, hawa watu mbali na kufanya vyote kwa nchi, kiti cha Uraisi wasingeweza kuachiwa. Haya angalia leo hii tuko wapi.

Pili, hakuna baya utakalolifanya halafu lisikurudie. Hili ntalithibitisha kwa mifano hai kabisa. Marehemu Mzee Nyerere alifanya mazuri mengi, lakini mwishoni mwake alifanya makosa mengi mno ambayo aliyajutia na yalikuja kumrudi mwenyewe. Kuhusu Zanzibar alijutia sana hadi dakika za mwisho, na Mzee Dr Kitine alipoonana naye uwanja wa ndege wakati anaenda kutibiwa nchini Uingereza walizungumza sana kuhusu Zanzibar.

Naamini, kama mambo yangekuwa ni mazuri kuhusu Zanzibar asingeongelea hata kuhusu wao kuwa huru. Muungano haujarekebishwa, na umegeuka donda-ndugu (gangrene) ambalo linaitesa taifa hadi sasa, na nashukuru kwamba watanganyika kizazi kipya wameanza kuelewa kile ambacho G55, CHADEMA na TUME YA WARIOBA wamekuwa wakikizungumzia kuhusu muundo wa muungano. Tungeyamaliza haya mapema, nadhani leo hii taifa lisingekuwa na nyufa na chuki za chini-chini kama ilivyo leo.

Jingine ni suala la Uraisi mwaka 1995, ndani ya CCM na UPINZANI. Tunasema Mzee Nyerere, Fumbled the Bag. Alitumia nguvu yake kubwa ya kiushawishi kuwaumiza wanasiasa wengi kiasi cha kuwageuza moyo na kuwafundisha kwamba michezo michafu inalipa. PRECEDENT ya Mzee Nyerere kumuweka Raisi Mkapa kwa gharama yoyote ile, ilikuwa sahihi kwa muda mfupi (Tactical) lakini mbaya kwa muda mrefu (A Strategic Failure).

Tanzania ilikuwa ndiyo inajifunza kufanya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, 1990-1995 was an advent of multi-party democracy in Tanzania. It simply was a defining moment that could reverberate generations to come. Ilitakiwa CCM chini ya ushawishi wa Baba wa Taifa ioneshe mfano na kuongoza njia, ili kujenga msingi imara wa utawala hapa nchini. Kama watanzania hasahasa wale waliopo ndani ya CCM wangeona kwamba demokrasia inafanya kazi, na wale wenye vigezo ndiyo wanapita na siyo CLIENTISM ambayo Mzee Nyerere aliitumia binafsi naamini hata wale waovu wangeona iabu na CCM ingekuwa imejijengea utamaduni imara sana.

Ila wote tunafahamu baadhi ya wanasiasa akiwemo Mzee John Malecela, Horace Kolimba na Jakaya Kikwete walichofanywa. Huwa najiuliza swali hili: Hivi Jakaya angekuwa Raisi wakati Mzee Nyerere yupo hai angeweza kweli kuunda mtandao ambao wa kutafuta madaraka kwa namna yoyote ile, hata kuumiza watu wengi na kuuza roho yake kwa Ibilisi ili mradi awe Raisi ? Bado najiuliza. Huwa tunaulaumu MTANDAO kwa jinsi ulivyoharibu CCM na nchi, lakini huwa hatupendi kuzungumzia nini kilichopelekea mtandao kuundwa.

Siasa za ndani ya CCM za mwaka 1995 zilichangia sana MTANDAO kuundwa. Vijana ambao walinyimwa haki zao kihalali mwaka 1995 waliamua kujipanga kuhakikisha jambo kama lile halitokei tena mwaka 2005. Bahati mbaya sana walivyounda ule MTANDAO ndipo safari yao ya kumkabidhi IBILISI roho zao ilianza. Nachelea kusema, siyo vizuri kuwasema marehemu, lakini mpaka leo hii wanamtandao wote hawapo hai na maisha yao yalijaa mno uchungu na maumivu. Wamebakia Mzee Jakaya Kikwete na Rostam Aziz.

Wazungu husema, THERE'S NO HONOUR AMONG THIEVES. Punde tu baada ya kutimiza adhma yao ya kuupata Uraisi kwa gharama zozote zile, MTANDAO ulikumbwa na vita kubwa ya wenyewe kwa wenyewe (A Civil War) ambayo ililitesa taifa hili na kutufikisha hapa tulipo leo. Matatizo yote yale ambayo tunakumbwa nayo leo hii ya UFISADI, UKOSEKANAJI WA UMEME, UONGOZI DUNI, MAKUNDI NDANI YA CHAMA, SIASA ZA VISASI, MFUMUKO WA BEI na MATATIZO MENGINE YA KIUCHUMI yalichochewa sana na VITA YA WANA-MTANDAO ambayo ilianza mwaka 2006, ikachukua sura mpya mwaka 2008, na kuleta matokeo mabaya kwenye uchaguzi wa 2010 na mwishowe kufikia mwisho mbaya mwaka 2015 ambapo Tanzania Citizenry was a living collateral damage.

Namalizia hoja hii kwa kusema, Mzee Nyerere alimuweka Mkapa kwa hila, lakini akaanza kujuta na kutaka Mkapa asigombee mwaka 2000. Bahati mbaya wakapishana pakubwa na kuanza kufanyiana siasa za CLOAK & DAGGER ambazo hazikuisha vizuri. Raisi Mkapa alipishana na Mzee Nyerere, na hakuweza kuwa na uvumilivu mkubwa ambao Mzee Mwinyi alikuwa nao, akaonesha wazi-wazi kabisa kukerwa na Mzee Nyerere. Wasomi wengi ambao walikuwa wanamshauri Mzee Nyerere kuhusu kupinga sera za Ubinafsishaji walikiona cha MTEMA KUNI. Mzee Nyerere alilalamika wazi-wazi kwamba kwanini Mkapa anamfedhehesha huku akiwa hai.

Haikuishia hapo, mwaka 2015 kama ilivyokuwa mwaka 1995, Raisi Jakaya akafanya kilekile ambacho yeye mwenyewe alifanyiwa mwaka 1995. Alikata majina ya watu bila hata kuwasikiliza. Kulikuwa na wagombea wazuri mno mbali ya Mzee Lowassa (RIP), kina Prof Mwandosya, Dr Mahiga, Dr Mwele, Jaji Ramadhani, Dr Kitine nk. ambao hawakupewa nafasi. Raisi Mkapa akaamua kutumia karata yake ya ushawishi kuhakikisha kwamba Raisi Magufuli anapenya na Mzee Kikwete akaridhia baada ya kuona mtumbwi unazama na wana-MTANDAO wenzake wanaelekea kumshinda.

Mambo ni mengi mno, aliyewekwa na Raisi Mkapa na Raisi Kikwete akawageuka na kuanza kuwanyoosha, kama ambavyo Mkapa aligeuka kumnyoosha Nyerere aliyemuweka. Mengine tunamwachia Mungu. Ila naomba ujiulize hili swali:

Hivi wangetenda mema mwaka 1995 tungefika huku leo ? Amini, Amini nawaambia. Kama ilivyokuwa mwaka 1995 vijana kuunda MTANDAO, vivyo hivyo mwaka 2015 vijana wameunda MTANDAO mwingine, tofauti ni kwamba sasa hivi iko MITANDAO MINGI na MIZITO.

Tatu, na mwisho kabisa. Mwanadamu usijifanye MUNGU (Never Play GOD), kwasababu mbali na kuwa na uwezo wa kubadilisha mambo, hakuna mwanadamu dunia hii anayeweza kuzuia mabadiliko (No Man Can Ever Stop Changes). Kama tu mwanadamu hawezi kuzuia ukuaji wake binafsi, sembuse taasisi kubwa kama dola. Hivyo basi, hatuwezi kuzuia mabadiliko ila tunaweza kuyamudu (We Can't Stop Changes, But We Can Manage Them). And how do we manage changes? Through thorough preparations. Sisi kama kizazi kipya inabidi tujifunze na kuangalia ni wapi wazee walijikwaa.

Kama tukiendelea kuamini hizi falsafa ovu ambazo tulizikuta, basi hili taifa halitakuwa na amani kwa muda mrefu. Mbinu ambazo zilitumika kuwashughulikia watanzania milion 10-20 kipindi cha TANU/CHAMA KIMOJA haziwezi kuendelea kutumia kudhibiti taifa la kiutandawazi lenye watu zaidi ya milioni 60, ambao wanaingia na kutoka nje ya nchi kila uchwao.

Zile falsafa za kuamini kwamba watu wa UKANDA FULANI, KABILA FULANI, ASILI FULANI, JINSIA FULANI au DINI FULANI ndiyo wanaotakiwa sana kupewa nafasi nyeti kitaifa huku wengine wa kundi jingine wakibaguliwa wazi-wazi utadhani siyo WATANZANIA, kwamba ni wenye hulka ya wizi na kupendeleana ilhali tunasahau kwamba wako wengi na walitangulia kusoma tokea ukoloni. Ukweli mchungu ni kwamba matatizo yanayotokea hapa nchini hayajaletwa na CHAGGAS, NYAKYUSA AU HAYAS. Ni sawa na ule upumbavu wa kuamini kwamba WASUKUMU wa Raisi Magufuli ndiyo wameleta matatizo, jambo ambalo ukiliangalia kimapana halina ukweli wowote zaidi ya STIGMA and STEREOTYPE.

AU kuamini kwamba WAHINDI na WAARABU ndiyo chanzo cha umasikini wa mtu mweusi, ilhali tunasahau ukweli mchungu kwamba hao WAHINDI waliokimbia Tanzania miaka ya 60's na 70's kuelekea Uingereza na America Kaskazini bado wamefika huko na kuendelea kuwashinda hata hao wazungu na jehuri zao. Jiji la London lina wahindi wengi matajiri wa kutupwa ambao walitokea Tanganyika, Kenya na Uganda. Hili ni jambo linalofikirisha.

Ukienda Marekani, ukakutana na Diaspora wa Tanzania, wengi wao ni Wazenji, Wachagga, Wanyakyusa na Wahaya. Sasa unabaki kujiuliza, hii chuki ilitokea wapi, mbona hata huku kwa wazungu bado hawa watu wanafanikiwa mno. Mwisho unakuja kufahamu kwamba, kuna kitu hawa wenzetu walikifahamu muda mrefu, ambacho hata wengi wakikifahamu watafanikiwa tu.

MUHIMU KUKUMBUKA: Mwaka 2024 kutakuwa na uchaguzi mdogo, Mwaka 2025 uchaguzi mkuu. Mambo yatakayofanyika kipindi hiki yawe mema au mabaya, fahamu kwamba tutaishi nayo miaka mingi sana ijayo, kama ambayo tunaishi na yale ya mwaka 1995, 2005 na 2015. Niseme tu, The Domino Effects of 2015 will be profound and long-lasting. Kazi kwetu watanzania.....

APANDACHO MTU NDICHO ATAVUNA, huwezi panda Magugu ukavuna Mtama.

Niwatakie Usiku mwema...​

Umeanalyse vizuri sana, hakika Mimi namkubali sana Nyerere 95% ila moja kati ya foundation mbaya alojenga ni hii ya ukabila ijapokua alikua sahihi in other side.
Mimi ni mchaga halisi Toka Babu pande zote mbili huko zamaaani, ila wazo la Nyerere kutaka kabila kubwa lisishike nchi, hasa kipindi kile bado nchi ni changa, na tunaimarisha umoja kama taifa ni sahihi. Imagine mpaka leo at least makabila hayo makubwa ndio zaidi yamedominate kwenye fursa kubwa nchini.... Ilihali hata hawakuwahi kuongoza nchi. Sasa Je ingetokea wameongoza nchi ingekuaje na mifumo yetu ilivokuwa mibovu? Nidhahiri tungekuwa kama Kenya saizi na chuki isingeweza kuzimwa Kwa urahisi tungekuwa tunatifuana saizi. Mfano mzuri ni usukuma ulivotaka kuanza kutuvuruga nakuona nchi nimali yakundi...juzi tu hapa. Kama taifa tujitadhmini tulipo nakutafuta suluhu nzuri hasa kujenga taasisi imara, ambapo mtu yeyote pande yeyote aongoze nchi Kwa kigezo Cha kuwa anastahili nafasi hio na SI udini, ukabila au ubara/Zanzibar.
 
Umeanalyse vizuri sana, hakika Mimi namkubali sana Nyerere 95% ila moja kati ya foundation mbaya alojenga ni hii ya ukabila ijapokua alikua sahihi in other side.
Mimi ni mchaga halisi Toka Babu pande zote mbili huko zamaaani, ila wazo la Nyerere kutaka kabila kubwa lisishike nchi, hasa kipindi kile bado nchi ni changa, na tunaimarisha umoja kama taifa ni sahihi. Imagine mpaka leo at least makabila hayo makubwa ndio zaidi yamedominate kwenye fursa kubwa nchini.... Ilihali hata hawakuwahi kuongoza nchi. Sasa Je ingetokea wameongoza nchi ingekuaje na mifumo yetu ilivokuwa mibovu? Nidhahiri tungekuwa kama Kenya saizi na chuki isingeweza kuzimwa Kwa urahisi. Nidhahiri tungekuwa tunatifuana saizi. Mfano mzuri ni usukuma ulivotaka kuanza kutuvuruga nakuona nchi nimali yakundi...juzi tu hapa. Kama taifa tujitadhmini tulipo nakutafuta suluhu nzuri hasa kujenga taasisi imara, ambapo mtu yeyote pande yeyote aongoze nchi Kwa kigezo Cha kuwa anastahili nafasi hio na SI udini, ukabila au ubara/Zanzibar.
Hakuna shida kwa mtu kutamani kuwa raisi wa nchi bila kujali atokea kabila lipi.

Tatizo ni pale huyo raisi mtarajiwa atakidhi vipi matarajio ya wapiga kura na si yake yeye binafsi.

Sasa kama alivyosema mleta mada haya makundi mazito ya mitandao ambayo tayari yapo ndio yamekuwa tatizo kubwa linomkabili raisi yoyote yule.
 
Back
Top Bottom